Pia kitendo cha Putin kuanza kuwakusanya raia kwa nguvu waende wakapigane Ukraine (sawa na leo hii itokee vita halafu Serikali iseme inawataka watu wote wenye umri kati ya miaka 18 na 60 kwenda vitani kupigana). Sasa Warusi wanahangaika kukimbia nchi yao kwa hofu ya kupelekwa mstari wa mbele nchini Ukraine kwa nguvu. Hapo katikati, Putin alianza kuwahadaa raia wakapigane kwa ahadi ya kuwalipa dola 2,700 kwa mwezi. Wajinga wakaenda, wakaishia kwenye majeneza, na hela waliyotegemea wapate, ikawa ndiyo mwisho.
Vita hii ikienda tu mpaka mwishoni mwa 2024, Russia itakumbwa na mdororo mkubwa wa uchumi. Mpaka mwishoni mwa 2024, nchi zote za Ulaya zinazotegemea mafuta na gas toka Russia zitakuwa zimepata alternative supplies, na hapo wataweza kuweka vikwazo kwa 100% dhidi ya chochote cha Russia.