Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Jamani nahitaji na mm hizo dawa ili nisafishe kidogo tumbo langu maana sometimes huwa linanisumbua
Kwa hapa Geita naweza Pata wapi?!
Na je nitumie ipi Kati ya hizi
Habari muluki
Castro oil
Au nikaulize kwenye maduka ya dawa za asili😳😳
Je ulifanikiwa kusafisha tumbo
 
Mkuu inachukua muda gani kumaliza manake nataka kutumia mida hii. Kesho niingie kazini au nitumie weekend? Ushauri please
Mkuu; Ukienda (yaani ukiharisha) walau mara sita na uwe unachunguza kinachotoka
na ukiona unatoa kitu kama kamasi nzito (malenda-lenda) rangi ya njano basi ujue GAME OVER! Hapo uwe umeandaa uji mlaiini wa unga wa mahindi (Dona) usitie sukari na unywe kiasi chochote kwa wingi kurudisha nguvu ndipo vyakula vingine vije baadaye - ikiwezekana uoge maana utakuwa umechoka. Hakika kesho utaenda kazini bila shida na utajisikia mwepesi. Mimi nilishaitumia hiyo kitu na Usiwe na wasiwasi nayo ila usizidishe idadi ya ulivyopewa na muuzaji.
NB:Kama ilivyotajwa hapo juu inaitwa Habbat Mulk. Inapatikana maduka ya Dawa Asili.
Kazi njema bro.
 
Salaam wana JF

Kwa wale wasafiri wa kanda ya ziwa hasa kutokana Mwanza kwenda mikoa mingine mtakua mashahidi kwa hili.

Kuna watu wanapanda kwenye basi kuanzia pale Shinyanga na kushukia Tinde au Nzega, watu hawa wamekua wakiuza Dawa mbalimbali za asili(Tiba mbadala).

Sasa Jana wakati nasafiri aliingia jamaa mmoja Ustadhi kwenye basi letu na kuanza kutangaza kuhusu Dawa anazouza.

Kuna moja ilinivutia, ni mbegu fulani kwa jina nimesahau,vmuuzaji akadai mbegu hiyi unaitafuna na kushushia na maji baada ya muda utaanza kuhisi hali tofauti mdomoni na tumboni kutaanza kuunguruma hapo sasa utaenda chooni kuharisha na utashuhudia uchafu mwingi ukitoka.

Akaenda mbali zaidi na kusema ili uamini jitahidi uharishie kwenye beseni uone mavitu yatakayotoka tumboni.

Abiria wengi walinunua nami nikashawishika kuinunua hiyo mbegu.

Sasa bado sijaitumia naomba kama kuna ambaye aliwahi kutumia hii mbegu atiririke hapa uzoefu alioupata baada ya kuitumia.

Ni hayo tu wakuu.
Ukiendaga chooni unatoaga uchafu au asali mwenzetu
 
Nitainywa hii dawa maana uzito wangu na uref haviendan
 
Salaam wana JF

Kwa wale wasafiri wa kanda ya ziwa hasa kutokana Mwanza kwenda mikoa mingine mtakua mashahidi kwa hili.

Kuna watu wanapanda kwenye basi kuanzia pale Shinyanga na kushukia Tinde au Nzega, watu hawa wamekua wakiuza Dawa mbalimbali za asili(Tiba mbadala).

Sasa Jana wakati nasafiri aliingia jamaa mmoja Ustadhi kwenye basi letu na kuanza kutangaza kuhusu Dawa anazouza.

Kuna moja ilinivutia, ni mbegu fulani kwa jina nimesahau,vmuuzaji akadai mbegu hiyi unaitafuna na kushushia na maji baada ya muda utaanza kuhisi hali tofauti mdomoni na tumboni kutaanza kuunguruma hapo sasa utaenda chooni kuharisha na utashuhudia uchafu mwingi ukitoka.

Akaenda mbali zaidi na kusema ili uamini jitahidi uharishie kwenye beseni uone mavitu yatakayotoka tumboni.

Abiria wengi walinunua nami nikashawishika kuinunua hiyo mbegu.

Sasa bado sijaitumia naomba kama kuna ambaye aliwahi kutumia hii mbegu atiririke hapa uzoefu alioupata baada ya kuitumia.

Ni hayo tu wakuu.
Weka picha Sasa tutajuaje Ni aina ipi ya mbegu uliyopewa
 
Niliwahi kutumia hii dawa. Halafu nilimeza vimbegu viwili jamani mwenzenu. Nilikaa chumbani kwangu naingia chooni kila baada ya sekunde kumi mwishowe nikavua nguo zote nikawa uchi muda wa kuvua hata kanga mwilini ulikuwa hautoshi unaweza shtukia vitu vimeshuka mapajani .

Tena niliambiwa niandae na yale madawa maalum ya watu wanaohara yanaitwa "oral" sijui nilikuwa na jug mbili zimejaa hayo maji. Yaani nikimaliza kunywa glass moja ni safari ya kukimbia chooni Baada ya masaa matatu nilihisi naaga dunia nguvu ziliisha na sauti ikagoma.

Nikitazama sink la chooni naharisha maji meupe kama kipindupindu hata hayana harufu. Nikajua hapo sasa namaliza stock ya maji ya mwilini nilitambaa hadi jikoni uchi kutafuta maji ya baridi kwenye fridge ndio pona yangu.

Ile kama utani tu unaweza kuondoka duniani kiulaini tu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Pole sana anti, hiyo ndio shida ya dawa za kienyeji huwa hazina dose maalum.--- mtu unaweza kufa kirahisi sana.
 
na hii je ni ya nini inatibu?
IMG_20210815_164009_1.jpg
 
ni moja ya dawa bora sana, na ukitaka ujue tumbo ni jalala Zaidi ya dampo, kunywa hii kitu, just be alone at home with a private toilet, hii dawa kiboko, the good thing is ukinywa maji ya baridi tu, inakata mda huohuo, lakin shughuli yake si mchezo

Dawa lakini shughuli yake si mchezo tena!!🤣
 
Haliumi lakini linavurugika mpaka basi, unaweza ukahamia chooni kabisa, lakin ikishakata you will feel different, mwili unakuwa mwepesi and more energetic

Lazima mwili uwe mwepesi kwani uharo utokao nao ni matter (maada)---- because it has mass and occupies space. 😏
 
Hiyo ni mbegu ya MIBONO ni kweli ukila utaharisha sana.Lakini swala la kuwa dawa inasafisha tumbo halina ushahadi.Mtu anapoharisha mara nyingi anaharisha vitu ambavyo amekula.Sasa angalia mtu kala mayai asubuhi saa 4 kala nyama mchana kala ugali na bamia na jioni kala pilau halafu kalala kesho anaanza kuharisha.

Hivi huo mkorogo aliokula kama ungewekwa kwenye chombo kimoja ukiuangalia unaweza kuukimbia kwa jinsi unavyotisha.Sasa hawa jamaa wa tiba mbadala wanaweza kujenga hoja za uongo kuwa dawa inasafisha tumbo kwa vile mhusika amehara uchafu. Usitegemee mtu kuhara manukato hata kama alikula biryani.

Mayai +nyama +ugali-bamia+ pilau+ digestive juices zilizomo tumboni=mseto wa ajabu.

Umesahau maji na pepsi ya kushushia.🤣
 
Mi naomba kujua Kama ukinywa hiyo alaf ukawa mjamzito wa mimba ndogo labda mwezi itahatarisha mimba kutoka? Nataka kumpa mtu atumie lkn ni mjamzito wa week tatu tu Nahofia nisije zua balaa lingine alaf nilinunua tu kwenye gari hata aikuuliza HV.

Mjamzito asile hiyo dawa. Anywe juisi ya ukwaju.
 
Nipo hapa, naendesha sina amani kabisa, nimekuja humu kucheki solution ya ku stop.
Ni tiba ndio lakini eeh kiboko.
Mpaka nimekumbuka umuhimu wa kuwa na afya njema na kujitunza wakati wote.
Tuepuke tu misosi isiyo rafiki kwa afya, na kuwa na kiasi.
 
Yaani me nimeitumia muda huu kinyeo kinawaka moto....na hakuna dalili za breki kushika....breki toka zimeachia saa saba mchana...saiv saa 12 kasoro...khaaa nifanyeje ili litulie wataalamu
 
Nimerudi tena, hii ni saa kumi alfajiri (4:02).
Nimetafuna Habat Mulk, saa nne usiku. Ninachokipitia ni hatari.

Niwakumbushe tu wadau kuwa, hii ni mbegu ya Castor. Tunaitumia kama laxative,na kwa imani kuwa kama umekula vitu sio vya kiimani basi vitatoka.

Lakini kisayansi hii kitu ina sumu inaitwa RICIN, hii sumu inaweza kutumika kama silaha ya kuua watu, na haina anti-dote.

Ukila zaidi ya mbegu moja au hata hiyo moja, ikikuta mwili kidogo hauko sawa stamina unaweza kupoteza maisha.

Tuwe makini, kwa mziki wa leo. Nadhani hii nimestaafu.
🤣🤣🤣🤣
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Habat Mulk ni mbegu ya castor?!

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom