Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Mkuu hata huko kwingine wanakosoma sana biblia, kuichambua na kuijua mambo ni yale yale.
 
Duh! Hiyo Ikihamia Huku kwetu nachukua familia yangu,Tunatengeneza kikanisa chetu Hapa Nyumbani Sadaka Tunatoa tunakula wenyewe Mimi Ndio Ntakuwa Mchungaji.Mungi yupo Popote na Yesu anaokoa mahali pote,Nikawafaidishe watu mi nyumbani familia inapiga mihayo.
 
Umesema umejikuta tu upo kwenye Ukristo

M nakushsuri jaribu kuusoma na Uislamu halafu utacompare mwenyewe ipi ni.dini sahihi
Mimi ninavyojuwa dini ni swala binafsi la mtu mahusiano yake na Mungu, hizi dini za Abraham sioni kama zinatofautiana, zote zinaongelea kitu kilekile ila tu tafsiri na mapokeo ni tofauti, vitabu ambavyo vipo kwenye biblia baadhi yake vipo kwenye Quran.

Huwezi kuamini nikikwambia huwa naita masheikh kufanya duwa nyumbani kwangu.

Tatizo la upande wa Ukristo sasa hivi viongozi wameamuwa kuwa wanyang'anyi na kuwafanyia uharamia waumini wake pasipo kuwaonea huruma.
 
🤣🤣🤣🤣🤣
Rc ina mambo mengi hivi?
 
Siku moja nimemtembelea mzee wangu nilipofika akaniambia anadaiwa elfu hamsini kanisani kwa ajili ya harambee.Akanieleza kuwa kila jumuiya imepangiwa kiasi flani cha fedha ambazo zimegawanywa kwa kila nyumba.Mzee wang anakaribia miaka 80..Na alinieleza kuwa siku ya harambee kila familia wanakuwa wanasomwa kanisani mnapita mbele kwenda kukabidhi hicho kiasi cha fedha na kama huna lazima utoe sababu za maana hapo na linakuwa deni mpaka ulilipe. Mambo yamekuwa magumu mno siku hizi.
 
Zamani nilikua napenda kusali Roma kwasababu ya time management, kumbe wameanza kuchelewa kutoka..?
 

sigh
/sʌɪ/
emit a long, deep audible breath expressing sadness, relief, tiredness.
Similar:
breathe out
exhale
groan
moan
suspire
noun
a long, deep audible exhalation expressing sadness, relief, tiredness, or similar.
"she let out a long sigh of despair
 
Sisi parokia yetu imezaa parokia tatu, unaweza kuelewa machozi na damu tuliyopitia.

Tuna nyumba ya masista, tuna nyumba ya mapadri ya zamani, ikajengwa ghorofa likaja hilo ghorofa likaonekana dogo utadhani mapadre wetu ni matembo tukajenga ghorofa nyingine mpya kubwa.

Tumemnunulia paroko Prado, tuna dispensary tuna maternity tuna Ambulance tuna nursery school, kama hiyo haitoshi kuna nyumba nne jirani tumezinunuwa tumevunja ndio umeanza upuuzi eti tujenge nyumba ya mama bikira Maria.

Yani the way nilichojifunza hakuna kipindi mtaachwa mpumuwe ni kutwishana mizigo mwaka mzima.
 
Hapana hapana hapana! Toa ulichonacho tuu hata kama umepata buku toa hiyo, Mungu huangalia moyo sio idadi ya maburungutu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…