Kuna familia kweli hapa mjini DSM hawajui makande?

Kuna familia kweli hapa mjini DSM hawajui makande?

Sijasoma uzi lakini nikuhakikishie tu kuna kabila kabisa hawajui makande.

Kama unawajua Wamwela basi hao watu hawajui kitu makande wala vyakula vya kuchanganya changanya. Na hata ukipika huwa wao siyo wapenzi sana wa kuvila (japo inatokea mara nyingine mwingine anatokea kupenda na kutamani uandae kila siku)

Niliwahi kuwauliza kwanini hampendelei vyakula hivi wakasema wanaona kama ni uchafu hivi (kinyaa) kama vile wengine waonavyo kinyaa vyakula vya Wasomali au rosholoo ya wamasai.

Vyakula vya kuchanganya mfano maboga na maharage au punje za mahindi mabichi, mlenda wa kutwanga (kikwetu tunaita wa kubunda) na maharage na vyakula vingine vingi!!! Hata pilau kwa wengi wao hawalijui na kama wanalijua basi hawajui kulipika na kama wanajua kulipika basi hawapendelei kulipika.

Tukipika makande wanashangaa sana na ukiona mtu anayajua basi alitembea nje na kwao. Hapo nimeongelea kwa hawa waliopo vijijini zaidi naomba nieleweke
 
Makande tunakula nyumbani sio boarding, la sivyo Wapare wote wako boarding!
Ni malezi ya hovyo, kuna ambaye amezaliwa na kujua kila aina ya chakula? Si unaonja kidogo. Hata wazungu wanaofikiri ndio wanawaiga hawako hivyo.
Kweli mkuu,niliwahi waona wazungu wakinunua vibama huko mbeya.Makande yanapikwa sana na mama ntilie Dar, inamaana hata kujichanganya magengeni Hamna.
 
Si bora hao wa makande kuna lidada la kwenda chuo kabisa halijawahi kuona viungo vya pilau..eti kuona mara ya kwanza maswali tele ndo nini hayo meusi akidhani dawa ya mganga😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Cha ajabu nini hapo?
Wazazi wamezaliwa DSM, watoto kazaliwa DSM, kakulia DSM, anasoma DSM hata boarding hajui.
Sasa makande atapishana nayo barabara gani?
Wadau nimeona hili niwape huku na ninyi mpate kushangaa kama Mimi

Leo tulipata ugeni nyumbani kuna rafiki yangu jirani yangu anakaa Masaki alinipigia simu nimtafutie kiwanja huku Kigamboni nikapambana nikapata

Leo amekuja kukagua sasa kaja na wanae wawili mmoja miaka 16 mwingine kama 9 hivi, baada kukagua wamekipenda kesho ataenda benki kulipia sasa muda ukawa umefika wa chakula cha mchana

Tumepita home apajue tukakuta Dada ameandaa lunch nikawaribisha ndani basi tukaanza kupakua chakula, wale watoto wanaongea kizungu mie sikujua lakini baba yao ndio akaniambia aisee hawa madogo awali ngoja nipige Mimi hizi kande chap chap (ni chakula mahindi wanachanganya na maharage)

Basi ikabidi tuwatafutie soda jamaa akasema hicho chakula hawakijui na wala hawajawahi kukiona aiseee nikasema kuna watu wanaishi aisee kumbe kuna nyumba hazijui kande.
Wanaume wa dar wao ni chips na fanta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo mitoto imelelewa vibaya na baba yao anawaendekeza, hata kama hukijui chakula utajaribu kula. Maharage wanayajua na mahindi wanayajua...nini kiliwashinda kula hata kidogo kuonja? Pambav kabisa...ingekuwa wamepelekwa marekani wakakuta makande ungeona jinsi wanavyofakamia
 
Si bora hao wa makande kuna lidada la kwenda chuo kabisa halijawahi kuona viungo vya pilau..eti kuona mara ya kwanza maswali tele ndo nini hayo meusi akidhani dawa ya mganga[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ha haaa huyo ni mke wa mtu mtarajiwa, kazi ipo
 
Makande siyapendi kabisa. Huku kwetu ni chakula cha msibani na siku hizi wameacha kuyapika. Tena bora kidogo za mahindi mabichi.
 
Kande ni chakula katika baadhi ya mikoa tu na si Tanzania nzima huwezi kufananisha na ugali. Mie makande nayasikia tu. Pyaar

Mie mara ya kwanza kula kande ilikuwa shule aisee, mwanzoni nilipata tabu kidogo ila nilivyozoea nikawa nayapiga haswa haswa! Sema hayajawahi nimalizia muda wangu.
 
Kwa kuwa ni dar es salaam sawa. Raiti kama watoto hao wangekulia Mbeya, walahi kande wangezijua na kuzipenda ile mbaya.
 
Makande siyapendi kabisa. Huku kwetu ni chakula cha msibani na siku hizi wameacha kuyapika. Tena bora kidogo za mahindi mabichi.
Bila shaka kwenu ni Arusha.
Ni kwamba hujawahi kula makande yaliyopikwa vizuri.
Mimi nayanogesha kwa sukari na blueband[emoji3][emoji3], ki-boarding school zaidi
 
Binafsi napenda makande, hata leo mchana nimekula. Hata wakisema ni chakula cha kimasikini fureshi tu, maana angalau nakula.
 
😂😂😂😂😂😂😂
Si bora hao wa makande kuna lidada la kwenda chuo kabisa halijawahi kuona viungo vya pilau..eti kuona mara ya kwanza maswali tele ndo nini hayo meusi akidhani dawa ya mganga😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Makande nilianza kula boarding nyumbani hakujawahi pikwa makande
 
Back
Top Bottom