Kuna faida zozote za kumtumia Architect? Ama ni kupoteza pesa tu?

Kuna faida zozote za kumtumia Architect? Ama ni kupoteza pesa tu?

Hivi architect aweza kamilisha kazi remotely? ama ni lazima afanye physical (site) visit?

Maana naona online kumejaa architects kibao wanajitangaza... unamueleza unachotaka, mnaafikiana malipo, anakuchorea ramani complete + mihuri, anakutumia popote ulipo, then mtu anaanza ujenzi.

Hii mkuu imekaaje? remote archtectural drawings pasipo mtaalamu kuivisit site.
Best way ni kutembelea site.

Hili huwa ni gumu Kwa sababu ya gharama. Hapa TZ, Watu wachache sana wanaweza au wako tayari kumgharamia architect atoke mkoa mwingine aje site kuingalia na kuanza kudesign. Kuna wasiotayari hata kumgharamia architect aliyeko ndani ya 20km radius na site ilipo.
Hivyo architects wengi wanalazimika kuadapt na Hali halisi na kutegemea kuwa mafundi au maengineer walioko site watajua namna ya kufanya wakati wa ujenzi.
 
Kumbe inategemea na utayari wa mteja mwenyewe kugharamika. Na kweli wabongo wengi tunataka mambo mazuri ili ni wazito to make things happen.
 
Architect kazi yake inaweza kuanzia site na kuishia mezani.

Site engineer ndio anasimamia vision ya Architect, anasoma kilichochorwa na kukitafsiri kwenye uhalisia wake.

Ahsante mkuu kwa ufafanuzi murua.
 
actually sheria za kwetu hapa haziruhusu kujitangaza kwa taaluma ya architecture kama ilivyo udaktari

lakini sbb ya social media boom, vijana kumaliza shule bila kupata after school
training, njaa na changamoto za kipato basi hadi wasio na fani wameingilia shughuli, wengi insta pia sio architects lakini wana pose kama
architects. ni wafanyabiashara yani madalali.

kabla ya kufanya design ni vyema architect apate taarifa za kutosha za site kama vipimo sio kwa meters bali hata geometry, slope/topography ya uwanja, miundombinu iliyopo, majirani wamekaaje kaaje, njia za kuingia na kutoka, kama ulivyosema awali sun path and winds direction, aangalie kama kuna hatari yoyote kama water table kua juu, aina ya udongo nk.. AFIKE site! na kwa mtalaamu
sahihi anaweza fika site na kukushauri hata musijenge hapo labda kwa changamoto atakazoziona, au swala la uchumi kwa jinsi site ilivyo kama steep slopy sites.

na kwa project zinazopitia due process basi kuna vitu vingi zaidi wanapima kwa utaalamu zaidi mfano topographical and cadastral survey, geotechnical investigation nk!

ukienda insta utapelekwa ki insta insta “tunatuma na mikoani”

So mtu atumie mbinu zipi ili kupick-up an architect ambaye ni real professional na ana uzoefu wa kazi? What criteria to look at when searching an experienced professional architect?

Maana ni kweli huko insta kumejaa architects wa kila bei, hawaachii pesa 😄. Ni vurugu mechi!
 
kwenye hatua za muhimu kama setting ya msingi tumia architect ambaye ndyo mchora ramani wako, pia unaweza kumshirikisha kwenye stages tofauti mf kuezeka, kujenga uzio na finishing ya nyumba
 
Kumbe inategemea na utayari wa mteja mwenyewe kugharamika. Na kweli wabongo wengi tunataka mambo mazuri ili ni wazito to make things happen.
Yes mkuu. Wengi hawataki kuingia gharama. Chochote anachoweza kukwepa, atakikwepa. Kina fundi Maiko na maduka ya hardware huwa ndiyo wanafaidi.
 
Wakuu,

Katika hatua za awali kabisa za kuanza ujenzi, kuna faida gani kumtumia Architect (msanifu ujenzi)?

Ama ni wastage of money na hamna ulazima?
Nimeanza ujenzi wa apartments zangu saba in one compound nachoweza kusema architech ni watu muhimu sana kama unataka nyumba idumu muda mrefu nje ya hapo unatafuta hasara ya pesa utakazojenga na kuwekeza kwenye ujenzi.
 
Hahaha sawa mkuu. Kwahiyo kwa fundi mzoefu, hamna haja ya kupoteza pesa kwa architect?
Kuwa na architect inategemea sana na ukubwa wa mradi wa ujenzi ulio nao mara nyingi ukiwa na kagorofa kamoja au jengo lolote dogo kuliko hilo unaweza mtumia fundi mchundo au ( technician) wale walio soma dit, must au atc kwa sbb unaweza pata vitu zaidi ya kimoja kwa garama nafuu zaidi kuliko garama kubwa za professional architect maana hawa fundi michundo ramani wanachora, design wanajua ( although basic design), na boq atakuandalia na mradi atausimamia

Note. Kuwa na mtu professional anayeelewa procedures za ujenz ni muhimu katika miradi kwa sbb hawa mafundi wanajua na wana uzoefu ila wana negligence fulani wakipenda kutumia uzoefu wao zaidi kuliko procedures zinatakaje maana ni muhimu kufwata procedures na proticol kuliko kurely kwny uzoefu wa mafundi pekee
 
kwenye hatua za muhimu kama setting ya msingi tumia architect ambaye ndyo mchora ramani wako, pia unaweza kumshirikisha kwenye stages tofauti mf kuezeka, kujenga uzio na finishing ya nyumba

Thanks Missy.
 
Yes mkuu. Wengi hawataki kuingia gharama. Chochote anachoweza kukwepa, atakikwepa. Kina fundi Maiko na maduka ya hardware huwa ndiyo wanafaidi.

Sawa mkuu. Kwa kazi yenye quality, architect ni muhimu.
 
Nimeanza ujenzi wa apartments zangu saba in one compound nachoweza kusema architech ni watu muhimu sana kama unataka nyumba idumu muda mrefu nje ya hapo unatafuta hasara ya pesa utakazojenga na kuwekeza kwenye ujenzi.

Hivi Architect anaishia kwenye uchoraji wa ramani pekee? Gharama ya architect (kuivisit site na kuchora ramani) inarange kwenye kiasi gani?
 
Uhalisia wa Architecture ya bongo...

Architects wetu wa kibongo wanalalamikiwa sana kuwa ni wababaishaji na kazi zao ni unprofessional. Kama ni kweli, kuna umuhimu wa kuwatumia?
Kila sehem kuna wababaishaji hata wewe hapo ni mbabaishaji. Sasa kama wewe ni mbabaishaji haimaanishi familia yako yote ni wababaishaji kama wewe.
 
Back
Top Bottom