Kuna delutional theory imesambaa kwenye jamii zetu za kiafrika kwamba kuoa kunafungua milango ya mafanikio

Mzee mmoja aliwahi niambia "ukitaka kuishi na mwanamke feminism vaa miwani ya mbao, pili kuna muda lazima uwe bubu au kiziwi Sijui alimaanisha nini
Kwa kifupi ni kwamba hawana utiifu na ile womanhood kama waliokua nayo wanawake wa zamani, kwaiyo anachotaka kumaanisha ndugu yetu wanaume tuzishushe standards zetu ili kwenda nao sambamba
 
Ni lini wanawake mmeanza kutusemea wanaume? Mnafikiri hatujui mkitumwagia misifa iyo ni ishara ya hatari?
 
Mfumo mzima wa ndoa katika ufanyaji kazi wake na endapo ndoa ikifika tamati ni kandamizi kwa mwanaume., hivi kwanini mnataka mambo rahisi kueleweka yaonekane magumu
 
Ukioa mke sahihi/mwema ambaye anajua nini maana ya ndoa,anajua maana ya maisha ,anajua umuhimu wa familia na mume ktk maisha yake, anayeijua nafasi yake kwenye nyumba na mwenye hofu ya Mungu,lazima milango ya baraka ifunguke.Ila baraka wengi wanaitafsiri ktk hela,sometimes mnaweza mkawa na kipato cha kawaida huku maisha yenu yakawa yamejawa furaha na upendo.

Changamoto ktk kizazi hiki cha sasa kumpata huyo mke mwema ni shughuli tena si ya kitoto.
 
Ninyi ndio (foolish principal -FP)wapumbavu waandamizi.tupe mifano ya matajiri Tanzania ambao hawajaoa.
 
Ubarikiwe sana
 
Kuna wazee wanawajaza sana ujinga vijana wanawahamisisha waoe na ukiangalia uchumi wao haueleweki eti mke anakuja na baraka

Wanawaambia utakachokula ndio hichohicho atakula mkeo

Sasa ugali wa mtu mmoja ni sawa na wa watu wawili?

Vijana tengenezeni uchumi kabla hamjaoa la sivyo mtawarithisha watoto wenu umasikini
 
Mfumo mzima wa ndoa katika ufanyaji kazi wake na endapo ndoa ikifika tamati ni kandamizi kwa mwanaume., hivi kwanini mnataka mambo rahisi kueleweka yaonekane magumu
Hii conclusion wewe unaitoa wapi ikiwa bado hujaoa?Baba yako na mama yako bado wanaishi wote mpaka leo kipi kinakufanya kuanza kuwaza maisha ambayo huyaishi wala hujawahi kuyaishi huku kuna ambao wanayaishi na hawana habari?

Bold ndogo,kwa sababu tuna akili kuwazidi,that's it!
 
Unajuwa Mtume Mussa alipokuwa na shida tena ugenini, aliomba nini akapewa nini na Mwenyezi mungu?
 
Natamani nijue umri wako mpaka sasa ni miaka mingapi na hayo unayoyaita maisha umeyatengeneza kwa kiwango gani wakati ukizisogelea siku za kuoa ili wanao usiwaachie umaskini!

Kwa sababu baba yako alijitengenezea maisha mapema wewe ulikulia mboga saba eti?na leo kila mmoja hapo nyumbani anaweza akapewa nyumba yake biashara akasoma anakotaka siyo?acheni masihara maisha siyo maigizo wazee hahah
 
Hebu tuambie rafiki, wengi hatujui aliomba nini Nabii Mussa Salaam?
Qur'an 28:24. Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayo niteremshia. 24

Dua hiyo ilijibiwa kwa Muumba wetu kumpatia Kazi, mke na pakuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…