Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Sio siri tena kwa sasa vita vya Ukraine imeshika kasi huku Russia ikipitia kipindi kigumu zaidi huenda kuliko kipindi kingine chochote tangu kuanza kwa hii vita.
Kuna dalili fulani ambazo zinazoonyesha kama vile Putin pumzi inaelekea kukata. Hizi hapa chini ni baadhi ya sababu muhimu zenye kueleza hayo;
1. Kitisho cha kutaka kutumia Nyuklia ili kumaliza vita.
Sote tunajua Russia ni taifa kubwa kijeshi likiwa na shehena za kila namna za kivita na kiteknolojia, kitendo chochote cha Russia kupiga mkwara kuwa huenda wakaanza kutumia nyuklia ili kuishinda Ukraine, hiyo ni dalili ya kukata tamaa kwa 100%. Ni sawa sawa na serikali ya Tz itangaze kutumia mizinga, makombora na vifaru ili kuwaliza panya road wa Dar!
2. Kuita wanajeshi wa akiba wasiopungua laki tatu ili kwenda vitani Ukraine.
Hawa wanaoitwa wanajeshi wa akiba kumbe ni raia wanaume wa kawaida wa Russia ama kwa hiari yao au kwa nguvu wanashurutishwa kwenda vitani sasa.
Mantiki yake ni nini na kwanini iwe sasa?
Je, wanajeshi rasmi wa Russia wamepungua sana?
Je, vita imekuwa kubwa na nzito kwa Russia kiasi cha kuokoteza vijana mtaani ili kuipigania Russia?
3. Putin kulalamika kuwa sasa amegundua NATO na USA wanaisaidia Ukraine kisiri kwa hali na mali.
Hili ndio limenishangaza zaidi. Sote tunajua (sio siri) kuwa USA na NATO wapo bega kwa bega na Ukraine tangu awali. Na tangu awali Putin alishaonya kuwa yoyote atakayeisaidia Ukraine moja kwa moja kwenye hii vita atakiona cha mtema kuni mara moja (immediately military reaction from Russia). Sisi tulitegemea Russia ateremshe kichapo cha chap chap kizito kwa USA na nchi za NATO halafu ndio aje kwa umma kusema hizo blah blah. Ama basi atangaze kuitisha special military operation against USA and NATO ili tumuelewe.
4. Russia kutangaza kuwa kwa sasa inataka zaidi mazungumzo ya kumaliza vita!
Wakati vita hii inaanza Russia ilikuwa haioni kivilee faida ya kumaliza mzozo huu kwa mazungumzo ya mezani na Ukraine, Russia ilikuwa mwendo mdundo kufurumusha mabomu katika ardhi ya Ukraine. Wakati huu ambao Russia inatamani mazungumzo zaidi ili kumaliza vita, upande wa Ukraine wao hawataki sana mazungumzo kama ilivyokuwa awali.