Kuna haja ya Tundu Lissu kuandaliwa kuiondoa CCM 2025 madarakani?

Kuna haja ya Tundu Lissu kuandaliwa kuiondoa CCM 2025 madarakani?

Habari wana Jf, kwa mara ya kwanza nimejikuta nasikitishwa sana na umasikini na ugumu wa maisha unaoendelea kuongezeka huku kukiwa hakuna suluhisho la kueleweka Kutoka CCM.

Nimewaza sana na kujikuta naona Tundu Lissu ndiye anaonekana mtu pekee kwa sasa mwenye ushawishi na uwezo wa kuongoza nchi, hasa kuiondoa CCM madarakani kupitia chama chochote hata kipya, aandaliwe na kuweza kuja kuiondoa CCM.

CCM imeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 40 lakini imeshindwa hata kuwatua kina mama ndoo za maji mijini kote. Pia imeshindwa kwa kiwango kikubwa katika kupiga vita ufisadi, kuendeleza na kujenga viwanda, kuondoa shida ya ajira, kuboresha huduma za afya na nk.

2025 CCM inaweza ondoka, aandaliwe vizuri tu.
Wewe ndio mwana ccm mwenye akili
 
Mkimweka Lissu basi Mama Samia atashinda kwa 100% tofauti na hii 90% inayotarajiwa. Nashauri muazime mgombea kutoka CCM ili angalau awavushe kwenye uchaguzi. Ongeeni na Ndugai au Mnyeti.
Acha uongo kamuulize Mwenyekiti wa Tume Ya Uchaguzi Wilson Mahera na IGP wa 2020 wakwambie ukweli moto wa Lissu.
 
Back
Top Bottom