Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

Sio sera, bali ni uongozi.

Dubai hawakuwa na kitu, ila uongozi umewafikisha walipo. Tanzania na nchi nyingi za Africa zina kila kitu yet ni maskini.

Uongozi bora na makini hutengeneza sera zilipo bora na huondoa sera zilizo mbovu.
Uko sahihi kabisaa. Ingawa hawa viongozi ndiyo huongoza utungajibwa sera. Kwa mfano, Sasa hivi kuna mchakato wa kutengeneza dira ya nchi tazama jinsi mchakato ulivyo. Nilitegemea time ya mipango ndiyo wawe mbele zaidi ya wanasiasa lakini ngoja uone.
 
Nimeona Rais wa Kenya Ruto amefuta visa entry requirement kwake.

Kuna faida yeyote ya kiuwekezaji?

Je dola 20 au 50 zilikua kikwazo kuingiza watu nchini?

Kwamba kuna wawekezaji serious walishindwa kwenda Kenya kwa kukosa dola 30?

Hii kwangu naiona kama njia ya kukaribisha magaidi nchini Kenya na sio njia au jambo zuri la kuiga Tanzania? ukifanya hivyo, kesho uhamiaji watajaa wasomali maelfu kwa kigezo cha utalii tutaingiza magaidi nchini.
Utalii na biashara.
 
Tanzania umeona ni nchi ya maana Sana mkuu
Mimi nikipata chance ya ku escape hichi kijiji cha wachawi ambacho ukfanikiwa tu watu wanakesha juu ya dari lako kukuwangia nasepa fasta.

Wabongo nuksi
 
Sio nchini Kenya tu nasema hivi huweza kuzuia watu kuzunguka kwenye ardhi hii hata uweke ukuta wa Trump

Wataingia tu, haya ni yenu tu kusema Wasomali magaidi ila hujui nani anashikilia Uchumi wa Kenya kwa sasa
Tembelea huko uone biashara zao na apartments wanazoshusha mpaka mkikuyu anaomba maji kwao apoze roho

Hapa [emoji636] nawaona Wahabeshi kila leo wanaingia na wanapita Tz mnawakamata wanahonga wanakuja huku kama wakimbizi
Nyie mmekalia ooh usalama
Kuna akili
 
Faiza usalama sio priority comrade?
Si amesema Rais wa Kenya akila anaekuja atakuwa verified na kupewa certificate.

Ni mfumo tu umebadilika lakini usalama yutazingatiwa kama kawaida.

Mbona Tanzania hatuhitaji visa kuingia Afrika Kusini na nchi nyingi tu nyingine. Kenya wameamuwa zote.

Rutoi ni mjanja sana, anataka aadae aitumie hiyo ili raia zake watoke kwa wingi kwenda kutafuta kazi nje ya Kenya, Kenya haina uwezo wa kuzalisha ajira kwa wingi kuwabeba wote.
 
Back
Top Bottom