Kuna hekima kubwa yenye mantiki juu ya asilimia kubwa ya vijana kukosa pesa za ziada

Kuna hekima kubwa yenye mantiki juu ya asilimia kubwa ya vijana kukosa pesa za ziada

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Ni vyema vijana tukashukuru mfumo wa maisha uliopo ambao sio rafiki kwa sisi vijana kumiliki pesa nyingi katika umri mdogo. Kama tunavyojua ujana una mambo mengi na pesa ni lugha ya dunia combination ya vitu hivi viwili yaani pesa na ujana matokeo yake kwa vijana wachache yaweza kuwa mazuri ila kwa vijana wengi ni majuto.

Kwenye series ya Breaking Bad kuna episode ambayo Jesse Pinkman ana dai mgao wake toka kwa partner wake Walter White kutokana na ujana pamoja na lifestyle ya Pinkman Mr White anaamua kumtunzia mgao wake na kumwambia endapo atampa mgao wake atakufa ndani ya wiki ila kupitia ushawishi wa girlfriend wake Pinkman anapewa mgao wake ila kinachotokea ni girlfriend wake anafariki kwa sababu ya matumizi yaliyozidi ya madawa ya kulevya na Jesse Pinkman anaishia kwenda rehab.

Kama Mr White alivyomwambia partner wake Pinkman na mimi BabaMorgan nawaambia vijana wenzangu haswa wale wanaopenda starehe mkipata pesa za ziada mtakufa chini ya kipindi cha mwezi mmoja tu.

Vijana tukiwa na pesa akili na miili vinaenda kasi na uwezo wa kuamua maamuzi yaliyo sahihi unapungua akili zetu zinakuwa zimebase kwenye anasa na vitu vyenye manufaa kwa muda mfupi tukishafika wakati ambao majukumu yanatukabili tunabaki na majuto pamoja na kumbukumbu mbaya ya ufujaji wa pesa enzi za ujana.

Too live long it's necessary to live slow. Pesa zinatupeleka kasi zinabadili watu na mifumo yao ya maisha zinawafanya vijana kuwa na dharau mbele ya watu wazima kuanza kutumia ushawishi wa pesa kushiriki ngono ambazo si salama na wanawake wengi ikiwemo wake za watu na matokeo yake ni magonjwa ya zinaa na visasi kutoka kwa wenye wake zao vinavyopelekea ulemavu na hata kupoteza uhai.

Haina maana vijana tukose pesa kabisa tuwe na pesa za kukidhi mahitaji muhimu ya maisha zinazoweza kutusaidia katika maisha na sio kututesa na kupoteza dira kwenye maisha yetu.

Tulio vijana sasa tusidhani kuwa uzee upo mbali na kuona huu ndio wakati sahihi wa kujilipua huku tukisahau kutengeneza future nzuri kwa kigezo kuwa muda wa kujipanga bado upo kujilipua siku moja moja sio mbaya ila ni vyema kubalance ili mambo yaende pamoja.

From northern part of Tanzania.
 
Back
Top Bottom