Kuna daladala zinaonekanaga kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 alfajir

Kuna daladala zinaonekanaga kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 alfajir

Jaribu kitunga uongo unaofanana na ukweli, daladala Arusha mwisho saa 4 ikizidi sana ni saa 5.
Hakuna abiria usiku kwa Arusha.
Barabara zinazochelewa kufunga kazi ni Ngulelo na Morombo.
Morombo hadi saa 6 zipo
 
I knew it girl...#by the way I'd like to know you better..na wewe hyo night Kali unakuwaga unaenda wap
Ilikuwa long time bana Tena sio Dar.

Zenji.

Kulikuwa Internet Cafe ilikuwa inachelewa kufungwa enzi za Hi5
 
Mi naishi kimandolu Arusha, daladala mwisho saa 5 na hapo za kubahatisha, sasa sijui hizi unazosema zinaenda wapi, kiufupi kusafiri usiku Arusha labda pikipik au private.
 
Kuna nyingine mchana ukizipata gereji ni Kama scrapper ila usiku ni daladala.
 
Ilikuwa long time bana Tena sio Dar.

Zenji.

Kulikuwa Internet Cafe ilikuwa inachelewa kufungwa enzi za Hi5
Oooh as salaam aleykhum ustaadhat karucee
Kumbe na wewe ni kujenga wa dar hotwire...
I knew it kuwa its not now...now una cruze na Mercedes Benz yako kama ile ya mwinyi katika streets za dar
 
Mkuu Sasa si hatry kubwa iyo
Sio hatari mara nyingi mwendo wao huwa ni aste aste sana ili kuokoteza abiria, lakini pia sababu usiku kama huo wapinzani sio wengi ko wanajaza fasta gari zao.
Kingine mkuu wanatuokoa na vibaka na gharama za uber,bort na bodaboda ambazo huwa kubwa mnoo, wakati daladala izo ni 400 tu.
 
At the end of the day kila Mtu lazima aende Choo
mjlol.png
 
Wakuu kuna daladala huwa mchana wala asubuhi hauzioni. Unaziona kuanzia saa 6 usiku. Hizi nimekutana nazo sana Arusha unakuta taa moja tu ndio inawaka, sasa usiombe wakati wa kupamba mlima, mbona utaomba poo. Ikifika saa 11 alfajiri hauzioni tena. Sasa sijui huwa wanaziiba gereji.
Zina Kazi kubwa Mbili 1. Kubeba Malaya, Walevi na Vibaka wa Usiku na 2. Kuwakwepa Matrafiki kutokana na Ukangafu ( Ubovu ) uliotukuka wa hayo Magari ( Mabasi )

Na mara hata wanayoyaendesha huwa ni Mafundi Gereji ambapo wakiwa wanayaendesha pia huwa wanakuwa wanayasikilizia pabovu wapi na wakienda Kuyalaza Asubuhi wanaanza Kuyatengeneza tena na yapo sana Gereji Bubu za Mikoa ( Miji )

Na Sifa Kuu ya Magari ya Usiku Mikangafu ( Mibovu ) ni Kuwaharibikieni popote pale na ukidai tu Nauli kwa Kondakta utakachoambulia ni Matusi ambayo tokea Mama yako Mzazi akulete hapa duniani hujawahi Kuyasikia.

Halafu yote tu ukibahatika Kuyapanda nyakati za Usiku kukutana na Panya, Mende na Mijusi mkiwa mnasafiri nao Wote ni jambo la Kawaida mno huku Madereva wake wengi Spana zao huwa wanaziweka standby katika ' dashibodi ' na Makondakta wake wengi huwa hawakai mbali na Madumu ya Kujaza Mafuta kwakuwa Mabasi haya ya Usiku kuzimika mara kwa mara ni sehemu ya Miiko yao.
 
Ferry -kkoo
Gari nje la njano kama school bus.
Linawaka taa moja Tu
 
Wakuu kuna daladala huwa mchana wala asubuhi hauzioni. Unaziona kuanzia saa 6 usiku. Hizi nimekutana nazo sana Arusha unakuta taa moja tu ndio inawaka, sasa usiombe wakati wa kupamba mlima, mbona utaomba poo. Ikifika saa 11 alfajiri hauzioni tena. Sasa sijui huwa wanaziiba gereji.
Hizo ni za tia maji x 2!😂😂😂! Daladala ya namna hiyo inayotembea ikilalamika na kutetemeka ka teja, nilipanda mara moja 2005 kutoka fire baada ya kikao kilichoahirisha mgomo wa madaktari kilichofanyika ukumbi wa korea kuisha saa nane usiku! Nilikutana na hiyo daladala inaendeshwa na teja na conda teja! Ina'vibrate' mwanzo mwisho! Sofa zimenyofokanyofoka! Ila nashukuru Mungu ilinifaa sana usiku huo kuniacha shekilango😜!
 
Wakuu kuna daladala huwa mchana wala asubuhi hauzioni. Unaziona kuanzia saa 6 usiku. Hizi nimekutana nazo sana Arusha unakuta taa moja tu ndio inawaka, sasa usiombe wakati wa kupamba mlima, mbona utaomba poo. Ikifika saa 11 alfajiri hauzioni tena. Sasa sijui huwa wanaziiba gereji.
Hahahaha
 
Back
Top Bottom