Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!

Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka...
😂😂😂😂😂
 
Kuna ile ya kuwataka waumini waliofiwa na wapendwa wao eti watoe sadaka kubwa kubwa kadri wawezavyo kama kikokotoo cha kuwawezesha hao wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki kupata ahueni ya maisha huko kaburini. Yaani mimi hii haijawahi kuniingia akilini kabisa.
Duh kumbe mnaambiwa ivo poleni sanaa

yni mtu kafiliwa bado unamkandamiza kama ivo aisee iyo imani embu ichunguzeni tena
 
Zamani makanisa yalikuwa yanapata sana misaada toka nje lakini kwa sasa nje hawatoi sana misaada (wanasema mioyo yao kuhusu dini imepoa) so inabidi makanisa yajiendeshe yenyewe. Hapo ndipo uhitaji mkubwa wa hela unapoanzia
 
Wajinga ndio waliwao

Yesu Kristo hakukusanya fedha hivyo, kama tunaishi kwa mfano wa Yesu Kristo basi tukatae mambo yote ya Caeisar, hivyo wakristo lazima tuwe macho sana kwa sasa, makanisa yamekuwa ni business as usual. Bahati nzuri sana, usipotoa, hakuna mashtaka.
 
Wazungu wana akili sana. Wana strategic plans za miaka karne na karne mbele. Sisi waafrika hata kupanda miti itakayotuletea faida baada ya miaka kumi tu tunaona ni kupoteza muda na fedha maana tunataka tuwekeze usiku na kesho yake asubuhi tuone faida yake. Dini ni uwekezaji mkubwa sana wa wazungu.
 
Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!

Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka...
Mkuu kwa iyo situation ilokukuta haihitaji kufikiria mara 2 kua kanisa linakunyonya.

Sasa kma anaumwa mbona kanisa halimsaidii kitu ila wao ndo wanataka?

Laiti angekua Muislamu huyo waislamu wangejichanga wangemuhudumia badala ya yy kudaiwa huduma

Uislamu ni dini ya haki
 
Ni vigumu kwa vijana wa kizungu kuwaswaga kama tunavyofanyiwa waumini wa Tanzania.

Uzuri wa wazungu wana reasoning, ndio maana hata walipoleta hii dini walikuwa wanajenga wao makanisa na hospitali target yao ilipotia wakavuta end break...
Yaani hapo ndo kuna shida hizo faida wanazopata kutoka kwenye miradi kama mashule, mahospitali, mavyuo na mabenki na miradi mingine mingi wanapeleka wapi?
 
Mkuu unaweza nisaidia sadaka hizi tisa zilikua zipi na mlitoa kwa wakati gani?. Ili ni muhimu usiache kujibu.

Mimi kwangu ilishabaki na sali sala binafsi nyumba. Ikiwa tofauti mara moja moja naenda kanisani nasali na kuondoka. Ukweli michango imekua mingi imefika hatua hadi kanisa wanajisajili kulipa kwa mpesa au tigo pesa. Huwa siaangaiki ata na mchango mmoja. Utasikia kanisa halijaisha, shule ya chekechekea, nyumba ya sisters.

Swala la zaka sijawai toa na sitarajii kama ntakuja kutoa. Ile asilimia 10 ya kipato cha mtu inatofauti gani kodi wanayotoza TRA katika kila faida anayopata mtu. Ni onyonyaji.

Nafikiri hofu ya wengi huwa wana hofu padri hasipokuja siku ya maziko yako. Kwangu ili si hofu maana ntakua mfu sitojua walinitupa au walinivisha nguo gani. Nani alikuja msibani nani hakuja

Hapa ndio naona dini wakati mwingine ni mchongo. Haiwezekani wao wakitaka gari aua nyumba tuwachangie. Ila sisi wauumini tukitaja gari au nyumba tupige magoti tuombe sana.
 
Zamani makanisa yalikuwa yanapata sana misaada toka nje lakini kwa sasa nje hawatoi sana misaada (wanasema mioyo yao kuhusu dini imepoa) so inabidi makanisa yajiendeshe yenyewe. Hapo ndipo uhitaji mkubwa wa hela unapoanzia

Hiyo sio sbb, sadaka za Jpili peke yake zinatosha sana, na kanisa ina miradi mikubwa mingi sana, iweje ikamue waumini kiasi hicho.

Kwnn kanisa liwe na matumizi makubwa hivyo, kisa ni nn? Yesu hakuwa na hayo yote, ukiona hivyo ni binadamu wanakula fedha hizo na kuzitumia sbb zinapatikana bure bure.

Mimi kanisani naenda wakati wa Pasaka na Christmas tu, siku nyinginezo nasali kwangu na familia yangu, makanisa yamekuwa tofauti kabisa, ni kukusanya fedha na michango isiyoisha, imekuwa biashara ya uhuni sana, narudia, Yesu Kristo hajawahi kuwa hivyo, full stop
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda...
Umesema umejikuta tu upo kwenye Ukristo

M nakushsuri jaribu kuusoma na Uislamu halafu utacompare mwenyewe ipi ni.dini sahihi
 
Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!

Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka...
Duuh, pole mkuu ila kiukweli kwa miaka ya karibuni,katoliki kuna shida nyingi sana,lakini kwa vile waumini haturusiwi kuhoji basi mambo yanakwenda kama yalivyopangwa,michango imekua mingi kupitiliza,zamani mtu anajivunia kuwa mkatoliki kutokana kutokana na jinsi kanisa linavyoendeshwa.

Hili nina uhakika wakatoriki wengi hatupo vizuri katika kuichambua na kuijua biblia, that's why tunapokuwa hata ktk mijadala ya kidini huwa hatuna majibu kwasababu hatusomi na kuijua biblia, viongozi wa kanisa huwa wamejikita ktk michango ambayo mingine sio muhimu kabisa.

Mnaweza mkatumia miaka minne kujenga kanisa,likiisha mtaambiwa mnunue gari la padri [emoji2],kapu la mama,mambo ni mengi
 
Ukishaingia mfumo wa jumuia lazima utowe pesa ya kuwa mkatoliki kila mwezi.

Pili harambee za kipuuzi na sadaka nyingi kwenye ibada inaondoa system ya kikatoliki ambayo tulizoea ibada ya misa ya jumapili ni lisaa limoja na nusu tu na ikizidi kwa special case ni masaa mawili tu, sasa kwa huu upumbavu ulioanza ibada inakwenda mpaka masaa matatu, misa ya kwanza mnaingia saa 12 asubuhi mnatoka saa mbili na kitu.
Itakuwa ni huko kwenu huku kwetu hakuna mambo hayo
 
dini zilishakufa zamani.kama huna pesa wahakufikirii mfano mtu kafanya zinaa alafu shekee kaja kupiga dua na kubariki kisa tu pesa anayo.
siku hizi mchungaji anasemee zambi kisa pesa unayo
 
Mkuu unaweza nisaidia sadaka hizi tisa zilikua zipi na mlitoa kwa wakati gani?. Ili ni muhimu usiache kujibu.

Mimi kwangu ilishabaki na sali sala binafsi nyumba. Ikiwa tofauti mara moja moja naenda kanisani nasali na kuondoka. Ukweli michango imekua mingi imefika hatua hadi kanisa wanajisajili kulipa kwa mpesa au tigo pesa. Huwa siaangaiki ata na mchango mmoja...
Labda tunawachangia fedha ili kununua hayo magari na nyumba baada ya wao pia kuwa wamepiga magoti na kuomba sana!
 
Ila huduma za kiroho hupati na ukifa hatuji.
Alie design hiyo business model ya church business ni genius ndio maana alihakikisha kuna njia za kukubana ili usiache kutoa hela maisha yako yote.

Kwanza kabisa wanaanzia mbali kwa kukuingiza kwenye system tangu ukiwa mtoto mchanga kwa ubatizo. Pili unaaminishwa kwamba bila kubatizwa kanisani na kupewa sakramenti wewe si mkristo.

Hiyo yote unajengwa kisaikolojia ili uje upigwe vizuri. Baadae unaaminishwa kwamba ili uwe mkristo lazima utoe sadaka na michango yote ili "kueneza injili" na kusaidia jamii wakati kiuhalisia hamna kitu kama hicho.

Mwisho unaambiwa usipotoa michango hautazikwa na kanisa na unatishiwa usipozikwa na kanisa unaenda motoni..!!! Yaani system ipo self contained mwanangu kila kitu ni mumo kwa mumo..!

Yaani mtu unafika mahali unajua kabisa hapa napigwa, ila huna pa kutokea dadeki..!
 
Back
Top Bottom