Ukisikia kusagiwa kunguni ndiyo huku sasa.
Lingekuwa ni suala la nia njema kuwatakia heri vijana wa huo mtaa, ungejumuisha na mitaa mingine yote nchini Tz.
Namaanisha hivii?: mtaa huo wakifungiwa kupika gongo, walevi wa mtaa huo watahamia mtaa mwingine kwenda kunywea na kuvutia huko.
Gongo na bhangi yamekuwa ni mapato haramu ya Polisi tangu enzi za Nyerere.
Huyo Polisi uliyemchomea utambi hapo akiacha kupika yeye, ataenda kukamata iliyopikwa mitaa mingine, ataendelea kula haramu za gongo na bhangi vile vile.
Kikubwa hapo ni kushauri sheria inayoharamisha matumizi ya gongo zaidi ya miaka 50, huku gongo hiyo ikiendelea kupikwa na kunywewa iangaliwe upya ama ifutwe.
Imekuwa ikiwanufaisha Polisi kwa mlango wa nyuma tangia itungwe.