Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Duuh, pole mkuu ila kiukweli kwa miaka ya karibuni,katoliki kuna shida nyingi sana,lakini kwa vile waumini haturusiwi kuhoji basi mambo yanakwenda kama yalivyopangwa,michango imekua mingi kupitiliza,zamani mtu anajivunia kuwa mkatoliki kutokana kutokana na jinsi kanisa linavyoendeshwa.Hili nina uhakika wakatoriki wengi hatupo vizuri katika kuichambua na kuijua biblia, that's why tunapokuwa hata ktk mijadala ya kidini huwa hatuna majibu kwasababu hatusomi na kuijua biblia, viongozi wa kanisa huwa wamejikita ktk michango ambayo mingine sio muhimu kabisa.Mnaweza mkatumia miaka minne kujenga kanisa,likiisha mtaambiwa mnunue gari la padri [emoji2],kapu la mama,mambo ni mengi
Mkuu hata huko kwingine wanakosoma sana biblia, kuichambua na kuijua mambo ni yale yale.
 
Duh! Hiyo Ikihamia Huku kwetu nachukua familia yangu,Tunatengeneza kikanisa chetu Hapa Nyumbani Sadaka Tunatoa tunakula wenyewe Mimi Ndio Ntakuwa Mchungaji.Mungi yupo Popote na Yesu anaokoa mahali pote,Nikawafaidishe watu mi nyumbani familia inapiga mihayo.
 
Umesema umejikuta tu upo kwenye Ukristo

M nakushsuri jaribu kuusoma na Uislamu halafu utacompare mwenyewe ipi ni.dini sahihi
Mimi ninavyojuwa dini ni swala binafsi la mtu mahusiano yake na Mungu, hizi dini za Abraham sioni kama zinatofautiana, zote zinaongelea kitu kilekile ila tu tafsiri na mapokeo ni tofauti, vitabu ambavyo vipo kwenye biblia baadhi yake vipo kwenye Quran.

Huwezi kuamini nikikwambia huwa naita masheikh kufanya duwa nyumbani kwangu.

Tatizo la upande wa Ukristo sasa hivi viongozi wameamuwa kuwa wanyang'anyi na kuwafanyia uharamia waumini wake pasipo kuwaonea huruma.
 
🤣🤣🤣🤣🤣
Kuna ile ya kuwataka waumini waliofiwa na wapendwa wao eti watoe sadaka kubwa kubwa kadri wawezavyo kama kikokotoo cha kuwawezesha hao wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki kupata ahueni ya maisha huko kaburini. Yaani mimi hii haijawahi kuniingia akilini kabisa.
Rc ina mambo mengi hivi?
 
IMG_20220410_075810.jpg
 
Siku moja nimemtembelea mzee wangu nilipofika akaniambia anadaiwa elfu hamsini kanisani kwa ajili ya harambee.Akanieleza kuwa kila jumuiya imepangiwa kiasi flani cha fedha ambazo zimegawanywa kwa kila nyumba.Mzee wang anakaribia miaka 80..Na alinieleza kuwa siku ya harambee kila familia wanakuwa wanasomwa kanisani mnapita mbele kwenda kukabidhi hicho kiasi cha fedha na kama huna lazima utoe sababu za maana hapo na linakuwa deni mpaka ulilipe. Mambo yamekuwa magumu mno siku hizi.
 
Ukishaingia mfumo wa jumuia lazima utowe pesa ya kuwa mkatoliki kila mwezi.

Pili harambee za kipuuzi na sadaka nyingi kwenye ibada inaondoa system ya kikatoliki ambayo tulizoea ibada ya misa ya jumapili ni lisaa limoja na nusu tu na ikizidi kwa special case ni masaa mawili tu, sasa kwa huu upumbavu ulioanza ibada inakwenda mpaka masaa matatu, misa ya kwanza mnaingia saa 12 asubuhi mnatoka saa mbili na kitu.
Zamani nilikua napenda kusali Roma kwasababu ya time management, kumbe wameanza kuchelewa kutoka..?
 
Duuh, pole mkuu ila kiukweli kwa miaka ya karibuni,katoliki kuna shida nyingi sana,lakini kwa vile waumini haturusiwi kuhoji basi mambo yanakwenda kama yalivyopangwa,michango imekua mingi kupitiliza,zamani mtu anajivunia kuwa mkatoliki kutokana kutokana na jinsi kanisa linavyoendeshwa.Hili nina uhakika wakatoriki wengi hatupo vizuri katika kuichambua na kuijua biblia, that's why tunapokuwa hata ktk mijadala ya kidini huwa hatuna majibu kwasababu hatusomi na kuijua biblia, viongozi wa kanisa huwa wamejikita ktk michango ambayo mingine sio muhimu kabisa.Mnaweza mkatumia miaka minne kujenga kanisa,likiisha mtaambiwa mnunue gari la padri [emoji2],kapu la mama,mambo ni mengi
Sisi parokia yetu imezaa parokia tatu, unaweza kuelewa machozi na damu tuliyopitia.

Tuna nyumba ya masista, tuna nyumba ya mapadri ya zamani, ikajengwa ghorofa likaja hilo ghorofa likaonekana dogo utadhani mapadre wetu ni matembo tukajenga ghorofa nyingine mpya kubwa.

Tumemnunulia paroko Prado, tuna dispensary tuna maternity tuna Ambulance tuna nursery school, kama hiyo haitoshi kuna nyumba nne jirani tumezinunuwa tumevunja ndio umeanza upuuzi eti tujenge nyumba ya mama bikira Maria.

Yani the way nilichojifunza hakuna kipindi mtaachwa mpumuwe ni kutwishana mizigo mwaka mzima.
 
Toa ndugu toa ndugu..ulichonacho..halafu unataka usitoe hilo kanisa litapelekaje injili..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje wahudumu..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje bills tofauti kama umeme na maji...unataka usitoe hilo kanisa litafanyeje logistics mbali mbali...unataka usitoe maintaince na repairs ya vifaa na miundombinu mbalimbali utatoa wewe.??

Acha kulalamika sana kama huna hela kaa kutulia

Uzuri hujalazimishwa..ila mkristo wa kweli hawezi kuona kama ni wizi mana hayo ndio mahitaji muhimu ya kuendesha taasisi.

Kingine kutoa ni upendo..kiwango itachojaliwa kutoa kinatosha sana.

Kama unaona hufiti nenda huko ambako hawatoi sadaka..hakuna aliyekushikiria unabaki kanisani.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.

#MaendeleoHayanaChama
Hapana hapana hapana! Toa ulichonacho tuu hata kama umepata buku toa hiyo, Mungu huangalia moyo sio idadi ya maburungutu
 
Back
Top Bottom