Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

F*#ck that!
Mie nilishasema nikifa hata manispaa ikinizika hamna shida. I don't care. BTW, Roman Catholic wana double standards sana katikaa hili.
Rejea kifo cha mzee kingunge ambaye aliasi kwenda kanisani kwa muda mrefu lakini at his funeral alizikwa kikanisa.
KKKT wanaongoza kwa ndimi 2: walimzika Mengi kikanisa wakati alikosa vigezo.

Ila RC hawakumzika Mrema wa Arusha kwa mambo hayo.

Kiufupi, ukiwa mtoaji sana kanisani wanaweza kukufikiria na hata kukusamehe
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
Mtaka sifa haogopi hasara!
Wacha punda afe mzigo ufike!
 
F*#ck that!
Mie nilishasema nikifa hata manispaa ikinizika hamna shida. I don't care. BTW, Roman Catholic wana double standards sana katikaa hili.
Rejea kifo cha mzee kingunge ambaye aliasi kwenda kanisani kwa muda mrefu lakini at his funeral alizikwa kikanisa.
Acha uongo bhana!!.Kingunge alizikwa na Katekista,wala hakukuwa na Misa napo ni kwa vile tu familia yake ilikuwa mshirika mzuri,pia dakika za mwisho alionyesha kutaka kumrudia MUNGU lkn bahati mbaya hakuwa ametubu.
 
[emoji1241]Waumini wanaongezeka kwa kasi ya exponential function

[emoji1241] Kila makao mapya yanapoibuka sehemu yanakusanya wakristu wengi hivyo lazima nyumba za ibada zijengwe

[emoji1241] Vilivyokuwa vigango vinapanda hadhi ya kuwa parokia hivyo lazima miundombinu ya kiparokia ijengwe

[emoji1241] Zamani tulitegemea misaada ya wazungu kujenga makanisa lakini sasa tunasimama wenyewe

[emoji1241] Sisi hatutegemei matajiri wamepiga fedha zao kwenye biashara halafu waje wajitakase kwa kutujengea nyumba za ibada

[emoji1241]Sisi hatutegemei nyumba zilizoachwa wakfu

[emoji1241]Hivyo michango ni zoezi la mpaka kufa utawaacha wengine waendelee na haimaanishi usipo changa utakuwa na utajiri au ukichanga utafilisika hapana

Kwa miradi iliyopo chini ya kanisa, ambayo kimsingi ilijengwa kwa nguvu za waumini…. ingetosha sana kujiendesha na hata kujenga miradi mingine yakiwemo makanisa mapya ambayo ni uwekezaji.
 
Kwa miradi iliyopo chini ya kanisa, ambayo kimsingi ilijengwa kwa nguvu za waumini…. ingetosha sana kujiendesha na hata kujenga miradi mingine yakiwemo makanisa mapya ambayo ni uwekezaji.
Una Elimu kiasi gani kuhusu usimamizi na uendeshaji wa miradi??.
 
Leta ushahidi na source yake
Hata nikikuletea utasema ni uchochezi wa maadui wa kanisa.
Lakini ukweli lazima usemwe, Kanisa katoliki lina kashfa nyingi na za kweli sii tu kwenye ufisadi bali hadi mapadre kulawiti watoto huko ulaya, na wengine wanazaa na wake za watu hasa huku Africa.
Mimi mwenyewe ni mkatoliki lakini uchafu wa hili kanisa letu unatisha.
 
Mwenyezi Mungu anasema hakuwaumba majini na watu ila wapate kumwabudu tu!

Mwenye macho........
 
Pole sana mkuu. Inasikitisha Sana.
Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!

Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.

Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!

Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??
Meanwhile wenye pesa hata wawe na mitaala (polygamist), bado watazikwa na kanisa,. Mifano hai ipo mingi .
 
Siku hizi mapadre wamekuwa sio watumishi wa wakristu bali watumikiwa.
Najiuliza kwa hizi anasa wanazoendekeza zinazonyonya waumini kama wale wamisionari waliokuja kuinjilisha wangekuwa hivi ukristo ungeishia huko huko ulaya.

Natoa mfano mmoja, mimi ninasali kanisa katoliki Kinyerezi (parokia ya Mt Bonaventura)
Hii parokia ina nyumba nzuri ya mapadre ambayo tuliinunua kwa majirani waliozunguka kanisa, mapadre wameishi hapo si zaidi ya miaka 6.
Ni nyumba nzuri ya kisasa kabisa.

Ajabu ni kwamba wametangaza inabidi tuchange ili mapadre wajengewe nyumba ya ghorofa. Yani ile ya chini pamoja na uzuri wake wanaona sio hadhi yao.
Waumini tunaotakiwa kuchanga wengine hatuna nyumba, au nyumba zetu mbovu mbovu, lakini tukamuliwe ili padre aishi ghorofani.
Hilo nimeapa sitachanga na niko tayari ku mchallenge paroko directly
 
Katekista!!! Acha kupotosha ukweli. Misa takatifu katika ibada ya mazishi iliendeshwa na mpakwa mafuta.
Acha uongo bhana!!.Kingunge alizikwa na Katekista,wala hakukuwa na Misa napo ni kwa vile tu familia yake ilikuwa mshirika mzuri,pia dakika za mwisho alionyesha kutaka kumrudia MUNGU lkn bahati mbaya hakuwa ametubu.
 
Back
Top Bottom