Kuna faida gani kumpaka mtoto aliyezaliwa damu ya uzazi?

Kuna faida gani kumpaka mtoto aliyezaliwa damu ya uzazi?

Kuna baadhi ya mama huwapaka watoto wao damu inayotoka ukeni punde baada ya kutoka kujifungua.

Kwa nilivyosikia hii kitu ipo sana kwenye jamii ya Watutsi.
Wanasema punde mama anavyokabidhiwa mtoto wake basi hufanya kitu hiki huku akinenea maneno.

Inasaidia mtoto asipate husda yoyote inayosababishwa na walimwengu.
Watu waliofanyiwa kitu hiki huwa hawarogeki, wengine wanakua na nyota kali sana.
Chochote kibaya kinachowapata labda akisababishe mwenyewe ila sio kwa kusababishiwa na watu.

Hii ishu nimeisikia mara mbili, na jamii hizo hufanya jambo hili kwa siri ndio maana sio kila mtu anajua kuhusu hii mila au desturi.

Nikaona nije kuuliza humu sababu kuna wajuzi wa mambo.
Naomba kujua ukweli wa jambo hili.
Mshana Jr LIKUD GENTAMYCINE mdukuzi ngara23 Kapeace
Na wewe unataka ufanye hivyo? Kama hao watu si.
 
Unamuamini mtu wa Kwanza ( Nesi/ Mkunga sijui ) anaebeba mtoto wako na kukukabidhi ?
Unajifunza Nini juu ya vilema wanavyozaliwa navyo watu ?

Unajifunza Nini wazee wanapokuambia bariki chombo kabla hakija beba mzigo ?.

Maneno ya wazee hayaanguki hovyo Kama embe bovu.
 
Back
Top Bottom