Kuna jamaa yangu ameenda kwa mganga ili kuwekwa sawa kwa ajili ya kupata hizi kazi za TRA.

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,275
Reaction score
3,316
Wakuu heri ya jumapili.
Sijajua ni kuchanganyikiwa au vipi,kuna jamaa yangu kafunga safari kaenda huko kwao Magu kwa mganga ili tu awekwe sawa kwa ajili ya hizi kazi za tra zilizotangazwa majuzi.
Jamaa mwanzo alinidokeza hilo jambo na akawa ananishawishi na mimi niunge tera but mimi sio muumini wa imani hizo,jamaa karejea juzi naona mikononi kajaa Chale ananiambia keshapikwa akapikika, hapa kwa sasa anasubiri awe shortlisted ili mtanange uanze.

Hakika dunia ina maajabu sana.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Yani wenzie wanaumiza vichwa kufanya maandalizi ya kujisomea,hilo boga lenyewe linawaza waganga?
Jitu kana hilo hata likipata hiyo ajira unategemea litakua na ubunifu wowote?
 
Unaweza kuliona jambo hili kama utani! Ila ukweli ni kuwa;

Mwanadamu ni imara au dhaifu rohoni si mwilini.

Inapofika swala kuchaguliwa katika wengi, na kama wenye kuwachagua ni wanadamu wenye roho na nafsi

Hao wenye kuchagua wanaweza kuchezewa akili (nafsi zao) ili kufanya maamuzi ambayo wao wenyewe hawajui kwanini wameyafanya!

Mwaka Jana Kuna Kitabu nilikiandika ... Katika hicho Kitabu

Nilielezea kwa namna Gani miungu (Mungu na shetani) wanavyopambana kumiliki nafasi katika kifumo ya nchi ili kuitawala kupitia binadamu.

Mungu na shetani ... Wote ni Roho ... Kwa Sheria ya ulimwengu wa mwili hawawezi kumiliki na kutawala eneo, ofisi au nafasi ya kicheo pasipo mtu!

Mfano; Mungu au shetani akitaka kuwa mamlaka ya kiutawala katika nafasi ya uwongozi katika ofisi ya TRA

Atahitaji mtu ... Akipata mtu anamvika na kumpa nguvu (Ndo unasikia kuhusu nguvu za Giza) au (Nguvu za Roho Mtakatifu)

Mtu akivikwa hizo nguvu alienda kwenye usaili, si yeye anayepambana na watafuta kazi wengine, Bali Ile roho au Nguvu iliyopo ndani yake ndivyo yenye kupambana!

Na katika maisha Iko hivi; Mwenye nguvu ndiye anayetawala!

Yesu mwenyewe hakuanza kazi pasipo kuvikwa nguvu!

Wanafunzi wake, baada ya yeye kupaa aliwaeleza kuwa ... Msianze kazi mpaka Roho Mtakatifu akapowajilia juu yenu Kisha mtapokea Nguvu ndipo Sasa mnaweza kufanyika kuwa mashahidi zangu yaani kufanya kazi!

Kwa hiyo, mtu huyo akipata nafasi ya kazi Ile roho iliyo ndani yake, ndivyo inatawala hiyo nafasi ya kazi kimaamuzi

Ndo unakuta Kuna mtu ana nafasi ofisini ila maamuzi na utendaji kazi wake ni kuumiza tu watu, si yeye ni Roho iliyo ndani yake!

Ko jamaa yupo sawa kulingana na Muktadha wa Kiroho!
 
Kinapatikana wapi mkuu?
 
Back
Top Bottom