Duh! Mbona hii hatari sasa, tatizo la Watanzania, huwa hawataki kuungana na majirani kwenye kupambana na haya magaidi, tuliwaambia uhusika wetu Somalia huwa tunapambana kuhakikisha mashababi hayaoti mapembe na kuvuruga ukanda wote wa Afrika Mashariki, tunawafuata hadi kwenye shina.
Watanzania wamekua wakichekelea na kukunja mikia kwa uwoga huku majirani wote wakiwemo Uganda, Rwanda n.k. wakipeleka majeshi yao Somalia wamesahau kuna vijana wa Kitanzania wengi tu wameenda kupata mafunzo ya ugaidi Somalia, na tunao ambao wamekamatwa Kenya wakifanya ugaidi.
Vivyo hivyo Tanzania imekua ikionyesha udhaifu na uzembe kwenye vurugu za Msumbiji, wanaambiwa kwamba raia wao Watanzania haswa ndio magaidi kule, wanachekelea na kunyamaza, sasa hayo magaidi yameanza kugeuza na kurudi nyumbani. Yanachoma vijiji na kukata watu vichwa, halafu huwa siyaelewi haya magaidi, unaua wanavijiji ili iweje, hovyo sana bladi mani na zao.
Magaidi wanapaswa kuuawa bila huruma, Watanzania acheni uwoga, uzembe na udhaifu, unganeni na wenzenu kwenye hili pambano, hawa vijana hawapaswi kuogopwa, wapewe moto kama dawa.