Kuna haja Marais wote wajao wa Tanzania wawe wanatoka Zanzibar

Kuna haja Marais wote wajao wa Tanzania wawe wanatoka Zanzibar

Zanzibar ina bajeti yake tofauti na bara!
Bajeti ya bara haina mpaka inavuka mpaka Zanzibar kwa kuwa nayo ni sehemu ya Tanzania na wanapotumia fedha za kujipendelea kwao wanazipitisha chocho bila kupitia bungeni.
 
Mkuu hao hata wasikusumbue kichwa. Sasa hivi watatelekeza ID waje na mpya. We subiri JK awe mwenyekiti wa ccm na Samia aanze rasmi kazi J3 utaona ID nyingi zitapotea zilizokuwa zinamuunga mkono Magufuli
Hebu nifahamishe kdg, jk ndo anakuwa m.kiti wa ccm?
 
Ukweli mtupu,Magu kafanya mtu akitokea kanda au mkoa fulani eti anaanza kujipendelea

Ni wazo zuri maana wao Wana utawala wa ndani wakiongoza bara hawatakuwa na upendeleo wa maeneo yao
 
Fanya mpango mfugale, kijazi, morogoro barabara, na hospital zote mzihamishie kanda ya ziwa ili mseme vizuri. Ninyi ndiyo mnaukabila mlizoea kila kitu kwenu hivyo sasa mwaumia sana kuona na wenzenu wamekumbukwa. Shame on you.
 
Kwa miaka mitano na ushee tukiwa chini ya Rais Magufuli tumeshuhudia utamaduni mpya ukijengeka Tanzania. Nchi imepoteza utaifa na sasa kuna ukabila, ukanda na ubaguzi wa kimaeneo! Kwa miaka mitano tumeshuhudia uwekezaji katika maendeleo ukiwa zaidi kanda ya Ziwa na hasa mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu wakati mikoa ya Rukwa, Songwe, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Njombe, Manyara, Singida nk ikiambulia kiduchu!

Hali hii inatokana na Rais kuwekeza zaidi maeneo ya karibu na kwao. Hali ya kukosa uwekezaji wa maendeleo pia uliyakumba maeneo yaliyokuwa chini ya upinzani. Kwa maneno yake mwenyewe Magufuli aliwahi sema hawezi kupeleka fedha kwa watoto wa jirani wakati pia ana watoto.

Mbegu hii ya ubaguzi aliyoipanda Magufuli tayari imeota kwa baadhi ya wanasiasa wetu kuanza kutoa upendeleo wa maendeleo katika wilaya na mikoa waliyozaliwa! Hali hii ikiendelea tutaishia katika kujenga chuki zisizo na msingi na hatimaye kupelekea vita miongoni mwetu.

Hivyo ili kujiepusha na janga hili ni heri kiongozi wetu mkuu yaani Rais awe na asili ya Zanzibar kwa sababu atakuwa hana maslahi yo yote katika mkoa wo wote huku bara.
Nimekosa tusi zuri
 
Je tubadili katiba aliyopo atawale milele sababu amevaa viatu vyake?
 
Stigler's inajengwa Chato, SGR imeanzia kanda ya Ziwa, Kijazi interchange ipo Mwanza .... Highway ya Njia sita inajengwa Mara...Waziri mkuu msukuma, Makamu wa Rais alikua anatokea kanda ya Ziwa, Mawaziri wote walikua wasukuma, Diwani ni mtu wa Bukoba, CPG ni wa Shinyanga ...Mama wa Uhamiaji ni Wa Geita kweli Mwendazake alikua mkabila na mkanda bro your stupid kabisa
Safi mkuu
 
Hao watawala kwa haki thus Hadi leo Mungu kawapa uhai mrefu wanaishi.Watawala wa Kikristo wote watatu hadi sasa Mungu kawachukua.waislamu utenda haki thus wapo hai hata sasa.
Kanuni ni mbili za haki
1.Usimwage damu za watu.
2.Usimwage machozi ya watu.
Siku zake za kuishi zitakuwa nyingi
 
Tukisema watu wana Chuki binafsi mnatuona wabaya.
Hii ni chuki binafsi inakupofua mleta mada
 
Mkuu hujaona mabarabara ya mtaani yakijengwa
Hebu nenda
Dodoma mjini vibarabara vya mitaa
Dar maeneo ya mbagala na temeke
kiwalani vibarabara vya mitaani
Nenda kigoma
Katavi
Mbeya
Sikuelewi mkuu unataka kujenga hoja gani?
Maendeleo yapo kila pahala usituchonganishe wtz
Wakati huna uhakika na kesho yako utakula nini!
 
Back
Top Bottom