Kuna mambo hutokea katika Uhusiano ujue mwenzi wako ni mtu wa namna gani. Huyu wangu nimegundua hana akili

Kuna mambo hutokea katika Uhusiano ujue mwenzi wako ni mtu wa namna gani. Huyu wangu nimegundua hana akili

Nimependa hiyo Haujambo ilivyokuja ghafla.🤣🤣🤣

Ila wanawake kuna muda tunazingua sana!!!😬
🤣🤣tatizo alikuwa anabwabwaja sana afu mimi sio mtu wa kupenda maugomvi.
Na mnazingua haswa, mtu unajitoa unampeenda yeye na mtoto eake lakini bado atakuona mbaya kwa kuwa mkweli tuu
Ila mpaka leo hajaniblock lakin msg hajibu
 
Dr. Unakubaliana mtoto wa miaka Saba kujikojolea?mtoto kuacha kukojoa kitandani wengi kuanzia miaka 3 wenye akili shape ni 2.8....huyo dada analea vibaya mtoto uongo ni dhambi,
Kujikojolea sio jambo la hiari ni jukumu la mzazi kumuamsha mtoto hata mara tatu usiku akojoe na sio kumchapa kuna athiri saikolojia ya mtoto.
 
Dr Restart mi natofautiana na wewe.

1. Mtoto wa miaka 7 kujikojolea sio sahihi, unless ana tatizo la kiafya. Mimi nilimchapa wakwangu akiwa na 5 ama 6 kama siokosei....na aliacha immediately maana katabia kenyewe kaliibuka out of nowhere. Watoto wana tendency yakujaribu watu kwakufanya makosa kwa makusudi pale wanapoamini they'll get away with it. Kuna mtoto wa dada yangu (12 yrs old), huwa anakojoa kitandani, tena sometimes asubuhi kushakucha. Nimeshasafiri nae mara mbili, biti analopigwa kuhusu kujikojolea ugenini huwa lina matokeo chanya, which proves nyumbani huwa anafanya makusudi maana anaeishia kugombezwa ni dada wa kazi na sio yeye.

2. Kama nimeelewa sahihi Tuta Absoluta Kantangaze alikua na malengo na mpenzi wake, so jambo la kuruhusu/taka mtoto awe sehemu ya muda wao pamoja halina ubaya wowote. Ilikua vizuri ili watengeneze bond, lakini pia imemsaidia kujua huyo dada ni mama wa aina gani. Angekuja kugundua miaka miwili/mitatu baadae wameshaongeza wakwao ingekua mbaya zaidi.

3. Jamaa haonyeshi kutokumpenda mtoto, nnachoona ni kwamba analazimishwa kumkubali na tabia zake hata ambazo sio nzuri pamoja na aina ya malezi anayopewa. Kitu ambacho sio sahihi. If we are being honest, huyo mwanamke anaweza kuona kama anamsaidia mwanae kwakumuendekeza (sio kumpenda) ila anamuharibu.

All in all, the guy is right. Kupitia maongezi yao inaonekana kabisa he's done his best, ila single mother hana shukrani wala hataki hata ku-acknowledge juhudi za jamaa. Amuache akachoshane na mtu mwingine mbele ya safari.
Naunga mkono, well said Dr
 
Ila kwa hizi conversation kama ni real hapo hakuna mtu , atakutesa wakati yeye anaona wewe unamtesa , Yani hata kama hujasoma sms zote ukisoma ya kupangiwa nyumba tu 300k unaona hapo hivi kichwa RIP

Yani hiyo 300k imenifanya nimekasirika ghafla nikasonya kumbe jirani kanisikia akajua namsonya yeye😂😂
 
Back
Top Bottom