Kuna mahali viongozi wa nchi yetu wanatukosea Sana wananchi

LandCruiser Hardtop 4X4 tena ina mkonga nje ingependeza sana !
Bei nafuu ya kununulia na ni imara zaidi na maintainance yake ni rahisi sana !

Kila ndege huruka kwa ubawa wake !
Kama Nchi ni masikini tuende hivyo hivyo kwa umasikini wetu !

Wapo Viongozi waliokuwa wakitembelea LandRover 109 na hawakutenguka viuno !

Kupanga ni kuchagua !
Naona tumechagua Kazi na Bata !
Kazi kidogo Bata mingi 🤣👍🙏
 
LandCruiser Hardtop’s white colour 4X4 inapita popote pale ambapo hata mavieite hayawezi kupita !
Kupanga ni kuchagua !
Sema tu tumechagua hivyo !
 
jikuma wewe hao mawaziri wanazunguka kwa issue gani zaidi ya kumsifia mama abdul na kukata mauno stejini wanazunguka sababu wana mafuta ya walipa kodi si kutatua shda za watz wanazunguka kulipana maposho hakuna jipya no maji, no ajira, no walimu, no madawa, no madawati nk
 
LandCruiser Hardtop’s white colour 4X4 inapita popote pale ambapo hata mavieite hayawezi kupita !
Kupanga ni kuchagua !
Sema tu tumechagua hivyo !
Ukienda kijijini kwetu, kufika kwanza hakuna lami ni changarawe tu, mvua ikinnyesha ni kasheshe kwa (4x4) RAV4.

Ukishamaliza hiyo njia ya changarawe hata siku nzuri unaingia mabondeni, hata hiyo RAV4 aiendi inabidi mshuke muanze kutembea kwa miguu kama mita 500 hivi ndio mfike.

Sasa hawa mawaziri na wakuu wa mikoa maeneo mengine iwe mvua au jua ndio ziara zao za kila siku na njia zingine hata hiyo barabara ya changarawe hakuna.
 
Ukitaka kuona una matatizo soma mada uone, mpaka sasa watu wanapingana kwa hoja kwenye ku-justify ni haki au la ya viongozi kuwa na magari wanayopewa.

Sasa wewe huna hoja zaidi ya kutukana watu, unafaidika na nini kutukana watu; kwenye mjadala.
 
Ndio maana nikawachagulia LandCruiser Hardtops rangi nyeupe tena zina mikonga ya kupumulia nje ili hata kwenye mito na mabwawa au maronga ipite bila kuvuta maji kwenye Injini !
Tena ni 4X4 ya Ukweli ikiwa na injini ya One HZ !
😅 Kupanga ni kuchagua !
 
Sasa hapo solution nikujenga barabara za lami au kununua hayo maV8 ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…