Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!

P kama P wa miaka ile, hongera.
 
.
 
Hahahaaaa, nimecheka sana. Na zanzibar itafikia level ya mauritius, kisha watavunja muungano tuanze upya na Tanganyika yetu
Hakuna lisilowezekana chini ya jua !
Naiona Zanzibar iking’ara kama ilivyokuwa zamani za kale 🥰

Nchi ya kwanza kuwa na TV 📺 ya Rangi Africa 😅

Nchi ya kwanza kuwajengea majumba makubwa wananchi wake na kuwapa waishi bure katika Africa !

Au nasema uongo ndugu zanguni ??!
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni 😅🙏🙌😂🙏
 
Kwani Habari yako ilihitaji blah blah zote hizi ili kueleweka?
 
Mimi nashangaa ni kwanini mtu ashauriwe asigombee ilihali Chama chake kinataka agombee ?

Suala la kama hatakiwi na Wananchi walio wengi basi suala hilo liachiwe kwa wapiga kura !

Maana wao wapiga kura ndio watakaoamua ama wamchague yeye ama wamchague mgombea mwingine wa Chama kingine cha Upinzani !

Just as simple as that ! Kwa sababu Uchaguzi Mkuu huo wa 2025 utakuwa na wagombea wengine wa URAIS kutokea vyama vingine vya siasa !!

Ni kwanini mnakuwa kama vile mmeshafanya uamuzi kwamba mtu atakayeshinda URais ni LAZIMA atokee Chama Tawala ??!!

Ina maana kumbe Uchaguzi utakuwa ni kiini macho tu kama alivyokwisha kutanabahisha Nape Nnauye ???!

Bado sijaona mantiki ya watu wengine nje ya Ccm kumtaka mgombea wa Ccm asigombee eti ili kusitokee matatizo mbele ya safari !

Waachieni CCM wenyewe waamue nani apeperushe bendera ya Chama chao !

Kisha Wananchi wataamua kama anatosha watamchagua kwa kura nyingi !
La kama hawamtaki watamchagua mgombea mwingine wa kutoka Chama chochote kile kitakachoweka mgombea watakayemtaka !
JUST AS SIMPLE AS THAT !

Acheni kuongea kama vile hakutakuwepo na Uchaguzi bali utakuwepo Uteuzi tu 🙏🙌👍
 
Waeleze Hawa chawa ushabiki tu hawaoni mbele
 
Dunia inakoelekea haitabiriki

Kila nikiwaangalia Ruto na Sir Starmer sioni furaha ya kuongoza kwenye nyuso zao 🐼
Hao Walidhani wanaenda kuiba na kula Raha
Mama Abdul anadhani bandari itampa familia hela nyingi

Atapata shida kuongoza post 2025 na nchi itavunjika vipande vipande
Asithubuti kugombea, wapambe wanamdangaya

Hi haiitaji utabiri wa Pasco Kila mtu mwenye akili anaona
 
Wanamtahadharisha tu. Inaoneka kuna mitego imewekwa, sema haambiwi ila hawa waleta mabandiko ndio malaika wenyewe sasa. 😃😃😃.
Mkuu Mpalakugenda , umesema jambo moja kubwa sana, kuna watu wanadhani malaika ni viumbe weupe wana mabawa wanaruka angani, kumbe sauti kama HII inaweza kabisa kuwa ndio sauti ya malaika mwenyewe wa Mungu!, watu wajinga wajinga watadharau kuwa huyu sini Paskali tuu atatuambia nini?!, kumbe sio Paskali bali ni YEYE mwenyewe anasema nasi kupitia Paskali.

Tembelea hapa uone nilimshauri nini yule Blaza wangu, Magufuli, "Kama Unaona Kazi ya Urais ni Ngumu Kwako, Jiuzulu! ". Mwaka 2017 kwenye andiko hili Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” nilishauri hivi Na mwezi April mwaka 2020, nilipandisha bandiko hili humu "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza humo nilishauri You never know, kama Blaza angesikiliza ushauri huu, labda saa hizi, angekuwepo!.

Na kuhusu katiba enzi za JPM, alipoingia kwa vile anajua atakaa vipindi viwili, japo issues ya katiba ilikuwepo kwenye ilani yake ya uchaguzi iliyomuingiza Ikulu, yeye akasema katiba sio kipaumbele chake!. Hili nililiulizia humu Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?

Kwavile mimi ni good trends reader kuhusu katiba, enzi za JPM, niliwaletea hii trends Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!

The same scenario inataka kujirudia kwa Rais Samia, she has a chance to make things right now kuhusu minimum reforms za Katiba, kwa vile na yeye amehakikishiwa ni yeye 2025, hili la Katiba, analiweka kiporo kwasababu anajua ana ample time 2025-2030, tuendelee kumsisitiza, if there is anything she can do under her powers kuhusu katiba, she better do it now, because no one knows about tomorrow, ndio maana tumemshauri Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Mama bado ana muda to make things right.

P
 
KWANI HUYU MAMA ATAPITA URAIS 2025?
 
Wewe Pascal sijui unamaanisha nini kwa kweli. Watanzania wengi wanajua Samia ni rais wa katiba tu. Wamekua na hofu kipindi cha mpito wakiona akiingizwa kwenye majaribu hatari kutaka kugeuza misingi ya siasa na itikadi inayoongoza taifa. Wanaccm asilia waliogopa sana pale kuona balozi wa marekani anakaribishwa makao makuu ya ccm. Wanaojua hila za marekani kugeuza kila nchi kikaragosi wake watanielewa. Ilikua kama kumleta shetani makao makuu ya CCM. Tutamuona mtu mwema kama mama akisimamia nchi kupata Kiongozi mwingine aina ya John Pombe Magufuli ili kurejesha taifa kwenye njia ya kweli ya maendeleo kwa umma wa wananchi. Akifanya hivyo hakika tutamkumbuka na kumpa heshima kubwa.
 
Mkuu Paskali, ukiitwa ukaambiwa uthibitishe hizi kauli zako, je utaweza?
Kwanini mimi ndie niitwe kuthibitisha kitu nilichosikia badala ya kumuuliza aliyetamka alimaanisha nini?. Mtu atoe tamko, anayeripoti kuhusu hilo tamko ndie ahojiwe badala ya aliyetamka!.

Hata issue ya zile pyu pyu za yule jamaa yetu, kuna mtu alitamka kitu hadharani kuhusu vita vya kiuchumi, na akamtaja mtu not expressly but impliedly, huyu aliyetajwa, zikamshukia pyu pyu za kutosha, niliposhauri aliyetoa kauli ile ahojiwe alimaanisha nini, niliambiwa nitahojiwa mimi! Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana
Kinga ni ya kutokushitakiwa!, hakuna kinga ya kuhojiwa!.
P
 
Hii nchi tunaishi kwa ulaghai nanukishakua mkweli basi ujue unakua treated kama muhaini na kua sio mzalendo ila ukweli ni kwamba masisiemu hayako tayari kwa uchaguzi huru wakati wowote hivyo nchi hii uchaguzi ni takwa tu lakini nigelesha ndio mana hutaina sikubwakikubali matokeo kupingwa mahakamani wanajua kabisa ndio mwisho wao utakapofika nakuvuna aibu hivyo wataendelea kuhodhi mifumo yote ili kuendelea kusalia madarakani kwa gharama yoyote na kama taifa tusitegemee miujiza toka kwa watu hawa mana wanafanya wanayoamua wao na sio matakwa ya wananchi tuombe Mungu atujalie huko siku za usoni kama tutapata kizazi ambacho kitaona umuhimu wakuwajibika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…