Kuna familia kweli hapa mjini DSM hawajui makande?

Kande tamu sana asikwambie mtu, Ila tusilaumu sana coz kila watu na background yao.
 
Nitashangaa mtu asipokula ugali.

Hao madogo hawali kande au hawajawahi kula kande.
Kutokuwahi kula kitu haimaanishi huwezi kula. Maana yake hapo ndio wangeanza kujifunza na huenda wangezipenda.
Napenda sana haya madude tena niyatie sukari, nipate na chai.
 
Makande ovyo ovyo sana sanà yalikuwa yakipikwa shule mimi naenda kununua wali basi
 
Mimi sitaki yawekwe sukari, yakitiwa nazi tu inatosha.
 
Kande za shule za hovyo sana,maharage yanaogelea kwenye mahindi na maji
 
Mie mwanangu hadi kafikisha miaka 6ndo kaja kuyaona makande na ni watu wwnye maisha ya kawaida kabisa ya mtanzania ila tu siku zote hakuna mtu anawazaga makande..tunawaza ugal ndizi lakn siyo makande kwasabu siyo utamaduni wetu..sishangai
 
Makande tunakula nyumbani sio boarding, la sivyo Wapare wote wako boarding!
Ni malezi ya hovyo, kuna ambaye amezaliwa na kujua kila aina ya chakula? Si unaonja kidogo. Hata wazungu wanaofikiri ndio wanawaiga hawako hivyo.
Mbona watu wa ajabu sana, malezi ya hovyo kivipi sasa
Yaani ni lazima umlishe mtoto kila chakula?
Mi mwenyewe tangia nimalize shule sijawahi kula makande, simaanishi ni chakula kibaya, ila upikaji wake ni mgumu na pia hakiuzwi kwenye migahawa mingi, hata mtoto wangu anaweza akawa mkubwa hajala, so ni malezi mabaya kivipi??
 
Fafanua Uzi, MAKANDE Ni. Kitu gani, Ni wapi, mtaa au nini! Panaumaarufu sana au ni pori kama MABEPANDE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…