Kuna familia kweli hapa mjini DSM hawajui makande?

Kuna familia kweli hapa mjini DSM hawajui makande?

Msio wakulima makande kwenu ni tabu kbisa kuna aina na aina za makande
Kande za maziwa
Kande za mahindi mabichi(tamu sana hata unaweza kuvimbiwa)
Kande za siagi(za siku hizi)
Kande za msibani(mahindi na harage makavu)
n.k. n.k.

Kande ni chakula all round,

Hata misibani hawali kande siku hizi, hata uzipambe vipi kande ni chakula duni!
 
Mkuu wewe pengine umesoma boarding za St Mzungu!

Siye boarding za Kayumba hicho chakula kawaida sana na kitamu tu.

Hata kule Kenya kinaliwa sana boarding, kinaitwa mudhokoi.
Hivi Mudhokoi na Githeri ni vitu viwili tofauti?
 
Hiyo kawaida ,hata Mimi makande siyapendi kabisa yani yamenipitia kushoto,wali wenyewe nakulaga tu nikienda mgahawani ,hapa kwangu nikipika wali naishia kuumwaga tu.
 
Hivi Mudhokoi na Githeri ni vitu viwili tofauti?

Mudhokoi-kande kwa kabila la kikamba, Kenya
Githeri-kande kwa kabila la Kikuyu, Kenya


Muthokoi recipe main photo

Muthokoi​

Cecilia MuasaCecilia Muasa
Muthokoi is a very popular among the Kamba tribe in Kenya.Made for 4 people

Ingredients​


  1. 1 cup Muthokoi (dry maize with husks removed
  2. 1 1/2 cup dry pigeon peas
  3. 1 large onion
  4. 2 chopped tomatoes
  5. Cooking oil
  6. Salt
 
Cha ajabu nini hapo?
Wazazi wamezaliwa DSM, watoto kazaliwa DSM, kakulia DSM, anasoma DSM hata boarding hajui.
Sasa makande atapishana nayo barabara gani?
Hapa inshu si kuzaliwa Dar... ni malezi na background ya wazazi maana kuna familia nyingi tu watoto wamezaliwa na kukulia Dar na ni zenye uwezo kifedha ila kande, dagaa ni kawaida..
 
Makande tunakula nyumbani sio boarding, la sivyo Wapare wote wako boarding!
Ni malezi ya hovyo, kuna ambaye amezaliwa na kujua kila aina ya chakula? Si unaonja kidogo. Hata wazungu wanaofikiri ndio wanawaiga hawako hivyo.
kwani lazima mtu kula unachokiona wewe ni bora.
 
ni mfumo tu wa kimaisha, wengine hawali samaki na wengine hawali nyama, me nilikuwa sijui kama kiboko na kenge wanaliwa. hahahaha
 
Msio wakulima makande kwenu ni tabu kbisa kuna aina na aina za makande
Kande za maziwa
Kande za mahindi mabichi(tamu sana hata unaweza kuvimbiwa)
Kande za siagi(za siku hizi)
Kande za msibani(mahindi na harage makavu)
n.k. n.k.

Kande ni chakula all round,
Kabisa mkuu, zinapikwa na nakshi kibao! Binafsi kande sili lkn nazipika vizuri walaji wale kwa raha zao, huwa naweka na nazi na vitu vya kuleta amsha amsha kama nyama pembeni mboga za majani watu wanaridhiiika...!
 
Ukiwapa yale mahindi yasiyokobolewa (ngararimo) sijui watasema nini.

Kesho unaoa na kusema ni mke wa shida na raha, sawa.
 
Yani makande ni gharama.. unaweza nunua maindi ya buku na maharage ya buku... Ila mkaa ukatumia wa buku tatu ili yaive...
 
Wadau nimeona hili niwape huku na ninyi mpate kushangaa kama Mimi.

Leo tulipata ugeni nyumbani kuna rafiki yangu jirani yangu anakaa Masaki alinipigia simu nimtafutie kiwanja huku Kigamboni nikapambana nikapata.

Leo amekuja kukagua sasa kaja na wanae wawili mmoja miaka 16 mwingine kama 9 hivi, baada kukagua wamekipenda kesho ataenda benki kulipia sasa muda ukawa umefika wa chakula cha mchana.

Tumepita home apajue tukakuta Dada ameandaa lunch nikawaribisha ndani basi tukaanza kupakua chakula, wale watoto wanaongea kizungu mie sikujua lakini baba yao ndio akaniambia aisee hawa madogo awali ngoja nipige Mimi hizi kande chap chap (ni chakula mahindi wanachanganya na maharage).

Basi ikabidi tuwatafutie soda jamaa akasema hicho chakula hawakijui na wala hawajawahi kukiona aiseee nikasema kuna watu wanaishi aisee kumbe kuna nyumba hazijui kande.
Ndio zipo mfano famikia za kihindi hawajui makande kabisaaa

Yaan ww una amini ukabwela wako ndio sawa na wenzako Eboo !
 
Binafsi sili makande na kama na mimi ningekuwepo siku hiyo ningekuwa upande wa hao watoto. Siku naoa mke wangu aliniuliza chakula gani haupendi nikamwambia makande. Nadhani uwa anapika nikiwa sipo maana kuna siku nilisikia watoto wanayaongelea
 
Back
Top Bottom