Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Mdau anauliza, mbona zamani haikuwa hivyo? Kuna bills na huduma gani zinazofanya kuwe na utitiri wa sadaka na matoleo mengi tofauti na zamani?
 

Mimi nipo Tabora, mbona hakuna huu mfumo?
 
Duuh
 
N
Nenda kanisa la masanja wao hawatoi sadaka Wala michango
 
N
Nenda kanisa la masanja wao hawatoi sadaka Wala michango
 
Mimi ni mkrist asiye udhuria kanisani lakini naikubali sana dini ya kiislamu, iko very social na hawana bla bla nyingi
 
Ukifa hawakuziki. Hapo ndipo wametushika pabaya

Acha uongo, hakuna mtu hazikwi kiss hajatoa michango. Mtu ambaye ana hatari ya kutozikwa ni yule ambaye ameasi, Yani haonekani kanisani muda mrefu na Wala Hana ushirika na waumini wengine.
 
Uzuri wake ni kuwa usipotoa si kosa la jinai.
Mkuu, ungelikuwa unaingia kanisani,hasa hilo Katoliki aliloliongelea, nadhani usingelicomment hivi.

Yaani ukiingia humo ndani hakuna pa kukwepea kutoa hizo sadaka.

Na kama hauna kitu ni bora usiende utaaibika kwa kujisikia dhalili.

Mfumo wa utoaji sadaka wa zamani ulikuwa ukiheshimu utu wa mtu asiye nacho.

Ilikuwa muda wa kutoa sadaka baada ya kiashiria cha wimbo wa "toa ndugu", basi kila aliyeandaa sadaka yake hupita mbele na kwenda kutumbukiza kwenye box la sadaka.

Sasa hivi utaratibu ushabadilishwa, watu mnasimama kwa safu ya mabenchi bila kuachwa mtu, utaratibu huo anaolalamikia hufanywa zaidi ya mara moja kwa misa moja!

Baada ya hapo zinawafuata bahasha zenye maudhui ya tozo mbali mbali kwenye Jumuia zenu.
Na unyenyekevu wote huo mtu anaufanya kwa kutetea asitengwe, basi.
 
Usilalamike sana, chukua hatua zifuatazo.
1. Acha kutoa hizo sadaka (michango), au toa ile inayokugusa tu, mingine kaa kimya, hakuna mtu wa kukufanya lolote.

2. Tafuta chenji za kutosha ukiwa unakwenda kanisani. Kama ukikuta sadaka za kutoa ni tano na wewe ulipanga kutoa sadaka ya jumla ya shilingi mia tano tu, basi chenji hiyo mia tano ili kupata sarafu za mia mia ziwe tano, kisha kila ukitakiwa kutoa sadaka unadondosha jiti tu kwenye chombo cha sadaka.
 
Acha uongo, hakuna mtu hazikwi kiss hajatoa michango. Mtu ambaye ana hatari ya kutozikwa ni yule ambaye ameasi, Yani haonekani kanisani muda mrefu na Wala Hana ushirika na waumini wengine.
Ni wapi nimesema usipotoa mchango huzikwi?
 
Wakati Niko mdogo, nakumbuka mlezi wangu alikuwa anabananishwa kuchangia pesa ya kununua/kujenga chuo cha RUCU Iringa. Sijui pesa huwa wanapeleka wapi! Hospitals, Dispensaries, Mashamba, Shule kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…