Kuna mahusiano kati ya kuacha pombe na kukosa usingizi(Insomnia)?

Watu hawaachi pombe wanapumzika

Ila sema Kuna muda tungi likiwa high mwili unakuambia usiendelee usije ukacheza Yope ukweni
 
Ni kawaida kupata insomnia wiki za mwanzo baada ya kuacha pombe, especially kama ulikuwa umezoea kunywa mara kwa mara. Mara nyingi hali hupungua taratibu kadri mwili unavyozoea bila pombe.

Cha kufanya,
  • Epuka simu/series usiku sana.
  • Punguza kahawa au energy drink jioni.
  • Fanya mwili uchoke mchana.
  • Lala na kuamka muda uleule kila siku.

Usikimbilie kurudi kunywa kwa sababu ya usingizi. Ila ukipata dalili kali kama kutetemeka sana, anxiety kali, jasho kupita kiasi au kukosa usingizi kabisa siku nyingi, muone daktari.

Jipe muda wa ku-heal, jitahidi kula bilinganya pia!yanasaidia kupata usingizi!
 
Ukikomaa unatoboa bila kufanya chochote kama unakula na unafanya kazi au mazoezi ya nguvu kidogo (siyo sana)na kulala unapojisikia usingizi. Ila pia kurahisisha mchakato unaweza tumia vidonge au kidonge cha "multivitamins" kila siku (fata masharti) mpaka uanze jisikia kawaida. Tafuta chenye vitamin B kadhaa ndani yake, hasa vitamin B1 na vitamin B12.

Unaweza pia tumia vidonge au kidonge cha vitamin B Complex kama mbadala (fata masharti). Hizi si dawa halisi bali ni vitamins tu ambazo zipo pia kwenye vyakula ila wataalam wanaziweka kwenye vidonge. Unashauriwa kuzitumia unapokua na afya duni (mfano kujifungua, ujauzito, ulevi etc) na ni kwa muda tu. Ila pia unaweza vitumia mara kwa mara kama mlo wako ni wa mashaka.
 
Shukrani sana mkuu kwa ushauri wako. Nitauzingatia maana hii vita ni kali sana🙏
 
Yaani ulichokosema mkuu ndio mimi nipitia hali hiyo mpaka inanipa wasiwasi. Tukomae mkuu tuone mwisho wake.
Ni kweli mkuu.Hivi hizi ndoto za kutisha na kuogofya zinauhusiano gani na pombe? Yaan kama mnywaji siku ukipumzika/ kuacha tu lazima ukose usingizi na ukiupata basi utashtuliwa na ndoto za ajabuajabu unazoziota mda mfupi tu baada ya kupata kausingizi.
 
Anza gym na piga mazoezi ya maana kila jioni Utasinzia tuuu.
 
Pombe husaidia kulala. Ila ukianza kuzeeka unapata tatizo la kukosa usingizi. Ni kama wakati unalewa ulilala na usingizi wa uzeeni.
 
Mimi ni mdau pia nakunywa daily pombe Kali KONYAGIIII ndogo mbili Kila jioni baada ya kazi.

Kuhusu usingizi ni sahihi...pia nikiamka asubuh kwenye kupiga mswakii Huwa napata hali ya kama kutapika IVIII nikauliza wadau mbali mbali wakajibu the same.

Natamani KUACHA ila najiuliza ntafanya nini kama sio kunywa pia natumia pesa nyingi sana kwenye uleviii / unywaji japo Mimi ni responsible ila nimechoka kwa kweriiiii NAOGOPA SANA SANAAAAAA

NB. Tukumbushane gharama za kuuguza UGONJWA /mgonjwa wa figo zipo juu sana sanaa kiasi cha watu wengi kutoweza kumudu gharama izooo
 
Yaani ndoto ya kwanza nimesinzia tu naona mti unanidondokea nikashtuka kwa kasi kama na ukwepa vile kumbe ndio naruka toka side moja ya kitanda mpaka nyingine. Usiku huo huo baadae tena nikaota gafra katokea mtu ananishushia kitu kama jiwe hivi nilipolala nikashtuka kwa kasi sana. Baada ya hapo sikulala mpaka kumi na moja na kushtuka mida ya saa moja na nusu asubuhi. Aisee wenye nia ya kuachana na maji ya dhahabu tunakazi kwakweli. Ila kuna mdau mmoja katupa moyo na kusema kuwa itachukua siku chache tu na mwili utazoea na kurudi kwenye hali yake. Tukaze mkuu😊
 
Unaachaje pombe mkuu😂
Punguza taratibu💯
On me it was just all over the suddenly maana niliamka nina hang over kali sana, mwili unatetemeka, hamu ya kula sina (Soup haipandi) nikaishia kula kula kidogo tu na kunywa maji the whole day. Shuguli ilianza usiku joto la mwili limepanda na kichwa kinagonga vibaya mno. Nikajiambia haya yote ya nini? Pesa yangu mbaya zaidi washkaji nawanunulia mimi, nikajiapia kuwa ngoja nihangaike kuuweka mwili sawa ila pombe ndio bhasi, bora hii hela ninayotumiaga huku niielekeze sehemu nyingine tu
 
Utaweza mkuu ila kuacha ghafla ndio hivo mwili unachoka ila baadaye utazoea.
Kama ungeweza kuacha taratibu ni vizuri pia,
Kama kwa siku ulikiwa unakunywa bia sita unaanza kupunguza.
Inawezekana💯
 
Ni kweli, huwa siku za kwanza usingizi utasumbua kidogo, ni sehemu ya kile kinachoitwa alcohol withdrawal, ila baada ya wiki moja hadi mbili utakikuta ubongo wako umerudi kwenye hali yake ya kawaida.
 
Mkuu kupitia coment yako ndio nimejua kumbe mwaka jana kichwa kimenisumbua kwa miezi 7 mfululizo kumbe kisa pombe kali nashangaa tangu januari hali haipo maana kila siku nilikua nabwiya panadol

Kingine ndani ya mechi nilikua na kumbana na hali ya kutokwa na jasho balaa feni inapiga lakini wap mwili unatoa jasho balaa
 
Kwanza hongera kwa hatua uliyoichukua. Fanya hivi bro. Kila siku jion hakikisha umefanya mazoezi ya kukimbia ili usweat na hapo hapo unakunywa maji kwa wingi yani maji kunywa hadi wakushangae na tena uepuke kutumia vinywaji vya kahawa kahawa ndan ya cku 3 utaona change. Kaza bro usirudi tena huko japo ukumbuke marafiki lazma wakutenge. Kama una wife mwambie ahakikishe anakupikia uji kila jion after mazoezini and you will thank me later.
 
Mkuu hii ndo ilinitokea mimi hiyo tarehe 26/04.., aiseee, ile homa sijawahi kuumwa. Mimi wakutapika mbele za watu hata kujizuia nilishindwa. Hamna chakula kinapanda hata kidogo, nikila natapika chote na hapo na kuhara kila baada ya dk10. Pombe ile nilihisi nimekunywa sumu dadeki. Hadi leo sitamani kwakweli!
 
Hiyo hali ni kawaida ukikaza utakaa sawa.

Pombe zinatusababishia matatzo sana mwilini. Akili inakua sio sawa kesho yake.
Ubaya wa pombe ni hangover, kutapika, kuharisha.

Na ukiharisha kuna muda unajikamua sana, sometime kuna misuli inapasuka unajikuta kimba linakuja na damu.

Kuna muda unaamka na hangover kazi haziendi....

Binafsi leo nmetafakari sana damage tunayojifanyia kwa hela zetu. Inaumiza sana. Kipindi flani niliweza kuacha miezi 6 nilikua productive sana.

Nmenuia kuacha tena. Nipumzike kwa muda zaidi.
Pia jihusishe na mazoezi itakusaidia mno.
 
Hapo kwenye kunywa maji mengi jioni si ataishia kushtuka kwenda kukojoa mara kwa mara usiku
 
Nimeufatilia mjadala.
Kiukweli umefanya kosa kuacha pombe ghafla,,, kwa uzoefu wa walevi kwetu kama unaacha pombe bila tatizo la lolote la kiafya anza na kupungunguza kwanza.
Kama ulikuwa unatumia 5 punguza Ziwe 3 na kama ilikuwa ni kila siku. Punguza siku za utumiaji na jipe nidhamu katika utumiaji .

Kiukweli na kama Kuna mtu anatumia spirit hizi konyagi, k -vant, value na visungura aina yoyote hakikisha unaacha mara moja kwa usalama wa afya yako.
Na hizi bia light zoote hakikisha unaziacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…