Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Naona wengi wenu hapa mnapuyanga tu. Sisi parokiani kwetu kuna sadaka mbili tu matoleo ya kawaida na ujenzi wa kanisa ambao infacts ni kweli.

Hata hivo hakuna mchango usiokuwa na maelezo na hii inategemea eneo na eneo.

Imagine parokia kama mavurunza wanajenga kanisa la ghorofa unadhani ni michango kiasi gani inahitajika?
 
Inasikitisha Sana[emoji26]
 
Zamani makanisa yalikuwa yanapata sana misaada toka nje lakini kwa sasa nje hawatoi sana misaada (wanasema mioyo yao kuhusu dini imepoa) so inabidi makanisa yajiendeshe yenyewe. Hapo ndipo uhitaji mkubwa wa hela unapoanzia
Ha ha ha....
Hapo ndo unapata picha kuanmakanjsa makanisa yaliletwa afrika kimchongo.

Mwendo wa
Explorers[emoji117] missionaries [emoji117]Traders[emoji117]colonialist
 
Nakazia[emoji106]
 
Milele Amina !

Kuna muda tusiwe wapotoshaji, wewe kutoa/kutokutoa humpunguzi kitu mtu. Kutoa inapaswa iwe ni jambo lako na moyo wako.

Na hii ieleweke kwa dini zote, maana hulazimishwi wala hutatajwa wewe hukutoa/wala hutatukuzwa kuwa umepotea ni vema sasa ujifunze kwa kujiwekea utaratibu kutoa ni moyo anayejua ni Mungu wako.
 
Nikisema nifuate ushauri wako na kufuata kanuni za Mungu basi hata sadaka ninayotowa sasa hivi hawataipata nitapeleka direct kwa yatima na wajane na kanisani sintokanyaga tena.

Siendi kanisani kuutafuta ufalme wa mbinguni haupatikani pale, nakwenda kanisani kuwa connected na jamii yangu ambao tunaamini katika kristu.

Mimi siamini katika kuuona ufalme wa mbinguni kwa kwenda kanisani au kunipa maandiko ili kuhalalisha uharamia wenu?

Mbona maandiko mnachaguwa ya kutumia wakati Timotheo wa pili imeandikwa wazi atamaniye kazi ya uaskofu basi atamani kazi njema, basi imempasa Askofu awe mume wa mke mmoja, sasa mbona kanisa katoliki limekumbatia useja kinyume na mafundisho wa biblia?
 
Huu uzi haujaandikwa na Mkatoliki, aliyeandika hapa anatoka kundi la wale wanaosababishaga biashara ya kitimoto izorote
 
Yule moigaji TU,
Anasema Hakuna sadaka, ila Kuna michango[emoji4]

Michango haina ishu hautoi...

Sadaka za makanisani nyingine zina hadi mkataba wa mwaka, unasaini kwamba mwaka huu jengo utatoa kiasi kadhaa, ahadi kiasi kadhaa...
 

Unaotaje sadaka ya shukrani kila unapofanikiwa. Mbona wao hatoi sadaka ya shukrani wakifanikiwa kupata magari au kujenga makanisa
 
Kumbuka hizi imani tuliletewa na wageni. Kipindi chote cha nyuma walikuwa kwenye matazamio. Vitu vingi walikuwa wanagharamia kwenye makanisa mengi. Hata ujenzi wa makanisa walikuwa wanahusika kwa kiasi kikubwa. Hata mishahara ya wachungaji walikuwa wanahusika. Kufupisha kwa sasa kila kitu wameacha kutoa,hata ruzuku zote wameacha kusaidia makanisa. Walikuwa wanasubiri tuwe addicted na hiyo imani. Kwa hiyo makanisa kwa sasa yanajiendesha yenyewe. Lazima wategemee hizo sadaka kwa kiasi kikubwa.
 
Mimi nipo Tabora, mbona hakuna huu mfumo?
Kila Askofu ni mkuu katika jimbo lake, itakuwa Askofu wenu hapendi upumbavu kama yule Askofu wa KKKT Askofu Bagoza.

Hongera zenu, jimbo kuu la Dar kumeharibika Askofu mkuu mchaga.
 
Even Muslim but , waislam ni bahili sana,
Waislam sio bahili, sema waislam wanajitambua sana, na wanaitambua dini yao na mafundisho yao.
Waislam hawalazimishwi kuchangia kama mtu hana kitu. Wapo radhi kumchangia myu asiye na kitu na sio kumlazimisha achangie.
Pia waislam wapo huru kuhoji juu ya mapato na matumizi ya sadaka zao.
Na kingine wanaruhusiwa kuchangia kulingana na mradi husika mfano kwenye ujenzi sio lazima utoe pesa unaweza kutoa bati, tofali, nondo, sementi na vitu vingine kama hivyo.
 
Utazikwa na ndugu na majirani, si lazima kiongozi wa dini awepo.
...Hata ndugu yako yoyote anayeweza kusoma TU anaweza kuongoza Misa ya Wafu Kwa ajili Yako!
Hakuna, rudia, Hakuna aliyepewa Mamlaka ya kukusalia wewe ukifa ili uingie peponi!
 
Kidogo akili imeanza kutuingia. Dhehebu langu niliyaona mengi yanayokwaza kupitia michango. Ugumu ni kuwalisha somo hawa wafia dini wanaojiita wasaidizi kama wazee wa kanisa, wakuu sijui viongozi wa vigango hadi waumini wa kawaida. Wataanza kukushambulia na kukuona pepo mchafu. Nikaona isiwe taabu, nikawaachia watoto na mama yao. Kazi kubwa kwangu ni kuandaa sarafu za Sunday school kwa watoto ilihali mama ajitafutie hiyo michango kadri atakavyobarikiwa.

Ni kama viongozi wakuu hawatafakari nasi tuna mahitaji binafsi ya kuzitunza familia zetu! Wao wanatembelea magari, watoto wao wanapewa elimu za viwango vya juu, wake na waume zao wanatunzwa kupitia jasho letu lilibatizwa 'kutegemezwa' sijui na taka taka gani.

Kimsingi sadaka ililengwa itoke kwa hiari sio shuruti kama ilivyo madhehebu mengi ya kileo.

Nashukuru sana GT kwa kuliona hili na ukatupia uzi.

Wengi wako nyuma yako, tunakuunga mkono kupaza sauti hadi huu uharamia upungue au wabaki kusali viongozi wa kanisa na familia zao. [emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]
 
Nakazia[emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…