Kuna kipi kinaendelea? Mbona kila kona malalamiko ni ndugu kupotelewa na jamaa zao?

Kuna kipi kinaendelea? Mbona kila kona malalamiko ni ndugu kupotelewa na jamaa zao?

Kumbe hupogo? Ulipoteaga hapa kati nikadhani na wewe umetekwa kwa kudhulumu kwenye udalali.
Dogo unanichafua, Nipo kwenye mchakato wa kupewa u moderator halafu unaniita Dalali?
 
Tatizo letu tunachukulia utani hili Jambo. Siku likishika Kasi hakuna pakujificha.
 
Umteke unaemdai umpeleke wapi...si bora unampiga cha moto tu. Hata South Africa walokubuhu kwa visasi hawatekani...kuteka ni kujiongezea kazi na hatari. Mara nyingi kibongobongo mamlaka ndio zinazoweza kukuteka
Hivi yule binti wa kiarabu aliyetekewa msasani peninsula alitekwa na mamlaka?
Kuna watu wametekwa na wao syo wanaharakati,hawajidhugulishi na siasa

Ova
 
Mfano ni mkoani Singida, familia tatu zinawalilia ndugu zao walio tekwa na watu wasiojulikana.

Familia mbili za huko Wilaya ya Iramba, zinazoishi karibu na Loya, zinalia kupotelewa na wafanyabiashara wa mazao jinsia yao ni wanaume wawili. Wawili hao inasemekana walitekwa na gari nyeupe aina ya Toyota LC. Na tukio hilo lilitukia tokea Oktoba mwaka jana.

Tukio jingine fanani na hilo limetukia ndani ya Manispaa ya Singida, likiwahusisha wafanyabiashara wa mbao nao ni wawili wa familia moja. Kama sikosei, walitekwa na gari fanani na ile iliyotajwa hapo juu na kwa ufanano uleule wa utekwaji. Nao ni wanaume.

Kipi kinaendelea kwa aina hiyo ya kutoweshwa!?
Vita ya ubunge huko Iramba! Manila kibubu hataki ushindani maana anajua atashindwa
 
Back
Top Bottom