Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ikiwa wanaokunywa wewe wanajinyea, wewe mwenyewe hali yako itakuwaje?
Naamini kuna tatizo katika vichwa/akili za viongozi wa juu wa CHADEMA. Wanachama na Wafuasi wao, ndani na nje ya chama. Siamini kama Mbowe tu ndiye anayewaburuza labda hata viongozi wenzake ni walemavu wa akili. Mifano iko mingi kutetea hoja hii.
1) Bunge la Katiba, walisusa vikao na kuunda UKAWA ambao umesaidia tu kukijenga CHADEMA.
2) Bunge la kwanza, kwenye utawala wa Rais Magufuli, walisusia kusikiliza hotuba yake. Kwa mtu mzima, makini, mwenye hekima na busara, kiongozi aliyechaguliwa na watu kuwawakilisha kwenye chombo kimojawapo cha juu katika Dola, na anaheshimu dhamana hiyo, asingefanya hivyo. Japo walitoka bungeni ni wazi waliendelea kusikiliza hotuba hiyo nje ya bunge na ndiyo maana wamekuwa wakirejea baadhi ya hotuba hiyo kwenye mijadala yao ya madai mbalimbali yenye msingi wa ubinafsi na siyo Taifa. Wanayaimba kila siku kama ndege kasuku.
3) Mara nyingi wamekuwa wakisusia vikao vya bunge vya bajeti ili hali wakidai majimbo yao yapate maendeleo. Pamoja na kususia vikao hivyo bado Serikali huwalipa mishahara, posho na pesa ya mfuko wa jimbo ambayo baadhi ya wabunge huitumia kwa maslahi binafsi.
4) Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mtukufu Mbowe aliwaagiza wagombea wote kususia na wakatii bila kuuliza kulikoni na madhara yatokanayo na kufanya hivyo.
5) Jana, M/Kiti wao, Mtukufu Mbowe, tena kawaagiza kususia kikao cha bajeti wakajifungie kwenye makazi yao hapo Dodoma, na wala wasiende kwenye majimbo yao, ati kwa kuogopa kuambukizwa COVID-19 kana kwamba hao wabunge wana akili za kitoto zisizojua athari za kutojikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko na usalama wa maisha ukibaki mikononi mwa wazazi.
6) Bila kusahau wanaCHADEMA, wakati wa Uchaguzi Mkuu, 2015, walivyokuwa wanazungusha mikono (ati ndiyo mabadiliko) na kupiga deki barabara ili Mabwana zao wapite.
Ni wazi kabisa, pasipo na shaka Mbowe ni BABA LAO. Na viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wamebaki kulamba na kumeza kila linalosemwa na kutendwa na Mtukufu wao Mbowe.
Kama Kujiweka Quarantene ni kukurupuka ,Kuazimisha NYUNGU ambapo hakuna mchanganyo( Ingridients) maalumu, Kila mtu anajichagulia majani yake na kuchanganya atakavyo,Hali kadhalika NYUNGU pia jichagulie saizi yako bila kujali chochote mwengine la kilo 2,3,5, Haina fomula .....
Kwenye hili hujaona UJUHA wala UKURUPUKAJI?,
Ushauri :-
Tuyape yote Nafasi na baadae tufanye Tathmini lipi ni la KIBWEGE na Lisilo na MAARIFA.
Simple logic ni kuwa mkusanyiko wowote wa watu huwa ni kichocheo kwa covid 19 na hivyo huendea kwa haraka zaidi.Umeona wabunge waliofariki ni watatu na hao wengine watakuwa kumi na tatu, ilà wabunge wametajwa kwa sababu ni wabunge. Hao kumi na tatu kiuhalisia wanaweza kuwa wengi zaidi, sina facts hivyo nasema HUENDA!!
Tuambie Mzee Baba alipo ndipo tutaelewa ujemedari wa wabunge wa CCM na mwenyekiti wao,si yeye pia ni sehemu ya Bunge?Wanakimbia vita kwamba watanzania wapigane wenyewe chini ya majemedali wa CCM.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umeona wabunge waliofariki ni watatu na hao wengine watakuwa kumi na tatu, ilà wabunge wametajwa kwa sababu ni wabunge. Hao kumi na tatu kiuhalisia wanaweza kuwa wengi zaidi, sina facts hivyo nasema HUENDA!!
Wewe acha ukichaa Rais huwezi mlinganisha na Mbunge!! Rais ni nembo ya nchi analindwa sana tu kama kuna tatizo lolote nchini yeye anakuwa wa mwisho kuumizwa unafikiri Rais anatakiwa kuwa mbele? Haijawahi tokea duniani labda kwenye Saccos ya Chadema!
Hata kama wabunge wa CHADEMA wasingeamua kuchukua hatua ya kujitenga na vikao vya bunge, bado ingebaki kuwa uamuzi sahihi bunge kubadili namna ya kuendesha vikao.
Hivi unahitaji ishara gani kuamini kuwa ndani ya bunge kutakuwa na maambukizi ya kutosha tu!
Nina mashaka Tanzania tuna tatizo la kimsingi tusilolijua na kwamba utatuzi wake ni mgumu au sintofahamu isiyo mithilika.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wabunge ni watu wazima, viongozi walioaminiwa na wananchi, wakapewa dhamana ya kuwawakilisha kwenye chombo cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali, wanapaswa kuwa na maamuzi binafsi ya mfano wa kuigwa walio wachaguwa.
Mbowe, kama Mbunge na KUB, na M/Kiti wa Chama Kikuu cha Upinzani, angepaswa kutumia madaraka hayo kuwasilisha hoja yake hiyo bungeni, badala ya kutoa maagizo kupitia vyombo vya habari.
Kwa agizo hilo na njia aliyoitumia, Mtukufu Mbowe ameonesha dharau ya wazi kwa viongozi wenzake, Bunge, Wanachama wa CHADEMA, wapiga kura, na Watanzania wote kwa ujumla. Mbowe, pia ameonesha makucha yake ya udikteta. Yumkini ndiyo maana viongozi wanahama chama CHAKE.
Mtukufu Mbowe, anathibitisha kuwa mtu hatari kwa amani katika Taifa. Kauli na matendo yake ni wazi yanahusika, pasipo shaka sasa, na matukio mbalimbali ya uhalifu ndani ya chama CHAKE km kupotea, kupigwa risasi na hata la maandamano haramu yaliyosababisha kifo cha Akwilina.
Selasini, Mb, wakati akitangaza kukihama chama cha Mtukufu Mbowe amedokeza machache tu ya kumhusu. Tutegemee mengi machafu na maovu ya kutisha kutokea ndani ya CHADEMA na jamii, kwenye uenyekiti wa Mtukufu Mbowe.
Haijafikia Demokrasia iliyoko CHADEMA ya kuwaacha kina Selasini na Komu kuendelea kuwa CHADEMA wakati wameshatangaza kuwa watahamia NCCR-Mageuzi!!Hiyo ni demokrasia iliyokomaa