Shukran mkuu. Short answer: Hapana.
Naweza kusema kuwa asilimia zaidi ya 90 -95 ya nyumba za kawaida za kuishi hazihitaji architect. Jamii imejaa mafundi wazuri na uzoefu wa kutosha wa tangu enzi na enzi uliorithishwa kwa vizazi vingi. Wakijenga vizuri, nyumba inakaa miaka nenda rudi mpaka wanarithi wajukuu.
Kwa makazi, Architects wanahudumia about 5% tu ya watu, haswa wale wanaohitaji kitu cha kipekee chenye hadhi na utambulisho wake wenyewe. Humu utakuta mpaka 'starchitects' wenye 'identity' na 'style' zao zinazopendwa mpaka kujitengenezea following kiasi kwamba nyumba zao walizodesign ni investment kwa clients wao. Mtu ananunua plot, anadesigniwa nyumba ya mabilioni na starchitect, baada ya miaka michache anaiuza kwa faida na mnunuzi anaiuza tena kwa faida and it goes on. Ni kama high end art. Levels hizo, Mtu hataki nyumba tu, anataka nyumba ya architect fulani just like mtu mwingine hataki nguo tu, zipo kibao mtumbani, bali anataka haute couture, range fulani ya Louis Vuitton ya Pharrell. Hii ndiyo ndoto ya Architects wengi.
Ila kwenye mahospitali, skyscrapers, airports, mipango miji, marinas, hotels, na mambo kama hayo, ni muhimu kuwa na architect.