Mtimkavuorg
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 655
- 527
Unataka baba Paroko ale nini na kanisa ajenge nani nashangaa sana Rc wenzangu ila mkienda kwny makanisa ya kilokole mnatoa sana hamsemi kauli ngumuKweli mkuu hata mimi nimeacha kwenda kanisani kutokana na sadaka na michango kuwa mingi mno kiasi kwamba ukipiga hesabu ya utitiri wa michango unakata tamaa ya kwenda kanisani.mara uta sikia mchango wa kununua gari la mtumishi nk. wakati Yesu huyo wanaomuhubili hakuwahi kumiliki hata baiskeli alikuwa anatembea kwa miguu! Naunga mkono hoja kuna haja ya kuhoji.
NEEMA YA BWANA IWE NANYI!
Kwa hiyo huyu alitaka Wakatoliki wawe wanagawiwa pesa kutokana na miradi hiyo??.Mimi ni muumin wa kawaida tu, huwa siingii deep sana na sina mazoea wala ukaribu na viongozi/mapadre natimiza wajibu wangu tu. Naomba kueleweshwa na mimi.
Sasa kwenye suala miradi huwa sijui tunanufaika vp na namna gani niwe muwazi hapo sasa ndiyo unipe shule mkuu ?
Umeona eenhh??!!!.Huyu ndugu yetu hamna lolote.Unataka baba Paroko ale nini na kanisa ajenge nani nashangaa sana Rc wenzangu ila mkienda kwny makanisa ya kilokole mnatoa sana hamsemi kauli ngumu
Mungu amponye katika ubatizo wake na akili imani yake [emoji120]Kwa hiyo huyu alitaka Wakatoliki wawe wanagawiwa pesa kutokana na miradi hiyo??.
Ngoja atuelezeeKwa hiyo huyu alitaka Wakatoliki wawe wanagawiwa pesa kutokana na miradi hiyo??.
Kwani zamani hizo bill alikuwa analipa nani?inaonekana na wewe ni mnufaikaToa ndugu toa ndugu..ulichonacho..halafu unataka usitoe hilo kanisa litapelekaje injili..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje wahudumu..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje bills tofauti kama umeme na maji...unataka usitoe hilo kanisa litafanyeje logistics mbali mbali...unataka usitoe maintaince na repairs ya vifaa na miundombinu mbalimbali utatoa wewe.??
Acha kulalamika sana kama huna hela kaa kutulia
Uzuri hujalazimishwa..ila mkristo wa kweli hawezi kuona kama ni wizi mana hayo ndio mahitaji muhimu ya kuendesha taasisi.
Kingine kutoa ni upendo..kiwango itachojaliwa kutoa kinatosha sana.
Kama unaona hufiti nenda huko ambako hawatoi sadaka..hakuna aliyekushikiria unabaki kanisani.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.
#MaendeleoHayanaChama
Kuna mambo Uislamu upo vizuri aisee.Wakati unatusifia Waislamu, sisi huku wenyewe tunatamani tungekuwa na moyo wa kutoa sadaka kama wenu.
Sisi ni changamoto watu wazito kutoa sadaka, madrasa na misikiti mingi inahitaji ukarabati na shule pia. Ila watu wetu wazito mno wa kutoa sadaka. Sadaka mpaka zitokee kwa waarabu ndio madrasa zijengwe
Kwani zamani hizo bill alikuwa analipa nani?inaonekana na wewe ni mnufaikaToa ndugu toa ndugu..ulichonacho..halafu unataka usitoe hilo kanisa litapelekaje injili..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje wahudumu..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje bills tofauti kama umeme na maji...unataka usitoe hilo kanisa litafanyeje logistics mbali mbali...unataka usitoe maintaince na repairs ya vifaa na miundombinu mbalimbali utatoa wewe.??
Acha kulalamika sana kama huna hela kaa kutulia
Uzuri hujalazimishwa..ila mkristo wa kweli hawezi kuona kama ni wizi mana hayo ndio mahitaji muhimu ya kuendesha taasisi.
Kingine kutoa ni upendo..kiwango itachojaliwa kutoa kinatosha sana.
Kama unaona hufiti nenda huko ambako hawatoi sadaka..hakuna aliyekushikiria unabaki kanisani.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.
#MaendeleoHayanaChama
Wewe siyo muislimu ila umejichomekaWakati unatusifia Waislamu, sisi huku wenyewe tunatamani tungekuwa na moyo wa kutoa sadaka kama wenu.
Sisi ni changamoto watu wazito kutoa sadaka, madrasa na misikiti mingi inahitaji ukarabati na shule pia. Ila watu wetu wazito mno wa kutoa sadaka. Sadaka mpaka zitokee kwa waarabu ndio madrasa zijengwe
Aiseee ๐๐พ๐๐พ๐๐พ๐๐พUkifa hawakuziki. Hapo ndipo wametushika pabaya
Hawa watu wanatumia kifo kutisha waumini.Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!
Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.
Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!
Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??
Nini tenaaAiseee ๐๐พ๐๐พ๐๐พ๐๐พ
Mmh hii ni hatari ni too muchMkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!
Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.
Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!
Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??
BTW, Roman Catholic wana double standards sana katikaa hili.Ukifa hawakuziki. Hapo ndipo wametushika pabaya
Hela yangu huwa nawasaidia wahitaji na wagonjwa,na naamini ndo sadaka yanguMkuu unaweza nisaidia sadaka hizi tisa zilikua zipi na mlitoa kwa wakati gani?. Ili ni muhimu usiache kujibu.
Mimi kwangu ilishabaki na sali sala binafsi nyumba. Ikiwa tofauti mara moja moja naenda kanisani nasali na kuondoka. Ukweli michango imekua mingi imefika hatua hadi kanisa wanajisajili kulipa kwa mpesa au tigo pesa. Huwa siaangaiki ata na mchango mmoja. Utasikia kanisa halijaisha, shule ya chekechekea, nyumba ya sisters.
Swala la zaka sijawai toa na sitarajii kama ntakuja kutoa. Ile asilimia 10 ya kipato cha mtu inatofauti gani kodi wanayotoza TRA katika kila faida anayopata mtu. Ni onyonyaji.
Nafikiri hofu ya wengi huwa wana hofu padri hasipokuja siku ya maziko yako. Kwangu ili si hofu maana ntakua mfu sitojua walinitupa au walinivisha nguo gani. Nani alikuja msibani nani hakuja
Hapa ndio naona dini wakati mwingine ni mchongo. Haiwezekani wao wakitaka gari aua nyumba tuwachangie. Ila sisi wauumini tukitaja gari au nyumba tupige magoti tuombe sana.
AMINAMungu amponye katika ubatizo wake na akili imani yake [emoji120]