Mimi sitaki yawekwe sukari, yakitiwa nazi tu inatosha.Nitashangaa mtu asipokula ugali.
Hao madogo hawali kande au hawajawahi kula kande.
Kutokuwahi kula kitu haimaanishi huwezi kula. Maana yake hapo ndio wangeanza kujifunza na huenda wangezipenda.
Napenda sana haya madude tena niyatie sukari, nipate na chai.
Makande ni chakula cha asili baadhi ya makabila, hivyo usidhani kila jamii, makande wanayajua.Miaka 16 ujui kande kaka
Mie mwanangu hadi kafikisha miaka 6ndo kaja kuyaona makande na ni watu wwnye maisha ya kawaida kabisa ya mtanzania ila tu siku zote hakuna mtu anawazaga makande..tunawaza ugal ndizi lakn siyo makande kwasabu siyo utamaduni wetu..sishangaiWadau nimeona hili niwape huku na ninyi mpate kushangaa kama Mimi.
Leo tulipata ugeni nyumbani kuna rafiki yangu jirani yangu anakaa Masaki alinipigia simu nimtafutie kiwanja huku Kigamboni nikapambana nikapata.
Leo amekuja kukagua sasa kaja na wanae wawili mmoja miaka 16 mwingine kama 9 hivi, baada kukagua wamekipenda kesho ataenda benki kulipia sasa muda ukawa umefika wa chakula cha mchana.
Tumepita home apajue tukakuta Dada ameandaa lunch nikawaribisha ndani basi tukaanza kupakua chakula, wale watoto wanaongea kizungu mie sikujua lakini baba yao ndio akaniambia aisee hawa madogo awali ngoja nipige Mimi hizi kande chap chap (ni chakula mahindi wanachanganya na maharage).
Basi ikabidi tuwatafutie soda jamaa akasema hicho chakula hawakijui na wala hawajawahi kukiona aiseee nikasema kuna watu wanaishi aisee kumbe kuna nyumba hazijui kande.
Mbona watu wa ajabu sana, malezi ya hovyo kivipi sasaMakande tunakula nyumbani sio boarding, la sivyo Wapare wote wako boarding!
Ni malezi ya hovyo, kuna ambaye amezaliwa na kujua kila aina ya chakula? Si unaonja kidogo. Hata wazungu wanaofikiri ndio wanawaiga hawako hivyo.
Hahaa ..Ngararimo, umenikumbushia mbali sanaUkiwapa yale mahindi yasiyokobolewa (ngararimo) sijui watasema nini.
Kesho unaoa na kusema ni mke wa shida na raha, sawa.