Kuna daladala zinaonekanaga kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 alfajir

Kuna daladala zinaonekanaga kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 alfajir

Kadi Poa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
2,015
Reaction score
1,005
Wakuu kuna daladala huwa mchana wala asubuhi hauzioni. Unaziona kuanzia saa 6 usiku. Hizi nimekutana nazo sana Arusha unakuta taa moja tu ndio inawaka, sasa usiombe wakati wa kupanda mlima, mbona utaomba poo. Ikifika saa 11 alfajiri hauzioni tena. Sasa sijui huwa wanaziiba gereji.
 
Wakuu kuna daladala huwa mchana wala asubuhi hauzioni. Unaziona kuanzia saa 6 usiku. Hizi nimekutana nazo sana Arusha unakuta taa moja tu ndio inawaka, sasa usiombe wakati wa kupamba mlima, mbona utaomba poo. Ikifika saa 11 alfajiri hauzioni tena. Sasa sijui huwa wanaziiba gereji.
Jaribu kitunga uongo unaofanana na ukweli, daladala Arusha mwisho saa 4 ikizidi sana ni saa 5.
Hakuna abiria usiku kwa Arusha.
Barabara zinazochelewa kufunga kazi ni Ngulelo na Morombo.
 
Japokua sidhani kama arusha zipo gari huo usiku wa saa 6 ila kwa dar hizo daladala tunaita VIBWENGO ni gari ambazo hazina ukamilifu kwenye kulipa bima au mapato so muda wake wa kutembea ni usiku. Pia mafundi gereji huiba gari za wateja wao zilizolala gereji na kwenda kupiga deiwaka.
 
Hakuna tatizo mradi hawaendeshi mwendokasi wala kihuni.

Hatujawahi kusikia ajali ya magari hayo.

Mijini watu hawalali wanatafuta riziki,

Wengine wanatoka kwenye harusi hawana magari ya familia kutokana na uwezo mdogo unazani wanarudije majumbani toka kwenye kumbi za harusi ?

Wengine wanatoka kazi za shift hawana magari binafsi unatemea walale majiani hadi asubuhi?

Wengine wanatoka mahospitalini kuona wagonjwa wao au kupeleka dawa zilizoandikwa na daktari n.k

Wawepo tu mradi wafuate sheria.
 
wabongo noma
 
Hizo gari kwa Dar zinasaidia mno kwa wale wanaochelewa kurudi home. Mfano mwendokasi hazifanyi kazi saa 24, Ikifika saa 6 usiku zinapaki. Hakuna anaetaka kulipishwa 10k kwa boda boda.
 
Back
Top Bottom