Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,667
- 21,296
Kwa miaka mitano na ushee tukiwa chini ya Rais Magufuli tumeshuhudia utamaduni mpya ukijengeka Tanzania. Nchi imepoteza utaifa na sasa kuna ukabila, ukanda na ubaguzi wa kimaeneo! Kwa miaka mitano tumeshuhudia uwekezaji katika maendeleo ukiwa zaidi kanda ya Ziwa na hasa mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu wakati mikoa ya Rukwa, Songwe, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Njombe, Manyara, Singida nk ikiambulia kiduchu!
Hali hii inatokana na Rais kuwekeza zaidi maeneo ya karibu na kwao. Hali ya kukosa uwekezaji wa maendeleo pia uliyakumba maeneo yaliyokuwa chini ya upinzani. Kwa maneno yake mwenyewe Magufuli aliwahi sema hawezi kupeleka fedha kwa watoto wa jirani wakati pia ana watoto.
Mbegu hii ya ubaguzi aliyoipanda Magufuli tayari imeota kwa baadhi ya wanasiasa wetu kuanza kutoa upendeleo wa maendeleo katika wilaya na mikoa waliyozaliwa! Hali hii ikiendelea tutaishia katika kujenga chuki zisizo na msingi na hatimaye kupelekea vita miongoni mwetu.
Hivyo ili kujiepusha na janga hili ni heri kiongozi wetu mkuu yaani Rais awe na asili ya Zanzibar kwa sababu atakuwa hana maslahi yo yote katika mkoa wo wote huku bara.