Kuna haja gani ya kusoma elimu ya juu wakati unakuwa mzigo kwa wazazi na serikali?

Siyo VETA tu mkuu. Kuna vyuo vingi tu private vilivyosajiliwa na NACTE vinatoa short and long courses zinazokuwezesha kujiajiri. Mfano masuala ya Graphics and Web designing, CCTV etc. Sema napo kunahitajika pesa ya kusoma Mkuu. Nadhani hapo ndipo changamoto ilipo. Kumwambia mtu akajifunze hizo short courses kwa 250K - 600K huku yupo mtaani bila kazi inaweza kuwa changamoto. Ila kama mtu anaweza kulipia gharama hizo ni vizuri akajifunza. Mie napanga kujifunza hizo short courses. Maisha ni kujipanga kwa kuyakabili kwa kila namna hakuna kuacha gap kabisa.
 
Maisha hayana formula, kuna watu wametoboa kupitia elimu (kuajiriwa) na kuna watu wametoboa kupitia kujiajiri

Kuna waliosema elimu ila wanakuta na kuna wasiosoma wanakuta, bora wangesoma iliwalipwe hata 350k

Kikubwa tuliotoboa kwa kujiajiri tuwaoneshe njia waliosoma na hawana ajira, ukizingatia elimu yote ni nadharia tupu na haimuandai graduates kujiajiri

Sasa kama unaona unaweza ukawasaidia vijana waliosoma basi fanya hivyo,

Lakini shida ya wakongo,, mtu akijiajiri na kupata vihela vya kula tena wengine hela ya kula majanga, wanaanza kuwakejeli waliosoma na kuwaona wajinga

Hivi hatujengi bali tunabomoa na kuzidisha chuki juu ya waliosoma na wàsiosoma
 
kama mtu ameweza kulipiwa ada akiwa primary privat school atashindwaje kupata 250k ya kusoma coz inayomuingizia kipata kwa mda mfupi, Pia wakiwa vyuo vikuu huwa hawaangalii maisha yajayo wao wanaishi leo kwa kutafuna boom na bumaraya bwao bwa chuoni huku hakijiona wao ni wakali na maisha wameyapatua,
 
Wewe ni muha?😁😁😁
 
Wazo lako nzuri sana. Mimi napendekeza kidato cha nne wote waende kusoma na kujifunza ufundi stadi VETA. Kabla ya kuendelea na kidato cha tano au vyuo mbalimbali.
 
Civilized kivipi ? Mbona wengi wao ndio Wala rushwa wakubwa !!
 
Umeandika point
 
We ndio maana ulishindwa kufikia hiyo elimu ya juu. Uelewa wako ni mdogo km **** ya mjusi
 
Elimu ndogo ulinayo haijakusaidia kujua role of education in life
 
Ushauri mzuri sana huu
 
Serikali ibadilishe mifumo ya Elimu, ikiwezekana Vocational training (VETA) iwe ya lazima then mambo ya chuo ni ya ziada
Yeah ni bora ingebadili mfumo ukifika form 4 uchague au kuwe na ulazima wa kwenda vyuo vya ufundi na serikali iweke mkazo sana huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…