Kuna mbinu za makusudi za kuiua Serengeti ya Tanzania na Masai Mara ya Kenya ili kukuza Dubai Safari Park kwa ajili ya utalii wa wanyama wa porini?

Hakuna mbinu za makusudi mnaziua wenyewe Mbuga zenu,mnatoa wamasai na kuleta wachimba madini mbugani,wawindaji si ukichaa huo.
Next 20 years tutakua tunaenda kushangaa wanyama kama tembo na Faru Dubai.
 
Ndio shida za nchi zisizo na mfumo imara, kila mtu chawa, kila mtu mchumia tumbo wanaogopa kusema, ina maana hata USALAMA wanashindwa kufanya majukumu yao sababu hii, yaani hawaoni ubaya wa hili jambo?

Swali la msingi tuna migodi mingapi sisi na imetusaidia kipi cha maana? Je kufanya shughuli za mgodi serengeti zitaongeza nini kwenye maisha yetu,
Hawa viongozi nibwana laana za tamaa ya mali hawatosheki nyama hawa.
 
Huyu mama anajiona ana akili kuliko Nyerere, Mwinyi, Mkapa , kikwete na Magufuli, wote hao hawajachimba ila kwakua yeye ni jiniaz basi anachimba.
Halafu hasikii la kuambiwa kwa sababu yeye ni.....
 
Jinga kweli wewe,,, kwa madini gani yanayoweza kuipeleka Tz mbali,,, kila kitu failures
 
Hakuna mbinu za makusudi mnaziua wenyewe Mbuga zenu,mnatoa wamasai na kuleta wachimba madini mbugani,wawindaji si ukichaa huo.
Next 20 years tutakua tunaenda kushangaa wanyama kama tembo na Faru Dubai.
Ni kweli kiasi fulani, lakini huoni kwamba safari hii mjomba factor imekuwa kubwa sana? Katika hili la Serengeti huwezi kusema "sisi wenyewe" tunaziua mbuga, wakati kulikuwa na msimamo mkali wa TANAPA kwamba hakuna kuchimba madini katika hifadhi yeyote ya serikali, jambo ambalo sasa limepinduliwa na raisi. Au unataka TANAPA waingie katika confrontation na raisi, watumie askari wao kuzuia kampuni yeyote ya madini kuingia mbugani kwa lengo la kuchimba madini?
 
Nachoona hata maeneo ya mashamba watachukua tutabaki tupu wakimaliza kugawa hizo mbuga..sasa makampuni ya Utalii ya nini kama huko huko tena anavuruga ina maana hayo madini yapo mbuga za Tanzania tu haoni Nchi zingine wapo makini kwenye hili swala..
Mkuu uchumi wetu utaharibika sana. Inasikitisha na kutia huzuni. Fisiumu ni janga kwa Tz
 
Mkuu uchumi wetu utaharibika sana. Inasikitisha na kutia huzuni. Fisiumu ni janga kwa Tz
Kuna msemo kwamba ukimwaga ugali na mie namwaga mboga. Sasa Nape na Makamba, wamemwagiwa ugali, labda sasa hii ni nafasi kwao kutuambia ni nini kinaendelea huko juu kuhusu mutakabali wa nchi yetu, maana tunaona kama kuna mambo ya ajabu sana yanaendelea. Kama hamuwezi kusema waambeni wale wenye uwezo wa kuchukua hatua. Ila muwe very careful, maana hata polisi, wakati hawajui watu wanatekwa na nani, wanasema sio wao wanaoteka.

What is going on, tuko salama kweli, nchi na mananchi mmoja mmoja?
 
Tuliambiwa hivi hivi kwenye tanzanite, gesi nk nk
 
Kwa ukubwa wa Serengeti kama 10% tu ya eneo lake litakuwa na madini either dhahabu au madini ya Vito kama safire n.k basi ni heri yachimbwe tu. Mapori yako mengi. Artificial safari ya Dubai haitaweza kushindana na Tanzania yenye hifafhi kama utitiri.
Vurugu na sumu za uchimbaji kwa wanyama zitaenea zaidi ya hizo 10%. Athari zake kwa utalii zitachafua Serengeti yote na si hizo 10% tu.
 
Uzuri au ubaya ekolojia ya Serengeti inafika hadi Masai Mara Kenya. Na tunawajua vizuri wakenya kwa kupiga kelele, hili watalivalia njuga.
 
mkuu hoja yako ni ya msingi, kukukumbusha tu hili suala halijaanza leo wala jana, kuna wakati kulikua mpaka na mkono wa CDF mmoja hivi, lakini usijali suala hili halitakua na mwisho mwema. Tamaa ya pesa haiwezi kutufanya kama taifa tukakengeuka, kama ni madini hatujaanza kuchimba leo.
 
Nafurahi kuona bado tuna sauti kama hizi nchini!
 
aisee umeandika kilekile nilichotaka kumuandikia huyo kilaza wahedi.
 
Pale stone town si kuna madini pale? Kwanini hawachimbi? Au yale madini wanachanganyia kwenye urojo na kula supu?
 
Wewe sio mtanganyika wala muafrika .
Huna uchungu na rasilimali za asili za nchi hii.
Kenya wamejikomboa kwa sasa baada ya kuona kuwa wanasiasa ni maajenti wa shatani kuharibu Uumbaji wa Mungu.

Huyu mama na hii katiba inayompa mtu mmoja mamlaka makubwa kuliko Mungu ni hatari sana kwa taifa la leo na kesho na vizazi vyote vijavyo.
Tuna katiba ya hovyo sana. Katiba isiyokuwa na uwezo wa kumzuia mtu mmoja kwa malengo yake na ndugu zake huko Omani kupoteza uzalendo ,umoja,uhuru, uchumi ,ulinzi na rasilimali za nchi.

Ni upumbavu mkubwa sana kuchimba madini kwenye mbuga za wanyama .

Madini tangu yameanza kuchimbwa Afrika na Wazungu wadau wa mama hayajainua uchumi wa nchi.

Madini hua yanwanufaisha watu wanaozungu eneo la machimbo tu lakini sio serikali. Matani ya madini yanayobebwa geita Kahama n.k yangeweza kuendesha bajeti ya nchi na kuinya thamani ya pesa yetu lakini wapi ni wachache wanajinufaisha tu .

Kongo madini ni laana kwao na sasa Mama anakaribia kuleta laana Tanganyika. Huyu mtu na Wazungu wake na waarabu wake wana chuki kubwa sana na Watanganyika.
Vyombo vyote vya dola ,mahakama,bunge ,chama, watanganyika mil.65 wote waleifyata wanamuangalia mtu mmoja analiingiaa taifa kwenye madeni makubwa, anauza bandari ,anauza mbuga za wanyama anauza kila kitu hasa maliasili.
Ina maana yeye ana nia nzuri kuliko Watanganyika wote waliomtangulia au kuna nini nyuma yake? Kwanza hakuwahi kuwa na vision ya kugombea urais sasa hiyo dira ya maana kwa Tanganyika ameipata wapi na kwa maono yapi aliyokua nayo katika siasa zake?

Amewahamisha Wamasai ili Waarabu wajenge mahoteli na viwanja vya ndege Loliondo na sasa anahamisha Wanyama kijanja kujanja kwa kuanzisha viwanda katikati ya mbuga ya wanyama na kuacha mashimo ya machimbo na ukame na jangwa Serengeti.

Huyu mtu asipewe hata fomu ya kugombea 2025.

Kama yeye ni mtaalamu wa kujenga uchumi basi akajaribu kuvunja katiba ya Zanzibar na kuwa mwanamke Rais katika nchi ya kiislam!!
Au kwao Omani .

Hata Obama alikua na asili ya Kenya lakini hakutumia urais wake kuhamisha uchumi na rasilimali za Marekani kupeleka au kuifavour Kenya.
 
Mkuu kweni Chama kinacho isimamia Serikali inasemaje juu hili? Je SERA hii ilikuwemo kwenye Mipango yao ya Muda Mfupi ama Mrefu? Jamani tujuzeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…