Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Cha msìngi beba mia 7 yani shilingi mia ziwe 7,kuanzia sadaka ya kwanza adi ya 7 unanyanyuka tu na washirìka wanakuona umetoa!
Wala hutaumia,kikubwa Mungu anaona moyo wako!
Hapo ulipomalizia Mungu anaona moyo wako. Umemrudishia mpira mtoa mada.
 
namshukuru mungu nimezaliwa nikajikuta mimi ni muislamu. woow thanks god
 
Kutoa michango kanisa ni suala la kheri na kila muumini mwenye utambuzi hawezi kua na kigugumizi kwenye hili.Bila michango kanisa haliwezi kujiendesha,hii ni kwa vile hata maparokia huwajibika kuchangia harambee za kijimbo.
Shida ni utitiri wa michango,mingine ikiwa ni ile isiyokua na ulazima kmf kuchangia jiko la gesi!!!?? Mbona issue kama hizi zinaweza kumalizwa na majitoleo ya sadaka tunazotoa?
Kitu ambacho hua nakwazika nacho zaidi ni msururu wa michango wakati wa sacrament kama ubatizo,komunio na kipaimara.....mara zawadi ya kumshika askofu au shukrani ya ubatizo.....vikoro koro ni vingi mno na vinaweza hata kukwamisha waumini wenye uwezo mdogo kupata sakramenti muhimu za kikanisa.Tusigeuze makanisa kama "capitalist institutions "
Naunga mkono hoja ya mtoa post.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwenyewe kanisani huko(ukatoliki) nadaiwa michango lukuki yaani Malaki hivi na sitotoa kwa kweli

Mara mchango wa ujenzi ,mara zaka ,zote hizi ni kumi kumi halafu sadaka tatu tatu.

Halafu mwisho wa ibada kiongozi anawananga kweli kweli msiotoa

"Hutozikwa na kanisa .." aisee [emoji2]

Basi Waumini wanaingia woga kweli kweli.
 
Ona waislam duniani kote wanajijua Kuna wale wajahidina na wasio wajahidina hata uende wapi duniani ukikuta muslam atakuwa kundi moja hapo ndio maana warabu wanawajengea misikiti, mda huu wa mwezi mtukufu Kuna misikiti Kila siku inatoa pesa kwa watu wasiojiweza kwenda kununua futari umeona hapo kwanini hawajaingiza ubinafsi na umimi kwenye Imani njoo kwetu Sasa

Kanisa la masanja mkandamizaji
Kanisa la mc pilipili
Kanisa la gwajima
Kanisa la mzee wa upako
Kanisa la mwamposa
Kanisa la kakobe
Na bado Kuna utitiri wa makanisa na bado wanapigana vijembe unasali wapi wewe ukisema kwa MC pilipili wanaanza kusengenya njoo uku yani

ingekuwa kula kitu moto inaruhusiwa uslam unaenda uko sema kiti moto kuacha dah ngumu, maana nishaionja Sasa kuacha ngumu
[emoji16][emoji16][emoji16]kuacha kiti Moto tuu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3526][emoji3526][emoji3526][emoji3526]
 
Tambua kitu kimoja kwamba hii Imani ililetwa kwa gharama by then, Sasa sio wachanga Tena tunatakiwa kujiendesha wenyewe Hakuna wafadhili Tena, source of income Ni Church members tu.
Pili sadaka kanisani siyo legal compursory payment, huna na nafsi yako inakusaidia huna, relax only God knows.
Sadaka au michango kanisani siyo quid pro quo, Ni shukrani kwa MUNGU wako kwa uhai ulionao.
Pia umesema umezaliwa umejikuta tu mkristo, now umekua jifunze KWELI then ubatizwe kwa maji mengi upokee kipawa cha ROHO mtakatifu, uwe na ujasiri wa kuahinda dhambi.
Mwisho hudhuria kanisani kila Sunday service Ni nzuri kwa afya ya kiroho.
 
Alafu unaiomba serekare iingilie kati,huo ushubwana peleka kule.
kama hujitambui kakufe mwenyewe.hata hivyo anayetoa zipo kama hazipo anatoa nini?
 
Watu weng wamekimbilia kuabudu kwa "manabii" na "mitume" maana wana amini huko kuna miujiza.. hivyo makanisa yetu yamebaki wazi waumin wamepungua sana
 
Toa ndugu toa ndugu..ulichonacho..halafu unataka usitoe hilo kanisa litapelekaje injili..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje wahudumu..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje bills tofauti kama umeme na maji...unataka usitoe hilo kanisa litafanyeje logistics mbali mbali...unataka usitoe maintaince na repairs ya vifaa na miundombinu mbalimbali utatoa wewe.??

Acha kulalamika sana kama huna hela kaa kutulia

Uzuri hujalazimishwa..ila mkristo wa kweli hawezi kuona kama ni wizi mana hayo ndio mahitaji muhimu ya kuendesha taasisi.

Kingine kutoa ni upendo..kiwango itachojaliwa kutoa kinatosha sana.

Kama unaona hufiti nenda huko ambako hawatoi sadaka..hakuna aliyekushikiria unabaki kanisani.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.

#MaendeleoHayanaChama
Ww ni mpumbavu sana usijibu watu nyodo si nenda ukatoe kimyakimya hiyo sadaka mwenzako anazungumzia uwingi wa uitisho wa sadaka vikapu 6 mpaka 7 kwanini isiwe vikapu 2 au 3
 
Wala hatubishanii mahesabu, hao wana fungu lao, kanisa lina kamati ya fedha wala hamna shida mahesabu, tatizo ni kukamuwa watu kupita hali halisi na vipato vya Watanzania.

Wewe angalia Mtanzania huyu mwenye kipato finyu kuna haya yanamkabili.

• Family maintenance

• Shool fees

• Michango ya kijamii, harusi n:k

• Vyama vya hiyari umoja fulani hivi au Vicoba

Hayo ni kwa uchache tu sasa jumapili unasema uende kanisani ukamuamudu Mungu unakutana na uharamia kama huu, muda wa sadaka unazidi muda wa injiri tunakwenda wapi?
Hata biblia hawasomagi kabisa wao pesa mbele
 
Wakati unatusifia Waislamu, sisi huku wenyewe tunatamani tungekuwa na moyo wa kutoa sadaka kama wenu.

Sisi ni changamoto watu wazito kutoa sadaka, madrasa na misikiti mingi inahitaji ukarabati na shule pia. Ila watu wetu wazito mno wa kutoa sadaka. Sadaka mpaka zitokee kwa waarabu ndio madrasa zijengwe
Nyamaza kwanza uzi uishe usitukorofishe tumeshaamua Moslem ndii lilmodo wetu kwa huu uzi [emoji23][emoji23]
 
Ona waislam duniani kote wanajijua Kuna wale wajahidina na wasio wajahidina hata uende wapi duniani ukikuta muslam atakuwa kundi moja hapo ndio maana warabu wanawajengea misikiti, mda huu wa mwezi mtukufu Kuna misikiti Kila siku inatoa pesa kwa watu wasiojiweza kwenda kununua futari umeona hapo kwanini hawajaingiza ubinafsi na umimi kwenye Imani njoo kwetu Sasa

Kanisa la masanja mkandamizaji
Kanisa la mc pilipili
Kanisa la gwajima
Kanisa la mzee wa upako
Kanisa la mwamposa
Kanisa la kakobe
Na bado Kuna utitiri wa makanisa na bado wanapigana vijembe unasali wapi wewe ukisema kwa MC pilipili wanaanza kusengenya njoo uku yani

ingekuwa kula kitu moto inaruhusiwa uslam unaenda uko sema kiti moto kuacha dah ngumu, maana nishaionja Sasa kuacha ngumu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa uzoefu wangu mdogo wa eneo nililokulia, zamani kulikuwa na mapadre wazungu, ambao mashirika yao na waumini wa huko ulaya, walikuwa hawaishi kuleta pesa,magari, mitumba, chocolate na biskuti, ambacho, viliwezesha kujenga makanisa, shule, na nyumba za mapadre na masista. Nafikiri siku hizi mambo yamebadilika, kama wapo wazungu ni wachache, na wazawa ndio wanashikilia uongozi na hakuna misaada kama ya mwanzo. Sasa hii michango lukuki kama inakwenda kimahesabu au ni ulaji, hilo sijui.
Tatizo unchanganya UKWELI NA UWONGO acha kupotosha
 
Back
Top Bottom