Kuna kila dalili CHADEMA na Sukuma Gang wameunda umoja wa siri dhidi ya Serikali. Umoja wenu uwe na hoja za msingi zenye mashiko

Kuna kila dalili CHADEMA na Sukuma Gang wameunda umoja wa siri dhidi ya Serikali. Umoja wenu uwe na hoja za msingi zenye mashiko

Chadema siku zote wanatumika na Pengo.... Pengo akisema Dr Slaa muunge mkono Magufuli....anafanya hivyo mara moja...na sasa Pengo kasema "zuia Samia 2025"...
Chadema nao hasa Dr Slaa ambae bado ana influence...wameingia kazini
Umeamini HATOGOMBEA?
 
Scandal ya Bandari na KARIAKOO, Kwa maoni yangu imeunganisha makundi yote hasimu.

Hivi sasa Kuna makundi makuu mawili.

1. Mafisadi na wasaliti ambao hawafiki 100,000!!!!

2. Wazalendo wenye kuitetea kesho ya vizazi vijavyo na Ajira ya Watanzania ambao ni zaidi ya 59 milioni.
 
Acha kushikiwa akili na wanasiasa uchwara wewe. Ni aibu kuona kijana kama wewe umezaliwa ili utumiwe na wanasiasa uchwara ambao wao watoto wao wako ulaya na marekani wakitengeneza maisha yao na ya wazazi wao ( hao wanaokutumia)

Nchi moja kuingia mkataba na nchi nyingine haimaanishi kwamba serikali imeshindwa, bali ni katika uboreshaji wa mbinu za kiuchumi.

Hii dp world ndio inayoendesha bandari za Marekani, Uingereza na nchi nyingine kubwa ambazo wenye akili na wafuatiliaji wa mambo ya dunia wanazifahamu.

So wewe unafikiri raisi wa Marekani au Queen Elizabeth wa Uingereza hawakuwa na uwezo wa kuendeleza bandari zao hadi kuwakabidhi hao jamaa?
Je wao hawana jeshi, fbi, cia nk?

Hawana matajiri wa kuziendesha bandari zao?

Akili za kuambiwa changanya na zako, usiwe kama bata anaerushiwa tunge la ugali na kukimbilia kulimeza bila kufikiri labda sometimes anaweza kuwekewa jiwe katikati ya tonge ili baadae lije kumdhuru.

Shtuka kijana, acha kutumiwa na wapiga deal, wakwepa kodi bandarini na wapitisha madawa ya kulevya.

Wenzio wanapiga kelele ili kupambania kitumbua chao pale bandarini afu wewe unaishia kutumia bando lako, pumzi yao na nguvu zako kupigania ulaji wao.

Imekaa vizur sana
 
Hizo nchi ulizozitaja kuna ambayo wanafanya wenyewe na wanaweza wewe yakwako imeweza nini?.Wenzako wanabinafsisha kwasababu zakiuchumi wewe tatizo linaanzia kwenye usimamizi.uoni tofauti.
 
Kwanza majaliwa ametupiga kamba mara ya pili hii kutuambia eti kilichokwenda bungeni ni mkataba wa ushirikiano kati ya Tanzania na Dubei akati tulisikia bunge likijadili na kutetea maazimio ya mkataba wa uwekezaji katika bandari zote tanganyika. Huyuhuyu alitudanganya eti yupo ikulu anaendelea na shughuli zake akati kumbe mtu alishazima.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mkataba ni miaka mingapi ? Vipi terms za kuvunja ?
Hauna mwisho. Jisomee 👇🏾

5:
4. Nchi Wanachama zinakubali kwamba Miradi ya Awamu ya 1 (kama ilivyofafanuliwa katika Kiambatisho 1) itakuwa ndiyo miradi ya kipaumbele katika kuiendeleza na kuitekeleza. Serikali ya Tanzania itahakikisha kwamba TPA haitaongeza mapendekezo mengine yoyote ya Miradi yoyote ya Awamu ya 1 kuanzia Tarehe ya Kusainiwa hadi tarehe ambayo majadiliano kati ya DPW na TPA kwa Miradi ya Awamu ya 1 yamesitishwa au baada ya kumalizika muda wa miezi 12 kutoka Tarehe ya kusainiwa kwa Mkataba huu, yoyote iliyo ya mapema
 
Waziri mkuu hajajibu hata swali,hoja za serikali hazitoi majibu,badala yake ni zimejaa kubeza, nakejeli,na mashambulizi binafsi(personal attack) dhidi ya wanaohoji,hata Samia nayeye hatoi majibu badala yake Yuko took general,hayuko specific,yaani anaongelea kitu kingine halafu la bandari anachopeka kwa mbaaaaaaali!!!!!, Hana hoja juu ya Hilo,wakati ambapo yeye Kama mkuu wa nchi alitakiwa kutoa coverage hata ya dk 45 kwenye media akilifafanua, Sasa kwa hoja mchopeko hizi za kuvizia vizia hakuna kinachoeleweka,majibu ya serikali hayako specific,tunashawishika kuamini kuwa mlungula umepitishwa ,wallet za na akaunti zao za Benki zimejaa
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Chadema siku zote wanatumika na Pengo.... Pengo akisema Dr Slaa muunge mkono Magufuli....anafanya hivyo mara moja...na sasa Pengo kasema "zuia Samia 2025"...
Chadema nao hasa Dr Slaa ambae bado ana influence...wameingia kazini
Wewe jamaa kwenye hili la DPW umeonyesha rangi zako halisi,huna uwezo tu lakini unatamani hata utusilimishe Nchi nzima na kwako Mwadhama Kardinali Pengo ni kikwazo kikubwa sana kwa ajenda uliyonayo.
 
Hauna mwisho. Jisomee 👇🏾

5:
4. Nchi Wanachama zinakubali kwamba Miradi ya Awamu ya 1 (kama ilivyofafanuliwa katika Kiambatisho 1) itakuwa ndiyo miradi ya kipaumbele katika kuiendeleza na kuitekeleza. Serikali ya Tanzania itahakikisha kwamba TPA haitaongeza mapendekezo mengine yoyote ya Miradi yoyote ya Awamu ya 1 kuanzia Tarehe ya Kusainiwa hadi tarehe ambayo majadiliano kati ya DPW na TPA kwa Miradi ya Awamu ya 1 yamesitishwa au baada ya kumalizika muda wa miezi 12 kutoka Tarehe ya kusainiwa kwa Mkataba huu, yoyote iliyo ya mapema
Hahahahaha.......kwa uwekezaji huo miezi 12 hiyo sio muda as mkataba .....UK wameweka wazi sana miaka 20
 
Hahahahaha.......kwa uwekezaji huo miezi 12 hiyo sio muda as mkataba .....UK wameweka wazi sana miaka 20
Unaongelea mkataba tofauti na uliosainiwa.

Watanzania mnasikitisha sana kujifanya mnajuwa kumbe hamjuwi.

Mkataba uliojadiliwa bungeni ndiyo huo, sasa kila uwekezaji una mikataba yake ya kibiashara. Mikataba ya kuendesha bandari duniani kwa uchache ni mik 25. Fanya tafiti kidogo, hutegemea na thamani ya kilichowekezwa.

Kuna hesabu za ROI zinapigwa , ndiyo raha ya watu kusoma.
 
kama wanaungana kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi na kulinda raslimali za Taifa ni jambo la kheri na lenye kumpendeza Mola, Kuliko hili lililofanywa na ccm la kumpendeza yule mwovu!
 
Unaongelea mkataba tofauti na uliosainiwa.

Watanzania mnasikitisha sana kujifanya mnajuwa kumbe hamjuwi.

Mkataba uliojadiliwa bungeni ndiyo huo, sasa kila uwekezaji una mikataba yake ya kibiashara. Mikataba ya kuendesha bandari duniani kwa uchache ni mik 25. Fanya tafiti kidogo, hutegemea na thamani ya kilichowekezwa.

Kuna hesabu za ROI zinapigwa , ndiyo raha ya watu kusoma.

Wao chochote kile wakiongopewa na PENGO basi hawarud nyuma,

Kwanza hizo hesabu zenyewe za Return Of Investment anazijua?
 
Wewe jamaa kwenye hili la DPW umeonyesha rangi zako halisi,huna uwezo tu lakini unatamani hata utusilimishe Nchi nzima na kwako Mwadhama Kardinali Pengo ni kikwazo kikubwa sana kwa ajenda uliyonayo.

PENGO na Dr Slaa vi mandumilakuwili,wanakosa moral authority ya kuzungumza kwani siku zote huchagua Regimes zinaegemea kwenye Iman zao na kuzisifia,Kisha zilizo tofaut kuzichukia,lazima waambiwe ukweli.
 
Back
Top Bottom