Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

Maga
Magaidi wakitaka kuingia wanaingia tu,kwa hiyo USD 20 inazuia gaidi
 
Mtego tu huo kwa Tanzania, hamna lolote.
 
Nimeshangaa sana, kikubwa hapo ulinz mipakani uimarishwe, ukaguzi uwe mzuri watu wasiingie na madawa ya kulevya na Silaga hatari bas,
 
Nadhani na sisi tuondoe vikwazo vya visa kwa nchi zote za Africa isipokua zenye usalama mbovu wa raia wake.
Hii italeta chachu ya maendeleo.
Ila serekali iwe makini na kuongeza ufuatiliaji.
 
Magaidi wanashindwa kulipa hiyo dola 30. Huna hoja
 
Tatizo sio visa fee but usumbufu wa kuipata. Wana maswali ya kipumbavu zaidi ya majaji wa bongo star search!
 
Kusema hivo unamanisha mustakabali wa maisha yetu upo kwa mataifa makubwa na sisi hatuna la kufanya.
Mkuu hapo kuna masuala mawili umechukua moja mkuu wangu.
Ni katika kubadilishana mawazo tu, nature ya viongozi wa africa, ufisadi, ulafi wa madarakA, ubabe, n.k unafikiri watakubaliana wenyewe kwa wenyewe?

Pili si suala la kuamuliwa na Mataifa makubwa, kwa picha kubwa ukitazama unafikiri wanaweza kubali?
 
(1)-Kenya wana uzoefu na magaidi,kule Mombasa Kenyatta kafweka masheikh ndugu zao na hawa wa UAMSHO akina Rogo hivyo lazima kuna T&C apply.


(2)-Pamoja na yote lazima hii fungulia mbwa itaathiri hadi usalama wa majirani hebu fikiria hivi sasa wahabesh wanakamatiwa Tz mamia na wamepita Kenya yenye kuhitaji Visa na hawana documents zozote.
 
Sisi sote ni watu na tunatakiwa kuishi na kufanya shughuli zetu kwa kufanya interaction freely,hii mipaka ni ya kikoloni yenye lengo la kutugawa , kututawala na kutunyonya.Hizi hoja za akina fulani watajaa huku ni hoja za uoga na umaskini.

Wakoloni? Mbona na wao nchi zao zina mipaka! Na wao wanataka kunyonyana? Kwani wao mipaka yao iliwekwa na nani? Sijaielewa hii hoja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…