Kuna haja Marais wote wajao wa Tanzania wawe wanatoka Zanzibar

Kuna haja Marais wote wajao wa Tanzania wawe wanatoka Zanzibar

NendaMbeya mjini,Tukuyu hadiRwangwa zinapigwa lami,Dodoma ndo usiseme.Hata ungekuwa wewe mtoa mada ukawa kiongozi huwezi kuungwa mkono na wote!Hata Mitume tunaowasoma leo katika nyakati zao hawakuungwa mkono.Hata wangekuwepo leo bado wangepingwa.Wewe piga kazi lisha familia yako,fuata sheria,pambana kujikwamua kiuchumi,Saidia wanyonge.Bila kusahau kumuomba Mungu wako!Usiwe mtu wa kulalamika utajiongezea stress zisizo za lazima.Ova.
MATAGA kazini
 
Stigler's inajengwa Chato, SGR imeanzia kanda ya Ziwa, Kijazi interchange ipo Mwanza .... Highway ya Njia sita inajengwa Mara...Waziri mkuu msukuma, Makamu wa Rais alikua anatokea kanda ya Ziwa, Mawaziri wote walikua wasukuma, Diwani ni mtu wa Bukoba, CPG ni wa Shinyanga ...Mama wa Uhamiaji ni Wa Geita kweli Mwendazake alikua mkabila na mkanda bro your stupid kabisa
Hivi ukichangia hoja bila kutukana unaamini huwezi kueleweka?
 
Izo lami za wapi, Mbona izo rami zinaonekana Ni mpango wa mda mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaangalie Busekelo kutoka Tukuyu hadi Rwangwa kinachofanyika kwa macho yangu nimeona watubwanabomoa vibanda vya na contractor yuko site,Tukuyu kwenda Ndembela lami,nk unatakaje?!Hata Rumi haikujengwa kwa siku moja,Hata mke tunaanza na ushumba upo?
 
Kwa miaka mitano na ushee tukiwa chini ya Rais Magufuli tumeshuhudia utamaduni mpya ukijengeka Tanzania. Nchi imepoteza utaifa na sasa kuna ukabila, ukanda na ubaguzi wa kimaeneo! Kwa miaka mitano tumeshuhudia uwekezaji katika maendeleo ukiwa zaidi kanda ya Ziwa na hasa mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu wakati mikoa ya Rukwa, Songwe, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Njombe, Manyara, Singida nk ikiambulia kiduchu!

Hali hii inatokana na Rais kuwekeza zaidi maeneo ya karibu na kwao. Hali ya kukosa uwekezaji wa maendeleo pia uliyakumba maeneo yaliyokuwa chini ya upinzani. Kwa maneno yake mwenyewe Magufuli aliwahi sema hawezi kupeleka fedha kwa watoto wa jirani wakati pia ana watoto.

Mbegu hii ya ubaguzi aliyoipanda Magufuli tayari imeota kwa baadhi ya wanasiasa wetu kuanza kutoa upendeleo wa maendeleo katika wilaya na mikoa waliyozaliwa! Hali hii ikiendelea tutaishia katika kujenga chuki zisizo na msingi na hatimaye kupelekea vita miongoni mwetu.

Hivyo ili kujiepusha na janga hili ni heri kiongozi wetu mkuu yaani Rais awe na asili ya Zanzibar kwa sababu atakuwa hana maslahi yo yote katika mkoa wo wote huku bara.
Magufuli alikuwa janga la taifa!!
 
Kwamba kwa sababu bara kwetu kumejaa Manyani kama alivyosema Ndugai sio?
 
Izo lami za wapi, Mbona izo rami zinaonekana Ni mpango wa mda mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana engineer hajatembelea Mbeya muda mrefu!Nimekutajia kinachoendelea bado unahoji maswali!Soma kwa makini na ikiwezekana uende maana tafiti hupingwa kwavtafiti au akili za kuambiwa changanya na za kwako,upo!!!!😎kama nakuona ukishangaa,Tukuyu -Rwangwa.Tukuyu-Chuo cha ualimu nk.
 
Mahaba yako na watu wa Zanzibar usiwapakazie na kuwatukana wengine

Wape mji wako wakuongozee (wakuolee na watoto), si unawahusudu sana!
Yaani watanganyika hawaamini kama saiv wanaongozwa na mzanzibar,saiv amir jeshi mkuu ni mzanizibar lazima mtapike nyongo dadeki.
 
Hakuna haja ya kwenda huko mbali. Watawale wa Zanzibar tu ambao ni Watanzania wenzetu.
unaonaje tuchukue raia wa Kenya au Uganda atutawale maana hatokuwa na interest ya bara wala visiwani kabisaaa..
 
Inaonekana engineer hajatembelea Mbeya muda mrefu!Nimekutajia kinachoendelea bado unahoji maswali!Soma kwa makini na ikiwezekana uende maana tafiti hupingwa kwavtafiti au akili za kuambiwa changanya na za kwako,upo!!!!😎kama nakuona ukishangaa,Tukuyu -Rwangwa.Tukuyu-Chuo cha ualimu nk.
Wewe huna tofauti na wanaotema jojo kwa karanga mbili za kuonjeshwa!
 
Kumbe mama wa uhamiaji ni wa Geita!
Waziri wa nishati na mlipaji mkuu wa serikali ni wa Geita pia!
Stigler's inajengwa Chato, SGR imeanzia kanda ya Ziwa, Kijazi interchange ipo Mwanza .... Highway ya Njia sita inajengwa Mara...Waziri mkuu msukuma, Makamu wa Rais alikua anatokea kanda ya Ziwa, Mawaziri wote walikua wasukuma, Diwani ni mtu wa Bukoba, CPG ni wa Shinyanga ...Mama wa Uhamiaji ni Wa Geita kweli Mwendazake alikua mkabila na mkanda bro your stupid kabisa
 
Naunga mkono hoja. Hawana neno WA Zanzibari ona Mwinyi alipokuwa kijana akisema kila kitu 'ruksa' SASA kazeeka anatuchekesha. Kafanikiwa kumchekesha Hadi mjane mama Janet.
 
Zanzibar ina Rais wake na kuna mambo mengi yasiyo ya muungano ambayo hawezi kuyafanya.
CCM ni ileile ili mradi Magufuli kaonyesha njia ya upendeleo kupendelea kwao Samia naye hataacha kufuata nyayo za mtangulizi wake, yaliyofanyika Chato yatahamia Zanzibar.
 
Ndugu Ileje tumwache apumzike tu......japo nikweli kanda ya ziwa ndiyo ilikuwa inaongoza hata kwa Ziara...mikoa uliyoitaja nikweli inahali mbaya kiasi
 
Kumbe mama wa uhamiaji ni wa Geita!
Waziri wa nishati na mlipaji mkuu wa serikali ni wa Geita pia!
If you don't understand sarcasm, allegory and the term esoteric you're going to hate my replies and threads ..you may even sometimes term me as barbaric 😥
 
Back
Top Bottom