Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili huenda mwiko unaenda kuvunjika

Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili huenda mwiko unaenda kuvunjika

Watakataje tamaa wakati kuna madege, mameli, mabwawa, mabarabara, madaraja, mareli na makodi mengi mengi...??
Hao wananchi hawaoni nchi ipo uchumi wa kati?

Hahaha 😂 😂 Kaka kwa maneno Haya jiandae kumtafuta mtu wa kukuwekea dhamana
 
Tunagombana bure Watanzania, kila mtu anajia kura yake ataipeleka wapi na kwasababu zipi. Kusema ukweli mimi nitaipeleka kwa Magufuli kwa sababu kama tatu kwanza umeme kufika kijijini kwetu na nyumbani ninautumia tena unit 75 nalipia 9150, pili maji salama na safi ninayatumia nyumbani na hayakatiki mwaka mzima nalipia tsh 9000 kwa mwaka na mwisho ni mawasiliano ya simu mitandao yote inapatikana mpaka uvunguni zamani tulikuwa tukitumia mitandao ya Burundi.
Ni kwa sababu hizo tu nitaipigia tena kura CCM na wagombea wake wote nilijia Philip Isdory Mpango atakuwa mbunge wangu

Miaka 50 ya uhuru unampa mtu kura kwa Sababu ya umeme duh
 
Siku nyingine huwa nawaeleza halafu hamfuati, niliwaambia mnichague mimi mkasema sawa, nikawaambia mnichagulie na mbunge wa CCM hamkunichagulia, nataka niwaeleze ukweli wala siwafichi asingekuwa Kapuya hii barabara nisingeijenga". Dkt.Magufuli
 
Jiandae kisaikolojia, Magufuli atashinda kwa kishindo kikuu hiyo Oct 28.Lissu hawezi kuwa Rais wa tanzania, ukawa walichemsha 2015, ndio basi tena.
Kuna maccm kama Polepole yana DHAMBI. Unafunga MIRIJA ya UCHUMI Nchi nzima. Wananchi wanalia NJA.

Wakisema vyuma vimekaza eti unawafunga badala kufungua mirija ya Uchumi.

Huu ujinga wote unafanywa ili uweze kuwaDHIBITI siku ya UCHAGUZI kwa kuwapa buku mbili wajaze viwanja.
 
One picture of Dr Magufuli sitting on a lonely boulder on a Ubungo Flyover Road side intently listening to barefoot Machingas went viral.

That picture symbolised deliberative government, grassroots consultation, servant leadership and humility.

In Dr Magufuli’s Tanzania, no citizen is too small. The biggest office is that of a citizen, not President What’s happening in Tanzania is revolutionary.

Presidents elsewhere should come to benchmark in Tanzania, not Belgium.
Delete ccm Oct 28
 
Wafanyabiashara hoi,wakulima masoko hamna, wafanyakazi miaka mitano(hamna nyongeza ya mishahara, kupanda madaraja kiduchu,wamezuia uhamisho toka 2018),vijana wanahitimu maelfu kwa maelfu ajira hamna, watu wameachishwa kazi kwa kisingizio cha vyeti, maisha mtaani kila mtu siri yake,ccm watachomokea wapi, labda utokee muujiza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katibu mkuu CCM anaweweseka balaa , amebakia kutoa vitisho
IMG_20200920_130350.jpg
 
Kwaviburudisho na post za comedy ingia Jamii forum fungua thread za makamanda.
Wanasubiri kuapishwa Tobo Lissu km sabato masalia walivyokuwa wanasubiri uwanja wa ndege kwenda ulaya bila passport! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ninaongea kila wiki na ndugu zangu huko kijijini; hakuna wanaojua chama cha upinzani, wanasema tangu mwaka 2010 wakati CHADEMA ilikuwa imeanza kujikita hapo kijijini, leo hii hakuna chama zaidi ya CCM. Wanashindwa kutofautisha kati ya serikali na CCM; kwao huwezi kuwaambia jambo dhidi ya CCM, ndiyo maana nina uhakika kuwa CHADEMA kinacheza kujifurahisha tu, ila siyo kutafuta ushindi. Ushindi hauji kwa mtindo huu wa CHADEMA.
Acha kujichamba na kunusa kidole mkuu!!!
Dunia inaenda kwa kasi sana.

Ushindi wa CCM unategemea dola tu kufumbia hila ya wizi wa kura utakao fanyika. Wakifeli hii njia ndo basi Tena.
 
Wasalam,

Pamoja na mazuri yote aliyofanya Mh magufuli bado wingu jeusi limetanda ndani ya ccm kutokana na uasi wa baadhi ya wanaccm.
Kuna kila dalili kwamba ccm inaenda kushindwa kwa fedhea ktk uchaguzi wa Oct 28.

Dalili moja mbaya ni kwamba wananchi ambao ni wapiga kura wamekata tamaa kutokana na ugumu wa Maisha na wengi wameapa kuikataa ccm Oct 28, huenda Tanzania ikaandika historian kwa Rais kuongoza kipindi kimoja cha miaka5.

Dalili zinaonesha Watanzania hawana imani na CCM pamoja na rais magufuli.

Maendeleo yana vyama.
JamiiForums-1625416118.jpg
 
Dalili moja mbaya ni kwamba wananchi ambao ni wapiga kura wamekata tamaa kutokana na ugumu wa Maisha
Unafuu wa maisha unaanza kwa wewe kuwa na familia ndogo unayoweza kuimudu. .. Mshahara wa laki saba, una mke na watoto watano na wazazi wanakutegemea, huo unafuu unautoa wapi?
 
Back
Top Bottom