Kuna delutional theory imesambaa kwenye jamii zetu za kiafrika kwamba kuoa kunafungua milango ya mafanikio

Soma uielewe paragraph ya kwanza
 
Soma uielewe paragraph ya kwanza
Umezungumza kitu kama “hao wazee wanaowashauri vijana waoe maisha yao nao ni mabaya kwa maana kuoa kungekuwa kunarahisisha maisha wasingekuwa maskini bado kama walivyo” ukiunganisha na ulivyomaliza pale chini ndipo hoja yangu iliposimama.

Kwamba wewe binafsi upo ktk hatua gani kwanza kiumri,kimafanikio huku ukimuiga baba yako tajiri mwenye tofauti na hao wazee uliowataja hapo juu?
 
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;Ndivyo mema yatakavyokujia,Ayubu.22:21...
 
Uelewa wako ni mdogo sana umekimbilia kupanick
 
Kama unaoa we oa tu, lakini mtu asikudanganye eti ndo utafanikiwa, Kama huna hela ndo utazidi kuwa masikini, ukipewa ushauri, Angalia kwanza na Hali yako, mtu asikupe nadharia ya zali, Duniani hakuna zali, mafanikio yanatokana na juhudi, hata maandiko yanasema hivyo.

We pambana ukipata hela, Kama unaona utaifirahia ukiwa na familia we oa tu, mbona Kuna watu hawana hela lakini wanatamani kutimiza ndoto ya kuoa? Kwani hakuna masikini wenye furaha?

Fanya ile kitu moyo unaipenda. Oa, tafuta pesa enjoy!
 
Kuna ambao wanaanza pamoja kutoka Chini, hao ni wengi pia
Katika iyo safari mwanamke alichangia nin? mtaji? ujuzi wa kitaaluma? connection ya kazi?.. usiniambie mchango wake ni sex na kupika chakula, huduma ambazo mwanaume anaweza kuzipata bila hata ya uwepo wa uyo mwanamke kwenye maisha yake.

Wanawake wa hivyo wengi huwa hawana options kwaiyo anaamua kujishikiza tu kwa mwanaume ili aje kujipa entitled kwenye mafanikio ya uyo mwanaume uko mbeleni.
 
Unanyimwa unyumba kwa sababu ya makosa yenu wenyewe.
Na ikithibitika umechepuka umekwisha kabisa.
Mchepuko hana nafasi kwenye mali za watoto. 😅
Kwa hii comment yako bado kuna watu wanabisha kwamba ndoa sio utumwa kwa mwanaume.

Embu tu-switch upande, ikithibitika mwanamke amecheat au amembambikia mtoto mumewe je sheria inamuwajibisha vipi huyu mwanamke?
 
Na hicho ndicho ninachowaambia watu hapa., mafanikio ni suala subjective ambalo halina connection ya moja kwa moja na ndoa labda uoe kimkakati from the first place, kama injia alivyooa kwenye familia ya gsm
 
Hoja yako ni nzuri ulichokosea ni kitu kimoja haujaclassify generation ipi ya ndoa? Maana ndoa za zamani zimedumu na zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno hata sisi wengine ni product za hizo ndoa ni kwasababu wazazi wetu kila mmoja wao anajua jukumu lake na hata mafanikio yenyewe yamechangiwa na uimara wa mama zetu bila kupepesa macho unaona kabisa. Wewe ulitakiwa ujikite kwenye hii generation ya wanawake wa sasa je wana quality kama za mama zetu hawa je ni productive wanastahili kuolewa? Wanamchango wowote? Maana unaweza ukapingwa na watu kwenye uzi wako kumbe unayepingana nae ni wa kizazi cha Zamani na ndio waliobahatika kupata wanawake wa maana mfano mzuri Grahams
 
Kwa hii comment yako bado kuna watu wanabisha kwamba ndoa sio utumwa kwa mwanaume.

Embu tu-switch upande, ikithibitika mwanamke amecheat au amembambikia mtoto mumewe je sheria inamuwajibisha vipi huyu mwanamke?
Siku zote chanzo huwa ni nyie, hawezi chepuka bila sababu yoyote ile ilhali alikupenda na akakubali kuolewa na wewe
 
1. Kuchepuka
2. Ulevi kupindukia
3. Kuchelewa kurudi nyumbani
4. Kuzaa nje ya Ndoa
5.Dharau
Ukiyachoka hayo mwanamke unadai talaka na mwanaume atawajibishwa kwa kupoteza sehemu ya mali zake ambapo unapewa wewe kama compensation ya muda na mchango wako kwenye iyo ndoa.

Sasa tubadilishe upande mwanamke ndie umechepuka, mlevi, unachelewa kurudi nyumbani, umebeba mimba nje ya ndoa na mwanaume anataka mtalakiane je sheria itakuwajibisha vipi wewe mwanamke?
 
Ni kweli lakini pamoja na sifa za huyu mwanamke uliemuongelea hapa tusisahau kwamba hisia zinabadilika, sasa huko mbeleni mwanamke huyu akikengeuka?

Tusisahau kwamba taasisi ya ndoa inalinda masilahi ya mwanamke haina time na masilahi ya mwanaume.

Kwaiyo bado tunarudi pale pale kwamba mfumo wa ndoa ni kandamizi kwa mwanaume
 
Achaneni na hizi fikra za kizamani, kama nyie mliingia kwenye ndoa blindly tu msifikiri na sisi tunatafanya ivyo ivyo.

Lazima kwanza tuziangalie hasara na faida tukiwa nje ya ndoa. Kwaiyo pale tunapozi-point hasara za ndoa tulieni.

Kizazi cha vijana wa sasa sio sawa na kizazi chenu ambacho mlikua mnaingia tu kwenye ndoa kichwa kichwa kama nyumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…