Ni kweli watanzania walo wengi hawaijui katiba iliyopo nikiwemo mimi mwenyewe.
Lakini ninafahamu kuwa kila jambo lina faida na hasara pia.
Sitaki kuongelea sana hasara inayotokana na huu ujinga (kutojua katiba) wetu.
Faida moja kubwa ya huu ujinga ni Amani na Utulivyo tulionao watanzania.
Nachelea kusema siku ujinga huu ukitutoka,naamini ndio itakuwa mwisho wa Amani na Utulivu tunaojivunia kama Watanzania.
Kwa mantiki hii,nadiriki kutamka wazi kuwa hili swala la kutuelimisha kuhusu katiba kama hatua ya awali ya kupata katiba mpya lisingefanyika kwa sasa.
Kwa maoni yangu, tatizo kubwa tulilonalo kama Taifa limejikita kwenye Uongozi.
Kama nchi, matokeo ya mfumo wa namna viongozi wanavyopatikana na mfumo wa uwajibikaji wao ndio kiini cha mahitaji ya Katiba mpya.
Sasa nini kifanyike?
Mimi naona Watanzania tusipiteze muda na pesa nyingi kutafuta katiba mpya.
Iliyopo inaweza ikatufaa sana kama itarekebishwa na kutengeneza mifumo bora ya namna ya kupata viongozi.
Hilo ni la kwanza.La pili ni kurekebisha mifumo ya namna ya kuwajibishana.
Isiwepo watu au viongozi walio juu ya sheria kwa maana ya kutoweza kushitakiwa Mahakamani.
Kwa mantiki hii,vyombo vya kutoa haki viwe huru kwa asilimia 100.
Tatu, swala la Haki na usawa miongoni mwa Watanzania liwekewe mifumo ambayo haina mawaa.
Swala sasa linakuwa,je ni nani atamfunga paka kengele?
Je, Watawala watakubali kujikata koromeo?
Majibu sahihi ya haya yakipatikana, hakuna haja ya kuhangaika na michakato mirefu ya kutafuta katiba.mpya.
Nadhani waliosoma Cuba wamenielewa.