Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Toa ndugu toa ndugu..ulichonacho..halafu unataka usitoe hilo kanisa litapelekaje injili..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje wahudumu..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje bills tofauti kama umeme na maji...
Nilijuwa watetezi hamuwezi kukosekana, hebu nieleze tu miradi ya kanisa katoliki ina faida gani kwa kanisa? Na ile benki yetu ya Mkombozi inalifaidisha vipi kanisa?

Kwani huko nyuma tuliweza vipi kujenga makanisa na mashule kwa sadaka za kawaida bila huu uharamia mpya ulioingia? Ni nini kilichobadirika?

Sisi parokia yetu ilikuwa na vigango vitatu na vyote vimekuwa parokia sasa zenye makanisa makubwa tu, tuliwezaje hayo kwa mwendo wa kawaida bila watu kunung'unika na leo kimebadirika nini?
 
Inakuwa kama mchango wa kuendesha NGO bwana! tena bora ya hiyo mnatoa ada na kiingilio kama 50,000 kwa mwaka lakini unanufaika maana siku nyingine mnaenda kula kuku pale SERENA hotel kwenye semina.

Mimi kuna siku nimeenda kusali anglicana na buku 5, michango iliyotajwa hapo ikaonekana ile hela ni takataka. Kilichoniokoa ni kwa siku hiyo alikuja askofu kwa hiyo ratiba ilibadilika kidogo wakasogeza mbele michango.
 

Hizo fedha wanapelekaga wapi ukizingatia jamaa wanasema hawaruhusuwi kuoa na wenzao hawaruhusiwi kuolewa?​

Wala hatubishanii mahesabu, hao wana fungu lao, kanisa lina kamati ya fedha wala hamna shida mahesabu, tatizo ni kukamuwa watu kupita hali halisi na vipato vya Watanzania.

Wewe angalia Mtanzania huyu mwenye kipato finyu kuna haya yanamkabili.

• Family maintenance

• Shool fees

• Michango ya kijamii, harusi n:k

• Vyama vya hiyari umoja fulani hivi au Vicoba

Hayo ni kwa uchache tu sasa jumapili unasema uende kanisani ukamuamudu Mungu unakutana na uharamia kama huu, muda wa sadaka unazidi muda wa injiri tunakwenda wapi?
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana...
Wakati unatusifia Waislamu, sisi huku wenyewe tunatamani tungekuwa na moyo wa kutoa sadaka kama wenu.

Sisi ni changamoto watu wazito kutoa sadaka, madrasa na misikiti mingi inahitaji ukarabati na shule pia. Ila watu wetu wazito mno wa kutoa sadaka. Sadaka mpaka zitokee kwa waarabu ndio madrasa zijengwe
 
Ndio maana nchi zilizoendelea makanisa yamegeuzwa museums watu walishashtuka siku nyingi kwamba huu wa sasa ni upigaji. Huku kwetu ndio bado watu wameng'ang'ania ila taratibu tutakuja kuelewana tuu.
Ni vigumu kwa vijana wa kizungu kuwaswaga kama tunavyofanyiwa waumini wa Tanzania.

Uzuri wa wazungu wana reasoning, ndio maana hata walipoleta hii dini walikuwa wanajenga wao makanisa na hospitali target yao ilipotia wakavuta end break.

Sasa ajitokeze mkatoliki hapa leo anieleze miradi mikubwa ya kanisa chuo kikuu cha SAUT mashule, mahospitali mahostel yana faida gani kwetu kama waumini tunaendelea kukamuliwa hivi?

Maana hata Martin Luther alipojitenga na Vaticano na yeye kuna mambo ya kipuuzi yalimkwaza.
 
Mavuno nadaiwa laki mbili mwisho mwezi wa sita.

Nadaiwa zaka sijarudisha bahasha hii lazima nitoe.

Leo jpili lazima nizame kanisani na sadaka 3.

Nadaiwa laki mbili mchango wa gari la Paroko...nili-pleadge.

nisipotekeleza haya nitaonekana sio mkristo
 
Wakati unatusifia Waislamu, sisi huku wenyewe tunatamani tungekuwa na moyo wa kutoa sadaka kama wenu.

Sisi ni changamoto watu wazito kutoa sadaka, madrasa na misikiti mingi inahitaji ukarabati na shule pia. Ila watu wetu wazito mno wa kutoa sadaka. Sadaka mpaka zitokee kwa waarabu ndio madrasa zijengwe
Tatizo la waislamu ni dogo sana, ni matter of generation tu.

Waislamu wanakwenda msikitini kuswali tu, tofauti na wakristo watataka kuwa na asset na miradi lakini shida ile miradi hailisaidii kanisa, sasa miradi ya nini? Hivi unajuwa kama msimbazi center tu wanatengeneza pesa kiasi gani? Halafu bado uende kanisani uendelee kukamuliwa?

Kwa style hii kanisa lisifanye biashara yoyote twende kusali tu na kutowa sadaka ya kuendesha shughuri za kanisa fullstop.
 
Kuna ile ya kuwataka waumini waliofiwa na wapendwa wao eti watoe sadaka kubwa kubwa kadri wawezavyo kama kikokotoo cha kuwawezesha hao wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki kupata ahueni ya maisha huko kaburini. Yaani mimi hii haijawahi kuniingia akilini kabisa.
 
Daaah! Nilifikiri Ni Mimi tu inafikia hatua siendi kanisani Kama ninasadaka haifiki 5000 maana utapata psychological torture but,si kweli kwamba sipendi kusali ila Kuna aibu wenzio wanaponyanyuka wote unabaki wewe tu kwenye benchi halafu unayo afya tele !kazi hasa sijui tunafanyaje wakati mwingine njia nzuri ya kusali naikosa sijui Ni ipi michango Ni kikwazo sana
 
Hujui waroma ww kama hutoi na ww huduma hupewi
Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!

Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.

Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!

Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana...

Ona waislam duniani kote wanajijua Kuna wale wajahidina na wasio wajahidina hata uende wapi duniani ukikuta muslam atakuwa kundi moja hapo ndio maana warabu wanawajengea misikiti, mda huu wa mwezi mtukufu Kuna misikiti Kila siku inatoa pesa kwa watu wasiojiweza kwenda kununua futari umeona hapo kwanini hawajaingiza ubinafsi na umimi kwenye Imani njoo kwetu Sasa

Kanisa la masanja mkandamizaji
Kanisa la mc pilipili
Kanisa la gwajima
Kanisa la mzee wa upako
Kanisa la mwamposa
Kanisa la kakobe
Na bado Kuna utitiri wa makanisa na bado wanapigana vijembe unasali wapi wewe ukisema kwa MC pilipili wanaanza kusengenya njoo uku yani

ingekuwa kula kitu moto inaruhusiwa uslam unaenda uko sema kiti moto kuacha dah ngumu, maana nishaionja Sasa kuacha ngumu
 
Back
Top Bottom