Pre GE2025 Kuna hofu gani ndani ya CCM? Hizi kauli zinaashiria mpasuko au mmeguko?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nani mmiliki wa ngurdoto hivi sasa. Iliwahi elezwa humu jukwaani kwamba wanafamilia walikuwa wameshikana mashati nani asimamie hoteli hizo. Je, walisuluhishwa. Sijasoma mrejesho kuhusu mvutano wao humu jamvini
 
Mkuu P

Huu uchama dola ndio hatuutaki tena
 
Adui muombee njaa kabisa maana ccm ni adui wa maendeleo ya wananchi.

Miaka 60 madarakani lkn wananchi ndiyo wanazidi kudhoofika kwa umasikini wakati huo viongozi wa ccm wanazidi kuneemeka.
 
Wewe una nafsi gani ndani ya ccm hadi ujifanye kujua hali yao?

Kama ulishindwa kupata nafasi ndani ya ccm kiuongozi wakati mjomba wako Jiwe yupo madarani basi nawa mikono.
 
Mbona kama unaweweseka. Kusema kuwa utamaduni ndani ya CCM ni kiongozi kuhudumu vipindi viwili nani anaupinga?
Tutajie ili tumjue.
Mpasuko uko kichwani mwako.
 
Pascal, kwanini unapenda sana generalization? Samia kaingia marakani kwa utaratibu ambao ulikuwa haujazoeleka tangu CCM iwepo madarakani, hivyo hana baraka za chama wala wananchi. Kwa hiyo ni kweli kwa maneno hayo ya Nchimbi inaonyesha kuna fukuto la chini kwa chini kuhusu mgombea wa Urais ajae ndani ya chama.

Tukiondoa unafiki, Samia hakubaliki ndani na nje ya chama. Na kama ni uchaguzi huru na haki, kwa joto la siasa lilivyo, CCM itapoteza asubuhi na mapema endapo Samia atasimama kama mgombea. Advantage aliyonayo ni tume ya uchaguzi, vyombo vya dola, rushwa na wizi wa kura.
 
Pascal, kwanini unapenda sana generalization?
Mkuu mbussi , generalisation is for the general issues, and specific issues ndio ninakuwa specific, mtoa mada ametoa general issue ya CCM ina mpasuko, jibu ni general CCM hakuna mpasuko wowote!. Akaja kwenye specific issue ya Samia hakubaliki, nikamjibu anakubalika!.
Samia kaingia marakani kwa utaratibu ambao ulikuwa haujazoeleka tangu CCM iwepo madarakani,
This is true Tanzania haijawahi kutokea tangu tunapata uhuru, siku zote VP ni standby president in case of anything happens to the president, sasa kwa vile nothing happened to all past presidents, watu tukazoea president is president na VP is VP, we no one expected this would happen!.
hivyo hana baraka za chama wala wananchi.
Sii kweli kwasababu alichakuliwa kuwa running mate wa JPM, hizo ni baraka za chama, na kila kura kura iliyomchagua JPM, pia ilimchagua Samia!.
Kwa hiyo ni kweli kwa maneno hayo ya Nchimbi inaonyesha kuna fukuto la chini kwa chini kuhusu mgombea wa Urais ajae ndani ya chama.
Hakuna fukuoka lolote kwasababu utaratibu wa CCM unafahamika.
Tukiondoa unafiki, Samia hakubaliki ndani na nje ya chama. Na kama ni uchaguzi huru na haki, kwa joto la siasa lilivyo, CCM itapoteza asubuhi na mapema endapo Samia atasimama kama mgombea.
Sii kweli
Advantage aliyonayo ni tume ya uchaguzi, vyombo vya dola, rushwa na wizi wa kura.
Japo sikubaliani na wewe, lakini naheshimu mawazo yako.
P
 
Si korosho na mbaazi mnauza Kwa mfumo Bora wa stakabadhi MAZAO ghalani!!? Na bei mnaipata nzuri ya MAZAO yenu....
 
Pascal, nikiendelea kucomment sana kwenye maelezo yako itakuwa kama tunabishana wakati kila mtu yuko huru kwa maoni yake na kwa jinsi anavyofanya analysis kwa siasa za hapa kwetu.

Tatizo ni moja, ukufanya analysis ukiwa tayari na upande au mapenzi kwa chama au kiongozi fulani, ni lazima utakuwa bias.

Kuna mtu nilimjibu humu jf, kwamba kuna mitizamo tofauti inayoitafuna CCM kuelekea uchaguzi 2025. Kuna kundi linaloamini kama nilivyosema Samia anapaswa kupitia mchakato wa kawaida wa ushindani ndani ya chama kama wanavyofanya wakombea wengine wanaoomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama kwa mara ya kwanza. Kipindi hichi anachokimalizia ilikuwa ni hawamu ya mwisho ya JPM (chawa na wanufaika wa utawala wake wengine hawataki kusikia hicho kitu).

Kundi jingine linaona kama mama nchi imemushinda na uchumi unaendelea kudolora. Huduma duni za jamii, kasi ya kutekeleza miradi ya kimkakati imepungua nk. Bado kuna wahafidhina wa Ubara na Uzanzibar, jinsia nk. Ni swala la muda tu hivi vitu vitakuwa wazi kadri siku zinavyosogea.
 
KKak
Hivi wewe ni kaka yangu Paschal au? Ukiondoa machawa Samia hakubaliki ccm wakimweka huyo kama mgombea utaona maajabu.
 
Uchaguzi wa 2025 ccm ikichimama nchale ikichuchumaa nchale ikikimbia nchale hasa endapo watamsimamisha mama Kizimkazi inaamisha Wana ccm watakuwa wamelazimishwa, kwakuwa;

1. Wanajua mama anaitumia bara kuinenepesha Zanzibar.
2. Ameonesha wazi kuwa ni mdini.
3. Ameonekana kuwakabidhi waarabuli rasilimali za bara na si visiwani.
4. Amewaachia matajir kujiamria watakavyo. eg kupanda bei ya nishati hatimae bidhaa zote kupanda.
5. Vijikodi na tozo za ajabu ajabu hence bibi tozo

Kwa hayo machache siyo kweli kwamba ccm wanakubaliana nayo ukiondoa machawa na familia zao.
Mambo mengine ni kwamba mwanamke kugombea hiyo nafasi ya juu ya nchi Kwa jamii yetu inayoongozwa na mfumo dume siyo kitu chenye afya atapata taabu sana hata atakavyokutana na vitasa kutoka Kwa TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU aliyemutwanga vitasa aliyekuwa akijiita jiwe Hadi kuugua sasa Wala urojo wataweza kweli?

Kwa hiyo ccm Wana wakati mgumu sana kwenye uchaguzi ujao Kwan mpasuko ni mkubwa sana fikiria mwenda zake pamoja na ubabe wake lakini fomu ya ugombea kupitia ccm ilichapishwa Moja kama sapraiz Kwa wapinzani wake ndani ya chama sasa bi Kizimkazi ametangaza miaka zaidi ya miwili kabla anaogopa Nini?
 
Uchambuzi wako umetulia, umeongea vitu vinavyoonekana wazi.
 
It courd be hard time😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…