Hili linadhihirisha kwamba viongozi wa CCM hawako kwA ajili ya kutatua matatizo ya wananchi bali akili na mawazo yao yote ni katika kubaki madarakani ili kuendeleza na kuulinda ufisadi wao.Habari za muda huu ndugu yangu
Huwa sina mtiririko mzuri wa kiuandishi, lakini napenda kujenga hoja kwa ufupi huku ikifuatiwa na maelezo mareeefu.
Kauli ya Katibu Mkuu mpya wa Chama Dkt. Emmanuel Nchimbi kwamba "Utamaduni wa CCM ni Rais wa JMT kuhudumu kwa Mihula miwili hivyo nawaambieni Mapema kabisa tusije kuzinguana huko mbele ya safari, amesisitiza Dr Nchimbi' ni mwendelezo wa kauli za viongozi wa juu wa chama ambao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Bara kuwa fomu ya mgombea urais itatoka moja tu.... na viongozi wengine wamefuata mkumbu huo huo wa kauli zinazofanana kuelekea mchakato wa kupata mgombea wa urais ndani ya CCM
Mwaka jana niliweka bandiko nikielezea namna ambavyo Muumba ameikataa CCM na sasa ameondoa kauli kwenye ndimi zao, hivyo kila wanachokiongea ni kama wanajidhalilisha. Sote tunafahamu kuwa chama kikichukua madaraka kwa njia halali au haramu kama inavyofanya CCM siku zote, basi wanapaswa kusimamia muktadha mzima wa maendeleo mtambuka ya nchi. Ulinzi, Usalama na Ukuaji Uchumi ni jambo ambalo linapambaniwa kupitia sera mbalimbali za vyama shindani.
Nchimbi amekuja na kauli hiyo ambapo kwa sisi wafia chama tulitarajia kupata kauli inayoponya majeraha yaliyosababishwa na michakato ya chaguzi ndani ya vyama. Lakini bila aibu Katibu Mkuu mpya anatoa kauli ya kwanza nzito kuelekea uchaguzi huku akianza kampeni hata kabla Tume ya Uchaguzi haijatangaza kuanza kwa mchakato.
Kuna maswali yanaibuka hapa
Mpasuko wowote ndani ya CCM ni dalili njema kwa nchi
- Je, sasa ni rasmi kwamba CCM imeshaanza kumeguka?
- Je mpasuko wa ndani ya chama umekuwa dhahiri?
- Je siasa za makundi na kambi ndani ya CCM zimeanza kuleta athari chanya kwa ukombozi wa nchi?
- Je, Katibu Mkuu mpya anajikomba au kudivert mada ionekanike yupo makini ilihali anajua kabisa kuwa mgombea wao ambaye ni incumbert hakubaliki kwa wapigakura?
Kuna tuhuma nyingi za ufisadi wa kutisha, mawaziri na viongozi wanamiliki mali za mabilioni bila maelezo ya jinsi walivyozipata. Wanafanya manunuzi na Matanuzi ya kutisha nk. Tunahitaji Nyerere mpya wa kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa majambazi yanayojiita wazalendo wa ccm