Kuna fukuto kubwa Ndani ya chadema kuwa uamuzi wa chairman wa Chadema kuamua wabunge wote wa Chadema waingie karantini zimeleta sintofahamu kwa wabunge wengi wa chama hicho
Baadhi ya wabunge wa Chadema wamelalamika kutokushirikishwa katika maamuzi yaliyochukuliwa na chairman Mbowe
Kuna wabunge wa Chadema wanalalamika kuburuzwa kila mara, Wengi wanaona kutokuhudhuria vikao vya bajeti ni kama kuwasaliti wapiga kura wao
Kwa inavyoonekana Chadema ni km bomu linalosubiria kulipuka
My take :chairman kuwa mwanademokrasia acha maamuzi ya kibabe lasivyo chama kitasambaratika
Naamini kuna tatizo katika vichwa/akili za viongozi wa juu wa CHADEMA. Wanachama na Wafuasi wao, ndani na nje ya chama. Siamini kama Mbowe tu ndiye anayewaburuza labda hata viongozi wenzake ni walemavu wa akili. Mifano iko mingi kutetea hoja hii.
1) Bunge la Katiba, walisusa vikao na kuunda UKAWA ambao umesaidia tu kukijenga CHADEMA.
2) Bunge la kwanza, kwenye utawala wa Rais Magufuli, walisusia kusikiliza hotuba yake. Kwa mtu mzima, makini, mwenye hekima na busara, kiongozi aliyechaguliwa na watu kuwawakilisha kwenye chombo kimojawapo cha juu katika Dola, na anaheshimu dhamana hiyo, asingefanya hivyo. Japo walitoka bungeni ni wazi waliendelea kusikiliza hotuba hiyo nje ya bunge na ndiyo maana wamekuwa wakirejea baadhi ya hotuba hiyo kwenye mijadala yao ya madai mbalimbali yenye msingi wa ubinafsi na siyo Taifa. Wanayaimba kila siku kama ndege kasuku.
3) Mara nyingi wamekuwa wakisusia vikao vya bunge vya bajeti ili hali wakidai majimbo yao yapate maendeleo. Pamoja na kususia vikao hivyo bado Serikali huwalipa mishahara, posho na pesa ya mfuko wa jimbo ambayo baadhi ya wabunge huitumia kwa maslahi binafsi.
4) Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mtukufu Mbowe aliwaagiza wagombea wote kususia na wakatii bila kuuliza kulikoni na madhara yatokanayo na kufanya hivyo.
5) Jana, M/Kiti wao, Mtukufu Mbowe, tena kawaagiza kususia kikao cha bajeti wakajifungie kwenye makazi yao hapo Dodoma, na wala wasiende kwenye majimbo yao, ati kwa kuogopa kuambukizwa COVID-19 kana kwamba hao wabunge wana akili za kitoto zisizojua athari za kutojikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko na usalama wa maisha ukibaki mikononi mwa wazazi.
6) Bila kusahau wanaCHADEMA, wakati wa Uchaguzi Mkuu, 2015, walivyokuwa wanazungusha mikono (ati ndiyo mabadiliko) na kupiga deki barabara ili Mabwana zao wapite.
Ni wazi kabisa, pasipo na shaka Mbowe ni BABA LAO. Na viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wamebaki kulamba na kumeza kila linalosemwa na kutendwa na Mtukufu wao Mbowe.