DOKEZO Kuna haja ya kufanyika uchunguzi Kuhusu Hili Soko lenye paa mbili za bati, soko la Mbuyuni (Manispaa ya Moshi) kwa thamani ya Bilioni 2!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sasa hizo lawama ni za nani; mkuu wa DED, Mkuu wilaya, DAS, Mkuu wa Mkoa, mkurugenzi TAMISEMI au waziri husika Mchengerwa.

Mpaka ujaeleweka shida ni nini; na lawama unampa nani.

Orodha ya wanaohitajika kulaumiwa:
1. Mkurugenzi Moshi Manispaa
2. Management ya Moshi Manispaa
3. Mayor na Diwani wa eneo husika
4. DC MOSHI
5. RAS MKOA WA KILIMANJARO
6. RC Kilimanjaro
7. Kamati za SIASA za CCM wilaya na mkoa( Hwakukagua huu mradi ).
8. Takukuru wilaya na mkoa
 
Wezi wamerudi kwa kasi baada ya msimamizi wa uchaguzi huo Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Moshi, kuwatangaza wadiwani wa ccm kushinda uchaguzi 2020 kinyume cha sheria.
 
Watu wanajadili ujenzi kwa kutumia picha, maajabu sana haya.
 
Je umeona Specification zake?
Je umeona mkataba wa B2 umehusisha kazi zipi?
Je una utaalam wowote wa masuala ya Ujenzi?
Kama huna majibu basi kaa kimya ujenzi hauzungumziwi kama Simba na Yanga lazima ujue details.
Huo ni wizi, hilo soko likigharimu sana ni TShs. Millioni 250 na si zaidi ya hapo. Hizo pesa zinaibwa mchana kweupe. Waafrica tuna shida na wengine mnatetea wezi. Shame on you.
 
Mwenye picha ya Soko Jipya la Mbuyuni, Moshi Manispaa aiweke hapo tafadhali
 
Miradi inayotekelezwa karibuni na uchaguzi huathiriwa na makusanyo ya pesa za kampeni!!
Mkurugenzi unapewa milioni mia unaambiwa ongeza sufuri mwisho... hizo nyingine zakumkampenia aliyekuteua ili arudi madarakani😔😔😔
 
Attachments

  • Screenshot_20250216-182754_1.jpg
    Screenshot_20250216-182754_1.jpg
    363.2 KB · Views: 26
Fedha zote hizi,huyu mama Nasonde,anazozichota Moshi,ni ili aende kugombea nazo Ubunge huko kwao.

Kitakachompata, ubunge atakosa, Ukurugenzi ataukosa,na atashitakiwa kurejesha fedha za Umma na mwisho ataishi Gerezani.

Anaye mlinda na kumwekea kifua Yuko ofisi za magogoni,kibabu Fulani,na amezaa Nako.
 
Utangulizi
Soko la Mbuyuni, lililojengwa katika Manispaa ya Moshi, limekuwa kivutio cha mjadala mzito miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa dhamani ya bilioni 2, wengi wanajiuliza ni wapi fedha hizo zimeelekezwa, hasa kwa kuzingatia hali ya soko lenyewe. Kila mmoja ana mtazamo wake, lakini kuna maswali mengi yanayohitaji majibu.

Kwanza, ni muhimu kuchunguza muundo wa soko hili. Picha ya soko inaonesha paa la chuma, mabati, na sakafu ambayo haionekani kuwa na viwango vya juu vya ubora. Hii inashangaza kwa sababu fedha nyingi zilipaswa kuleta mabadiliko chanya katika muonekano na huduma za soko.

Je, ni kiasi gani cha fedha kilitumika katika ujenzi wa miundombinu hii, na je, fedha zilizotumika zinakidhi viwango vilivyokusudiwa?

Pili, kuna haja ya kuangazia mchakato wa ujenzi wa soko hili. Ni wazi kwamba kuna watu wengi waliohusika katika hatua hizi, lakini je, kulikuwa na uwazi katika utendaji wa kazi?

Takwimu za matumizi ya fedha na taarifa za wakandarasi wanahitajika ili kubaini kama kuna upotevu wa fedha au ufisadi. Serikali inapaswa kutoa taarifa ya wazi kuhusu mchakato mzima wa ujenzi na matumizi ya fedha hizi.

Pia, kuna wasiwasi kuhusu usimamizi wa soko hili. Je, kuna mfumo mzuri wa kusimamia shughuli za soko ili kuhakikisha kuwa wanunuzi na wauzaji wanapata huduma bora? Watu wanahitaji kujua ni vipi soko hili litakavyowafaidi kiuchumi. Mambo kama usalama, usafi, na huduma za msingi zinapaswa kuwa kipaumbele.

Wakati huu, ni muhimu pia kuangalia jukumu la taasisi za serikali kama Takukuru. Kila mmoja anatarajia kuwa watachukua hatua za haraka katika kutafuta ukweli kuhusu matumizi ya fedha hizi.

Hali hii inahitaji uchunguzi wa kina ili kubaini kama kuna wizi au ufisadi uliofanyika. Kutokuwepo kwa hatua zozote hadi sasa kunaweza kuashiria kuwa kuna matatizo makubwa katika usimamizi wa fedha za umma.

Kwa upande mwingine, ni muhimu kwa jamii kujihusisha na masuala haya. Wananchi wanapaswa kutoa maoni yao na kushiriki katika mijadala kama hii ili kuweza kushawishi mabadiliko.

Ni lazima wawe na sauti katika masuala yanayohusiana na maendeleo yao na matumizi ya rasilimali za umma.

Katika hitimisho, soko la Mbuyuni linaweza kuwa fursa kubwa kwa jamii ya Moshi, lakini lazima kuwe na uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha. Ni jukumu letu sote, wananchi na viongozi, kuhakikisha kuwa soko hili linakuwa kielelezo cha maendeleo na si kashfa ya ufisadi. Wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua na kutaka majibu.View attachment 3267964
Awamu ya mama ni wizi na ufisadi kwenda MBELE!
 
Tusipokuwa na Katiba inayoruhusu watu kunyongwa hadharani wanapo chezea mali ya uma kwa maslai yao binafsi bado vituko vitaendelea kuwepo tu. Kama hapo waliohusika na hilo soko lenye MASHAKA sahizi walitakiwa wasiwe uraiani.
 
Utangulizi
Soko la Mbuyuni, lililojengwa katika Manispaa ya Moshi, limekuwa kivutio cha mjadala mzito miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa dhamani ya bilioni 2, wengi wanajiuliza ni wapi fedha hizo zimeelekezwa, hasa kwa kuzingatia hali ya soko lenyewe. Kila mmoja ana mtazamo wake, lakini kuna maswali mengi yanayohitaji majibu.

Kwanza, ni muhimu kuchunguza muundo wa soko hili. Picha ya soko inaonesha paa la chuma, mabati, na sakafu ambayo haionekani kuwa na viwango vya juu vya ubora. Hii inashangaza kwa sababu fedha nyingi zilipaswa kuleta mabadiliko chanya katika muonekano na huduma za soko.

Je, ni kiasi gani cha fedha kilitumika katika ujenzi wa miundombinu hii, na je, fedha zilizotumika zinakidhi viwango vilivyokusudiwa?

Pili, kuna haja ya kuangazia mchakato wa ujenzi wa soko hili. Ni wazi kwamba kuna watu wengi waliohusika katika hatua hizi, lakini je, kulikuwa na uwazi katika utendaji wa kazi?

Takwimu za matumizi ya fedha na taarifa za wakandarasi wanahitajika ili kubaini kama kuna upotevu wa fedha au ufisadi. Serikali inapaswa kutoa taarifa ya wazi kuhusu mchakato mzima wa ujenzi na matumizi ya fedha hizi.

Pia, kuna wasiwasi kuhusu usimamizi wa soko hili. Je, kuna mfumo mzuri wa kusimamia shughuli za soko ili kuhakikisha kuwa wanunuzi na wauzaji wanapata huduma bora? Watu wanahitaji kujua ni vipi soko hili litakavyowafaidi kiuchumi. Mambo kama usalama, usafi, na huduma za msingi zinapaswa kuwa kipaumbele.

Wakati huu, ni muhimu pia kuangalia jukumu la taasisi za serikali kama Takukuru. Kila mmoja anatarajia kuwa watachukua hatua za haraka katika kutafuta ukweli kuhusu matumizi ya fedha hizi.

Hali hii inahitaji uchunguzi wa kina ili kubaini kama kuna wizi au ufisadi uliofanyika. Kutokuwepo kwa hatua zozote hadi sasa kunaweza kuashiria kuwa kuna matatizo makubwa katika usimamizi wa fedha za umma.

Kwa upande mwingine, ni muhimu kwa jamii kujihusisha na masuala haya. Wananchi wanapaswa kutoa maoni yao na kushiriki katika mijadala kama hii ili kuweza kushawishi mabadiliko.

Ni lazima wawe na sauti katika masuala yanayohusiana na maendeleo yao na matumizi ya rasilimali za umma.

Katika hitimisho, soko la Mbuyuni linaweza kuwa fursa kubwa kwa jamii ya Moshi, lakini lazima kuwe na uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha. Ni jukumu letu sote, wananchi na viongozi, kuhakikisha kuwa soko hili linakuwa kielelezo cha maendeleo na si kashfa ya ufisadi. Wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua na kutaka majibu.View attachment 3267964
 
Attachments

  • 5999764-8960f3660d2a19b8257f048d9af870e4.mp4
    8.7 MB
Hata ungeniambia Million 300, bado ningekataa. Labda 1 B imeliwa kwenye vikao vya utangulizi.
kma ni uzarendo haswa hata milioni 50 haifiki kama hizo paa mbili pichani na vipande vya frame hvyo
 
Back
Top Bottom