Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Mzee Matola,wewe Unaumwa ugonjwa wa Sonona,mada iliyopo mbele yetu ni juu ya Sadaka na Michango mbalimbali, Sehemu uliyoiquote ni jibu langu kwa muuliza swali kuhusu Taratibu za mazishi,sasa hbr ya Akina Galileo Galilei imekujaje hapa?,Oh!!,mara wewe Hujui kitu,kipi nisichojua kuhusu Kanisa langu Katoliki??, Sasa km kwa upeo wako umeona sijui Kwanini unaniquote na kutoa comment yako??.Anyway Jitahidi kupunguza mawazo ya chuki za kidini utaishi kwa furaha sana.
Sema jamaa anasema ukweli ....
 
Hichi ni kitabu gani tena maana najua vilikuwepo vitabu 66 hiyo wakabayo imetokea agano gani tena,turudi kwenye mada hiyo sadaka anaondoka nayo padri inaenda jimboni ama?
Hicho ni miongoni mwa vitabu sita vilivyo chomolewa na Martin Luther, hivyo Waprotestanti hamna.Hiyo sehemu inahusu kuombea wafu.Sadaka hiyo hupelekwa Parokia I kwaajili ya kumwombea misa ya wafu huyo Marehemu.
 
... kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.
... kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka
Mimi nijuavyo misa ya Kikatoliki isiyokuwa na tukio maalum la sherehe au sakramenti huwa haizidi saa moja na nusu. Umesema mmeinuliwa mara saba kutoka katika benchi, na nafsi yako inashuhudia hayo kwamba uliyosema ni ya kweli, kwamba mmeinuliwa kutoa michango mara saba! Kwangu mimi hiki kitu ni kipya kabisa katika Kanisa Katoliki, na siwezi kukupinga kwa kuwa nafsi yako imetoa ushuhuda huu hadharani, na kwamba ushuhuda huu ni wa kweli. Ninachoweza kusema ni kwamba kama uyasemayo ni kweli kabisa, basi yanahitajika marekebisho makubwa hapo Parokiani kwenu, maana Paroko kuruhusu misa kuwa ndefu kiasi cha kutoa sadaka kwa kuinuka mara saba sio jambo la kawaida
 
Kwani watoto wasipobatizwa wanakwama wapi mi kuna mguso ninao kuwa haya ma dini wanatutishia MUNGU ili watukamue.Siku hizi ukikwama na ukaenda church kuomba msaada wa hata chakula hawakupi ila wao wakati wa mavuno wanachagua eti mpuka kuanzia debe mbili as if tulisaidiana hela za mbolea
Hakuna anayekutisha Mzee mzima,na wala haulazimishwi.
 
Hicho ni miongoni mwa vitabu sita vilivyo chomolewa na Martin Luther, hivyo Waprotestanti hamna.Hiyo sehemu inahusu kuombea wafu.Sadaka hiyo hupelekwa Parokia I kwaajili ya kumwombea misa ya wafu huyo Marehemu.
Kuhusu hilo nisikubishie ntakuwa nakutenda vibaya ,sema nini me napenda kitu inaitwa logic!
 
Suala la sadaka na zaka kwa karne hii naona inamantiki Sana kama utaitumia sadaka yako na zaka yako kusaidia wahitaji na wasiojiweza kuliko kutoa kwenye makanisa ambayo Sasa yamegeuka biashara. There are a lot of needy people out there wanahitaji msaada.

Yah na hii ndio imani ya kweli. Au ibada safi
 
Namshukuru Mungu sna saivi mm wala kanisa halimipi presha nimeamua kuishi vile naona sahihi kama kuzikwa na pdri hii denia watu wengi Tu wanakufa bila kuzikwa
 
Siku hizi mapadre wamekuwa sio watumishi wa wakristu bali watumikiwa.
Najiuliza kwa hizi anasa wanazoendekeza zinazonyonya waumini kama wale wamisionari waliokuja kuinjilisha wangekuwa hivi ukristo ungeishia huko huko ulaya.

Natoa mfano mmoja, mimi ninasali kanisa katoliki Kinyerezi (parokia ya Mt Bonaventura)
Hii parokia ina nyumba nzuri ya mapadre ambayo tuliinunua kwa majirani waliozunguka kanisa, mapadre wameishi hapo si zaidi ya miaka 6.
Ni nyumba nzuri ya kisasa kabisa.

Ajabu ni kwamba wametangaza inabidi tuchange ili mapadre wajengewe nyumba ya ghorofa. Yani ile ya chini pamoja na uzuri wake wanaona sio hadhi yao.
Waumini tunaotakiwa kuchanga wengine hatuna nyumba, au nyumba zetu mbovu mbovu, lakini tukamuliwe ili padre aishi ghorofani.
Hilo nimeapa sitachanga na niko tayari ku mchallenge paroko directly
😂😂 Hapo kuna kitu sio sawa kama uzi huu unavyonadi. "..Yani ile ya chini pamoja na uzuri wake wanaona sio hadhi yao". Mkuu, Simamia hapo-hapo kidedea.
Kwani walioishi hapo hiyo miaka takribani 6 hawakuwa Mapadre?
Ila narudia tena Ila kama haijitoshelezi kwa mfano Nyumba na Ofisi au Huduma kwa Idadi ya wale wanaoishi hapo e.g. Uwepo wa Masister, Ukumbi wa mikutano, Huduma Mtambuka e.g. Vyoo, Bafu,Stoo, mahali pa chakula au Jiko la ndani n.k. na Eneo lililopo ni dogo au finyu. Kweli inabidi Mjinyime/Mjibane zaidi lakini pia kuwe na maboresho kimawasiliano kwa mfano kutumia neno linaloonesha kudharau au Kubeza e.g. sio Hadhi ya mapadre....sio kauli nzuri. Pia namna nzuri na ya unyenyekevu Kuwahamasisha Waumini ili washiriki kutoa michango kwa Hiari bila vitisho.
 
Hizo fedha wanapelekaga wapi ukizingatia jamaa wanasema hawaruhusuwi kuoa na wenzao hawaruhusiwi kuolewa?
Wanapata posho ndogo sana, fedha nyingi zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya kanisa. Mfano ni ununuzi wa viwanja kwa ajili ya vigango vipya, ambavyo baadaye huwa Parokia. Lakini kuna fedha za mavuno, hizi huwa si mali ya Parokia, huwa zinaenda Jimboni na kuwa ruzuku kwa Parokia zisizojiweza, mfano Parokia iliyopo Rufiji kwenye waumini wasiozidi 200, haiwezi kujitegemeza bila ya ruzuku kutoka Jimboni. Tuondoe mentality ya kuwa kila matoleo ni kwa ajiliya matumizi ya mapadre, labda madhehebu mengine ila sio RC
 
Kuna ile ya kuwataka waumini waliofiwa na wapendwa wao eti watoe sadaka kubwa kubwa kadri wawezavyo kama kikokotoo cha kuwawezesha hao wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki kupata ahueni ya maisha huko kaburini. Yaani mimi hii haijawahi kuniingia akilini kabisa.
Kwa hili niliwahi hudhuria msiba wa ndugu yangu mkatoliki nikasikia hii, nikasema duuuh kwa hili asee watu wanapigwa , kwa Hy wale wenye wapendwa wao wanao wapenda Sana wawatolee hao ndugu mpaka lini, ? Manaka hata tukitenda dhambi tujivunie kuwa huku dunian watakao Baki watanitolea sadaka ili nisamehewe? Alie anzisha hili jambo aliwapiga na kitu kizito kichwani
 
Umeshawahi kufuatwa au kulazimishwa kutoa sadaka? Umeshawahi kusitishiwa huduma yoyote mf ekaristi kitubio n.k Kisaa haujatoa sadaka? Umeshawahi kwenda kusali ukaambiwa hapa wanaingia waumini waliochangia ujenzi wa kanisa pekee? Kanisa uliloenda unajua waliochangia mpaka Leo unaingia bila shida??
 
Milele Amina mkatoliki mhenga mwenzangu,

Umeandika hoja moja muhimu ambayo kama huna mihemuko ya dini utaona ni kiasi gani ukristo wetu unatoka kwenye imani.

Binafsi huwa nashangaa na jinsi polepole tunavyokuwa brainshwashed kuwa kutoa kuwa direct relationship na kuingia mbinguni au luwa mkristo bora. Naamini kubwa la kupata kwenye misa ni mahubiri, maelekezo yatakayonifanya niwe mkatoliki mkristo bora then niwe mtu mwema na nisaidie kwa kadri ninavyoguswa.

Leo hii tuna michango hii ambayo inaandikwa majina na ukikosa kila mtu anakutolea macho; sadaka, tuna zaka , tuna tegemeza jimbo, wawata, uwaka, utoto mtakatifu , viwawa, mavuno ( hii tunayo kwetu), shukrani ya mwaka ( tunayo kwetu), bahasha ya mtoto Yesu krismas, bahasha ya pasaka, mapaju jumuia ikihudumu kila familia elf 10, ujenzi wa kanisa ( letu tunachangaga ujenzi since 2005 _ 17 yrs back) na halijaisha.

Jumuia tuna mchangonwa familia kila mwezi , sadaka ya jumuia jumamosi .

Hizi ni fixed ila kuna zile adhock askofu anatembelea tumpe zawadi, gari la mapadri , nk nk

Sawa kanisa linategemezwa na waamini but come on tusiwe vipofu hivi to what extent??? Mbona kanisa hili halitoi kwa waamini? Na bado hakunaga usawa hata msemeje hakuna usawa - uwe na mgonjwa anataka sacrament ya wagonjwa utapita mlolongo huo balala. Hao wanaoniita makatekista ndio wakwanza kuwa warasimu .
Nimewahi kuomba mtoto ninaemlea miaka 6 agongewe muhuri tu alitaka kijiunga seminari dah nilienda pale parokiani mara 4 , nikaulizwa mambo yasiyihusiana na issue husika ( je namlea kivipi, je yuko kwenye sensa ya waamini na nimemtolea mchango wake - hamtaamini ila it was pathetic nilimjibu katekista na padre vubaya sana kuwa kama issue ni muhuri naweza kuchongesha ila kwa kujali ukristo wa mtoto nimefuata taratibu.

In short viongozi hawa wakatoliki wasioobadilika wajue wao ndio kikwazo kikuu na sababu ya waamini kukimbia kanisa na andiko linasema ole wake anaesababisha makwako kwa wengine.

Kuna siku jumuia yetu ilikuwa na zamu yanusafi na jumapili yake kupeleka mapaji ...hii ya mapaji nayo imekuja miaka hii ya 2000 zamani haikuwepo ; wasio wakatoliki mapaji ni kama mayai,sabuni, mahitaji ya kutumia mapadre ina week ( najiulizaga kama tunatoa sadaka iendeshe nyumba ya mapadre mapaji ya nini ila ndio kwa ufinyu wetu ukiuliza unaambiwa una lucifer kichwani) now back to the story, katekista akatuma ujumbe kuwa mapaji tunayopelela yawe ya aina fulani sabuni, mayai nk , nilitafakari sana tumefikia hapa mapadre au katekista anachagua sio mbaya sawa ila alikuwa aki dictate na brand za margarine, cooking oil. Tukumbuke kanisa ni kimbilio la wanyonge je wale wahitaji kanisa lina give back vipi kwao. Miaka 2 nyuma tulikuwa na harambee ya kununua gari la mapadre waumini wakasema tununue Rav4 ,mapadre walikataa wakataka navara tukasema jamani parokia iko mjini na inahudumia wanaparokia kwanini hawataki rav4 - we never won na prado lilinunuliwa. I can go on and on ila tuna tatizo kubwa sana kanisani.

Hiinya kupangiana sasa zaka ,eti nijaze form na mshahara wangu ndio naona mpya kanisa, who brough us here ? Nijaze napata laki 2 ,so kanisa linadai elf 20 bila kujali nina mama mkwe, wategemezi, watoto ,nk nk . Wanasema fungu la 10 ni strickt asimilia wanasahau tuna operate in a complete different environment ya tozo kila pahala.

Binafsi naipenda sana imani yangu ila nakwazwa sana na behavior ambazo zinaonekana ni strategy kuwba kuanzia juu hadi chini. Inakera zaidi wanapoogopesha waamini kuwa kutoa ni tiketi ya ukristo bora ,kuzikwa ni ishara njema , watasema ooh marehemu alilipenda kanisa ,what nonsense?? Bora waseme marehemu alisaidia majirani hata kama alikuwa mpagani.

Uzi huu usomwe na makasisi warekebike ,wanatukwaza kwa. Kwa kiwango cha juu sana. Kizazincha vijana chipukizi kinakuja na reasoning power na wasipoangalia watakosa waamini.

Sijui tunashun

Ufike hadi huko italy wausome na michangi yote. Maana tukija kuongelea kanisani tutaonekana wapinga kristo. We padri apewe mapaji ambayo ni matumizi yake kusaidia kuishi parokiani. Tena atake sadaka ni mbaya
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
Ukiona mambo ya kanisani hauyaelewi , nenda kaabudu mizimu yenu.
 
😂😂
 
Back
Top Bottom