Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

KKKT wanaongoza kwa ndimi 2: walimzika Mengi kikanisa wakati alikosa vigezo.

Ila RC hawakumzika Mrema wa Arusha kwa mambo hayo.

Kiufupi, ukiwa mtoaji sana kanisani wanaweza kukufikiria na hata kukusamehe
 
Mtaka sifa haogopi hasara!
Wacha punda afe mzigo ufike!
 
Acha uongo bhana!!.Kingunge alizikwa na Katekista,wala hakukuwa na Misa napo ni kwa vile tu familia yake ilikuwa mshirika mzuri,pia dakika za mwisho alionyesha kutaka kumrudia MUNGU lkn bahati mbaya hakuwa ametubu.
 

Kwa miradi iliyopo chini ya kanisa, ambayo kimsingi ilijengwa kwa nguvu za waumini…. ingetosha sana kujiendesha na hata kujenga miradi mingine yakiwemo makanisa mapya ambayo ni uwekezaji.
 
Kwa miradi iliyopo chini ya kanisa, ambayo kimsingi ilijengwa kwa nguvu za waumini…. ingetosha sana kujiendesha na hata kujenga miradi mingine yakiwemo makanisa mapya ambayo ni uwekezaji.
Una Elimu kiasi gani kuhusu usimamizi na uendeshaji wa miradi??.
 
Leta ushahidi na source yake
Hata nikikuletea utasema ni uchochezi wa maadui wa kanisa.
Lakini ukweli lazima usemwe, Kanisa katoliki lina kashfa nyingi na za kweli sii tu kwenye ufisadi bali hadi mapadre kulawiti watoto huko ulaya, na wengine wanazaa na wake za watu hasa huku Africa.
Mimi mwenyewe ni mkatoliki lakini uchafu wa hili kanisa letu unatisha.
 
Mwenyezi Mungu anasema hakuwaumba majini na watu ila wapate kumwabudu tu!

Mwenye macho........
 
Pole sana mkuu. Inasikitisha Sana. Meanwhile wenye pesa hata wawe na mitaala (polygamist), bado watazikwa na kanisa,. Mifano hai ipo mingi .
 
Siku hizi mapadre wamekuwa sio watumishi wa wakristu bali watumikiwa.
Najiuliza kwa hizi anasa wanazoendekeza zinazonyonya waumini kama wale wamisionari waliokuja kuinjilisha wangekuwa hivi ukristo ungeishia huko huko ulaya.

Natoa mfano mmoja, mimi ninasali kanisa katoliki Kinyerezi (parokia ya Mt Bonaventura)
Hii parokia ina nyumba nzuri ya mapadre ambayo tuliinunua kwa majirani waliozunguka kanisa, mapadre wameishi hapo si zaidi ya miaka 6.
Ni nyumba nzuri ya kisasa kabisa.

Ajabu ni kwamba wametangaza inabidi tuchange ili mapadre wajengewe nyumba ya ghorofa. Yani ile ya chini pamoja na uzuri wake wanaona sio hadhi yao.
Waumini tunaotakiwa kuchanga wengine hatuna nyumba, au nyumba zetu mbovu mbovu, lakini tukamuliwe ili padre aishi ghorofani.
Hilo nimeapa sitachanga na niko tayari ku mchallenge paroko directly
 
Toa sadakaya hiari na zaka mengine achananayo
 
Katekista!!! Acha kupotosha ukweli. Misa takatifu katika ibada ya mazishi iliendeshwa na mpakwa mafuta.
Acha uongo bhana!!.Kingunge alizikwa na Katekista,wala hakukuwa na Misa napo ni kwa vile tu familia yake ilikuwa mshirika mzuri,pia dakika za mwisho alionyesha kutaka kumrudia MUNGU lkn bahati mbaya hakuwa ametubu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…